Masha alimpigia simu ngombea wa chadema wanje kumuomba asigombee ubunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masha alimpigia simu ngombea wa chadema wanje kumuomba asigombee ubunge

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Japhari Shabani (RIP), Sep 12, 2010.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sokomoko sasa yazuka CCM Mwanza

  Mwandishi Wetu Septemba 8, 2010

  Kurejeshwa mgombea wa CHADEMA kwanza kutafuna
  UAMUZI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumrejesha kwenye kinyang’anyiro mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Nyamagana, Ezekiah Wenje, umeongeza mpasuko mkubwa katika Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza kutokana na mmoja wa viongozi waandamizi wa chama hicho kudaiwa kuhusika kufanikisha rufaa iliyokatwa na mgombea huyo wa CHADEMA.
  Awali msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Nyamagana, Wilson Kabwe, alikubuliana na pingamizi la Lawrence Masha dhidi ya mpinzani wake huyo pekee hivyo kufanya waziri huyo wa Mambo ya Ndani kupita bila kupingwa.
  Katika pingamizi lake Masha kwanza alidai kuwa Wenje si raia wa Tanzania; hakuwasilisha tamko la kisheria kuthibitisha yale aliyojaza kwenye fomu za kugombea kama inavyotakiwa; mgombea Wenje alidai kuwa ni mkazi wa Burola A wakati si kweli kwani hana makazi katika mtaa huo na kwamba mgombea huyo pia alisema uongo juu ya cheo chake katika ajira pamoja na kushindwa kujaza fomu ya kugombea kama inavyotakiwa.
  Hata hivyo, katika maamuzi yake kupitia barua yenye kumbukumbu Na: AE 74/141/02/4 iliyosainiwa na Mkurugenzi wa NEC, Rajabu Kiravu, Tume hiyo ilikubaliana na rufaa iliyokatwa na Wenje hivyo kumrejesha kuwa mgombea halali katika Jimbo la Nyamagana.
  Siku moja kabla ya uamuzi huo wa NEC kutangazwa rasmi, habari zilivuma jijini Mwanza huku ujumbe wa simu ukisambazwa ukisema kwamba “Wenje ameshinda rufaa yake na sasa Masha amepata mpinzani”.
  Habari na ujumbe huo zinamhusisha kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM mkoani hapa kwamba alikuwa nyuma ya jitihada zote zilizomsaidia mgombea huyo wa CHADEMA kukata rufaa na hatimaye kushinda, ikiwa ni baada mgombea aliyetakiwa na kiongozi huyo na kundi lake kushindwa vibaya kwenye kura za maoni za CCM.
  Inaelezwa kuwa suala la ukabila bado linaendelezwa ndani ya uongozi wa CCM mkoani hapa na kwamba katika kura za maoni wapinzani wakubwa wa Masha walikuwa wanaungwa mkono na kundi linalopendelea ‘wazawa’ kwa maana ya Wasukuma, lakini likashindwa vibaya na Waziri huyo wa Mambo ya Ndani.
  Ni kutokana na kushindwa huko, kundi hilo ambalo liliasisiwa na wafanyabiashara na matajiri wa kabila hilo walioko Mwanza na kupata nguvu kubwa kifedha kuanzia miaka ya 90, lilitaka kuhakikisha kuwa Masha angalau anapata mpinzani mwenye nguvu.
  Kupitishwa kwa Masha kama mgombea asiye na mpinzani inaelezwa kuwa ilikuwa pigo kubwa la pili kwa kundi hilo hivyo kudaiwa kumsaidia Wenje kukata rufaa kupinga maamuzi ya msimamizi wa jimbo hilo.
  “Suala hili la ukabila ndilo lilikuwa mtaji wa kumwangusha Masha wakati wa kura za maoni ndani ya chama. Ukiangalia wapinzani wake wakuu walikuwa ni wa kabila moja la Wasukuma. Na mwaka 2005 baada ya Masha kumshinda kwenye kura za maoni aliyekuwa mbunge wa jimbo hili (marehemu Stephen) Kazi ) kundi hili hili lilimsaidia mgombea wa CUF (Omar) Mbalamwezi hivyo kuonekana tishio. Hivyo mambo haya haya ndio yanaendelea,” anasema kiongozi mmoja wa CCM Wilaya ya Nyamagana ambaye hakutaka jina lake litajwe.
  Katika kura za maoni Masha alishinda kwa kupata kura 8,627 huku wapinzani wake wa karibu wakiwa ni Malogoi Mboje aliyepata kura na 2,420, na Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza, Joseph Kahungwa, aliyepata kura 1,941.
  Kahungwa ndiye alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kumshinda Masha lakini aliambulia nafasi ya tatu kwa tofauti ya kura nyingi na Masha.
  Uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kuwa siasa za makundi ndani ya CCM mkoani Mwanza ziliongezeka kuanzia wakati wa uchaguzi wa viongozi wa CCM mwaka 2008 hasa upande wa viongozi wa wilaya na mkoa na mwaka huu wakati wa kura za maoni za wagombea udiwani na ubunge huku vigogo kadhaa wakijitahidi kuimarisha ngome zao za kisiasa.
  Baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM Wilaya ya Nyamagana na Mkoa wameiambia Raia Mwema kuwa kuna ushahidi wa kimazingira kuwa kiongozi huyo mwandamizi kwa kushirikiana na baadhi ya wafanyabiashara ‘walimsaidia’ Wenje kukata rufaa na hatimaye kurejeshwa na NEC kwenye kinyang’ayiro hicho cha Ubunge Jimbo la Nyamagana.
  “Labda nikwambie tu kwamba katika suala ambalo liliwanyima usingizi hawa watu (wapinzani wa Masha ndani ya CCM) ni kuona Masha anapita bila kupingwa. Wametumia fedha nyingi kwenye kura za maoni lakini akawashinda, sasa wakaona haiwezekani akose upinzani wakati kundi lao karibu wote wana upinzani. Kwa hiyo wamemsaidia Wenje ili ampe Masha upinzani lakini kwa chama hili ni pigo kubwa kwani tulishahesabu jimbo letu la Nyamagana na Kata ya Nyamagana hivyo inabidi sasa tujipange upya na hizi ni gharama tena,” anaongeza kiongozi huyo.
  Aidha inaelezwa kuwa kiongozi huyo ambaye ndiye kinara wa mipango mingi inayofanywa na kundi hilo kwa misingi ya ukabila hana uhusiano mzuri na Masha na kwa muda mrefu wamekuwa wakisigana katika masuala mbalimbali ya kisiasa mkoani hapa.
  Kiongozi mwingine wa CCM mkoani hapa anasema kuwa wamefuatilia kwa karibu suala hilo la rufaa ya Wenje na kujiridhisha kuwa kulikuwa na mkono wa kigogo huyo na kwamba jambo hilo liko wazi na hata nguvu ya mgombea huyo wa CHADEMA inatokana na kuungwa mkono na baadhi ya viongozi wa CCM na matajiri wa jijini Mwanza.
  “Kuna taarifa kuwa walikuwa wakifanya vikao vya siri na mgombea wa CHADEMA. Na walimsaidia katika kila hatua. Hata siku mbili kabla ya Tume kutangaza rasmi maamuzi yake juu ya rufaa ya Wenje, tayari kiongozi huyu alituma ‘message’ (ujumbe mfupi wa simu) kwa baadhi ya watu kuwajulisha kwamba Wenje ameshinda rufaa yake na Masha lazima apate mpinzani. Hii inaonyesha alivyofurahia uamuzi huu,” anasema kiongozi huyo bila kutaka kutajwa.
  Kwa mujibu wa barua hiyo ya NEC, kikao kilichopitia rufaa ya Wenje kilifanyika tarehe 26.8.2010 wakati barua ya kuwajulisha Masha na Wenje juu ya uamuzi huo iliandikwa tarehe 29.8.2010.
  Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Musa Matoroka anasema kuwa wanakubaliana na uamuzi wa NEC ingawa wanashangazwa na hatua ya Tume hiyo kuzingatia kipengele kimoja tu cha uraia wakati katika pingamizi la mgombea wao Masha kulikuwa na vipengele sita.
  Kuhusu habari kuwa kuna kiongozi mmoja mwandamizi mkoani hapa ambaye alimsaidia Wenje, Katibu huyo anasema: “ Na sisi hilo suala la kushikana miguu tunalisikia lakini kwa sasa hatuwezi kulithibitisha kwani hatuna ushahidi ila tunalifanyia kazi”.
  Matoroka anasema pia kuwa rufaa ya Wenje ilikatwa nje ya muda na kwamba haikupitia kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Nyamagana kama inavyotakiwa.
  Naye katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Alhaji Yahaya Mwangi Kundya, anasema kuwa kama chama bado hawana uhakika na suala hilo ingawa anakiri kuwa wanasikia habari hizo kwani zimeenea sana mitaani.
  “Hatuna uhakika na jambo hilo. Na sisi tunasikia tetesi hizo, lakini hatujapata ushahidi hivyo tunaogopa kufukuzana na kivuli. Tukipata ushahidi tutachukua hatua kwa mujibu wa kanuni za chama kwa wale wanaokisaliti… maneno mengi huwa yanasemwa, mengine huwa ya uongo na mengine huwa yana ukweli lakini katika hili hatujapata mtu wa kutupa ushahidi.
  “Na kichama hatujapokea malalamiko rasmi kutoka kwa mwanachama yeyote ili tuweze kulifanyia kazi rasmi. Lakini hata kama tukipata malalamiko, tutayashughulikia baada ya uchaguzi kwani lengo letu kwa sasa ni kushinda uchaguzi hayo mengine yatafuata baadaye. Tulikwisha kujiandaa kuingia kwenye uchaguzi na Wenje hatuna shaka naye kabisa. Tutamshinda mapema asubuhi. Hayo mengine (ya kushikwa miguu) hayatusumbui kwa sasa kwani ushindi uko wazi,” anasema Kundya.
