Masha agonganisha serikali na Ujerumani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masha agonganisha serikali na Ujerumani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, May 3, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,760
  Likes Received: 83,063
  Trophy Points: 280
  • Atuhumiwa kutumia madaraka vibaya
  • Ubelgiji nayo kukoromea serikali

  Na Saed Kubenea
  MwanaHALISI-Maslahi Ya Taifa Mbele

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha ameingiza serikali katika mgogoro mkubwa na wafadhili kutokana na madai ya matumizi mabaya ya madaraka, MwanaHALISI limeelezwa.

  Masha anatuhumiwa kupendelea raia wa Ubelgiji, Brigitte de Floor, katika mgogoro kati yake na Wiebke Gaetje ambaye anatoka Ujerumani, jambo ambalo limeingiza serikali katika mgogoro wa kidiplomasia.

  Brigitte de Floor na Wiebke Gaetje ni wajane wa Klaus Gaetje ambaye anatoka Ujerumani. Klaus Gaetje ambaye alikuwa mfanyabiashara mkoani Mwanza, alifariki dunia katika mazingira ya kutatanisha Julai 2004 huko Port Bell, nchini Uganda.

  Waziri Masha anatuhumiwa na Wiebke Gaetje kuwa kikwazo katika upatikanaji wa urithi wa mume wake.

  Gaetje anadai kuwa kampuni ya uwakili ya Masha, IMMMA Advocates, imehusika katika kushughulikia baadhi ya nyaraka ambazo zimesaidia “kupora mali” ya marehemu mume wake.


  Miongoni mwa mali ambazo Masha anatuhumiwa kusaidia Brigitte de Floor kupora ni vivuko vitatu, viwanja vinne na “baadhi ya magari ya kampuni.”

  Vivuko vinavyohusika ni Kamanga, mv Uzinza na mv Karumu. Vyote viko katika eneo la Kamanga.

  Taarifa kutoka ubalozi wa Ujerumani nchini zinasema tayari serikali ya Ujerumani imelalamikia hatua hiyo ya waziri Masha ikiiita, “Matumizi mabaya ya madaraka.”

  Naye Ofisa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa jijini Dar es Salaam, ambaye aliomba jina lake lisiwekwe wazi, alithibitisha kwamba “serikali ina taarifa hizo.”

  Klaus Gaetje na Wiebke Gaetje walifunga ndoa tarehe 12 Oktoba 1979 nchini Ujerumani na kuzaa mtoto mmoja wa kiume, Mark Gaetje (28). Mtoto huyo na mama yake wanalalamikia Masha kushirikiana na Brigitte de Floor kutapanya mali yao.

  Kwa sasa, Mark Gaetje anaishi Uholanzi na alitarajiwa kuwasili nchini juzi, Jumatatu saa nne usiku kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uholanzi (KLM) ili kushughulikia suala hilo. Tayari mama wa Mark amewasili nchini.

  Mgogoro huu uliomuingiza Masha katika kashifa nyingine, umetokana na hatua ya Brigitte de Floor, ambaye anajiita mjane wa Klaus Gaetje kudaiwa kugushi baadhi ya nyaraka ikiwamo cheti cha ndoa na wosia kwa lengo la kujimilikisha mali hizo.

  Cheti cha ndoa kinachodaiwa kugushiwa ni Na. E 087887 kinachoonyesha kuwa kimetolewa 10 Oktoba 1999 wilayani Magu, mkoani Mwanza. Kimesainiwa na Msajili Msaidizi wa Ndoa, Anthony Jakonyango.

  Hata hivyo, katika hati yake ya kiapo ya 5 Julai 2008 mbele ya kamishina wa viapo, Elias Kitwala, ambayo gazeti hili linayo nakala yake, Jakonyango anakana kufungisha ndoa hiyo; anasema cheti hicho ambacho waziri Masha anang’ng’ana nacho kimegushiwa.

  Anasema, “Mimi nilihama Magu, 20 Mei 1999 kwenda Bukoba, mkoani Kagera. Hivyo kwa vyovyote vile, nisingeweza kufungisha ndoa Magu 10 Oktoba 1999.” Jakonyango anasema cheti cha ndoa anachodaiwa kusaini siyo halali.

  MwanaHALISI limefahamishwa kwamba kwa msaada wa Masha, Brigitte de Floor amefanikiwa kumuondoa Mark na mama yake Wiebke Gaetje katika umiliki wa hisa za kampuni ya Kamanga Ferry Limited (KFL).

  Katika nyaraka kadhaa ambazo ziko mikononi mwa MwanaHALISI, Masha amesaini, kama Katibu wa kampuni ya Kamanga Ferry Limited huku kampuni yake ya IMMMA Advocates ikithibitisha baadhi ya nyaraka ukiwamo wosia wa marehemu Klaus Gaetje.

  Tayari wosia huo umelalamikiwa na mke wa kwanza wa Klaus Gaetje, Wiebke na mtoto wake Mark kwa hoja kwamba mke wa pili Brigitte de Floor amegushi.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka Idara ya Uhamiaji, Brigitte de Floor aliingia nchini kama mtalii na amekuwa akiishi nchini bila kibali cha kufanya kazi, lakini kutokana na mahusiano yake na Masha, serikali imeshindwa kumchukulia hatua.

  Taarifa zinasema tayari mipango inasukwa ili kumpatia mama huyo kibali cha kuishi nchini ili kuendeleza kile kinachodaiwa na Wiebke, “urafiki wa damu na waziri Masha.”

  Anasema, “Ninajua ukaribu wa familia ya Masha na de Floor. Baba yake Masha amekuwa akipewa misaada na de Floor. Tayari ameipa familia hiyo viwanja vinne ambavyo ni mali ya mwanangu.”

  Katika wosia huo, Brigitte de Floor ambaye anatambulishwa kama shahidi amesaini kila karatasi, wakati saini ya marehemu inaonekana katika karatasi moja tena ya mwisho.

  Aidha, familia ya Masha inatuhumiwa kumilikishwa viwanja vinne vilivyopo Kamanga, na kwamba suala hilo tayari limewasilishwa Ofisi ya Rais, kwa Waziri Mkuu, Wizara ya Sheria na Katiba, Taasisi ya Kuzuia na Kupamban na Rushwa (TAKUKURU) na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

  Wiebke Gaetje alitalikiana na mumewe, Klaus Gaetje, mwaka 1996 na baadaye Klaus alimwoa Brigitte de Floor, mtalaka mwenye watoto wa kike wawili ambao si wa Klaus Gaetje.

  Hata hivyo, katika hali ambayo haijulikani chanzo chake, Masha ameridhia mali za Klaus Gaetje, zimilikiwe na watoto wa mke wake, jambo ambalo limelalamikiwa na mke wa kwanza Wiebke na mtoto wake Mark.

  Brigitte de Floor anadaiwa kuhamisha fedha nyingi na kuzipeleka