  Kwa upande wake Masha anakiri kusikia taarifa hizo lakini anasema hivi sasa amejikita zaidi katika uchaguzi baada ya uamuzi huo wa Tume na kwamba hana mpango wa kwenda mahakamani kupinga uamuzi huo.
  “Ninaheshimu uamuzi wa Tume ingawa kwa upande mwingine haukuwa fair (wa haki). Sina mpango wa kuupinga ila ninaingia kwenye uchaguzi na nina hakika kuwa nitaibuka kidedea tena kwa kishindo.
  “Hayo mengine (ya kuhujumiwa) nami nayasikia tu, ila huu si muda wa kutafuta mchawi. Ni kuingia kwenye uchaguzi ili wananchi wenyewe waamue. Hayo mengine kwakweli siwezi kuyazungumzia kwa sasa,” alisema Masha.
  Habari za uhakika zinasema kuwa huenda suala hilo limefikishwa kwa viongozi wa juu wa CCM na huenda likafanyiwa kazi baada ya uchaguzi kumalizika ambapo kwa kawaida chama hufanya tathmini ya uchaguzi na wale waliokisaliti hujadiliwa na pengine kuchukuliwa hatua ingawa inakuwa vigumu kuwachukulia hatua viongozi waandamizi wanaodaiwa kukisaliti chama.
  Hata hivyo, kitendo cha mgombea urais wa CCM Jakaya Kikwete kumtangaza Masha kama mbunge mteule wakati wa ziara yake ya kampeni mkoani hapa kimezua maswali mengi kwani wakati anafanya hivyo tume ya uchaguzi ilikuwa haijatoa maamuzi juu ya rufaa ya Wenje huku baadhi ya watu wakisema huenda mgombea huyo anapewa taarifa potofu.
  Kwa upande wake, Wenje anakanusha kusaidiwa na kigogo wa CCM mkoani hapa katika rufaa yake bali alisaidiwa na wanasheria wa CHADEMA wakiongozwa na Mabere Marando.
  “Hayo yanayosemwa kuwa nimesaidiwa na kigogo wa CCM mimi siyajui. Hayo ni matatizo yao CCM wenyewe hivyo mimi siwezi kuwaingilia. Wanajuana wao wenyewe na tofauti zao. Mimi nilisaidiwa na wanasheria wetu wa CHADEMA, wakiongozwa na Marando,” anasema.
  Kuhusu kukata rufaa nje ya muda pamoja na kushindwa kupitisha rufaa hiyo kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo lake, Wenje anasema: “Kabwe (msimamizi) alikataa kupokea rufaa yangu kwa madai kuwa nilichelewa dakika mbili wakati yeye ndiye alichelewa kutupa fomu Na. 12 ili tukate rufaa. Na hilo wanalosema Tume haikuzingatia vigezo vingine katika pingamizi la Masha, wajue kuwa kigezo kikubwa kilikuwa ni uraia wangu na hayo mengine hayakukidhi vigezo vya mimi kuenguliwa. Hivyo baada ya ku-prove (kuthibitisha) mimi ni raia halali wa Tanzania Tume ilinirejesha”.
  Wakati wa mchakato wa kuchukua fomu Wenje alimtuhumu Masha kutumia nafasi yake ya uwaziri kumtishia juu ya uraia wake pamoja na kumtaka ajitoe katika kinyang’anyiro hicho kwa ahadi kuwa angemsaidia kurudi kazini kwani angepoteza ajira kwa kitendo chake cha kujiingiza katika siasa kinyume cha sera za mwajiri wake.
  Masha alikiri kumpigia simu Wenje kumwomba asigombee lakini
  akakana kutumia vyombo vya dola kumtishia pamoja na kufuatilia uraia wake.
  Katika hatua nyingine Wenje anasema atazindua kampeni zake Jumamosi hii kwa kufanya maandamano makubwa ya magari ambapo atapita katika kata zote za Jimbo la Nyamagana kabla ya kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika Uwanja wa Sahara.
  “Nakuja rasmi Mwanza tarehe 11 mwezi huu. Nitapokewa kwa maandamano makubwa ya magari kuanzia Airport na kupita kata zote za Jimbo la Nyamagana kuwasalimia wananchi. Baada ya hapo tutafanya mkutano mkubwa wa hadhara kwenye uwanja wa Sahara. Atakuwepo (John) Shibuda, (Zitto) Kabwe, (Wilfred) Rwakatare, Mwita Waitara na Godbless Lema,” alisema.
  Kwa upande wa CCM, Katibu Matoroka anasema kuwa hawajapanga uzinduzi wa kampeni zao kwani wanasubiri ziara ya kampeni mgombea mwenza wa CCM Dk. Mohamed Gharibu Bilali itakayoaanza kesho Alhamisi.
  Kwa vyovyote vile, kurejeshwa kwa Wenje kutafanya uchaguzi kuwa na msisimko mkubwa Jijini Mwanza hata kama yeye mwenyewe si maarufu kabisa hapa, lakini chama chake cha CHADEMA kinaonekana kuwa mvuto katika jiji hilo.
   
 2. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #2
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kama mtu amabae ananafasi yajuuu katika serikali na ndiye mlinzi namba moja wa raia wote (WAZIRI MASHA)Anampigia simu mgombea kutoka chama cha upinzani kumtishia na kumuomba asigombee ubunge,hata kama hakumtishia kitendo cha kumpigia simu na kuomba asigombee na kutoa ahadi za kumsaidia .Wachambuzi wa sheria hii imekaaje?INANUKIA KOSA LA JINAI KWA WAZIRI MASHA MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  there is so much trouble in the world, lakini siasa ni balaa
   
 4. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  :confused2::confused2:huyo ndiyo alikuwa waziri wetu wa mambo ya ndani, kweli tuna kazi.....nchini
   
 5. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Ndio tabia yake Masha na hawezi kuiacha kwani kenge haachi mila zake mpaka atokwe damu ya masikioni ambapo sasa tayari masha kajaa tele kwenye kikaango cha Chadema (+ CCM), hakuna kingine bali ni kitu kimoja tu ambacho Masha amebaki nacho ili ashinde uchaguzi wa Nyamagana nacho ni kuiba kura/matokeo kwa njia yoyote ambapo nahisi atawatumia maPolisi wetu na kuwahonga mawakala kwa gharama yoyote ile...lakini kwa mjini Mwanza?...sijui na tusubiri 31/10/10
   
 6. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2010
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Na hiyo ahadi ya kumsaidia asipoteze ajira yake ina tafsiri gani kwenye hiyo sheria yao kimeo ya uchaguzi?
   
 7. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hawa daima wanadhani mkwala anapigika mtu anajitawala kiakili, ndiyo walopotezea sasa
  thy show how stupid thy are, shame on them!
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huyu ndiyo tuliambiawa ni a new generation type of a leader, na kwamba Tanzania tuna bahati aliamua kusettle bongo azawaizi tungekuwa tunamsikia tu, Can someone predict what will January bring about???????
   
 9. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Only in Tz, nchi za watu kwisha habari yake. Pona yake CHADEMA ishindwe.

  Mungu ibariki Tanzania
   
Loading...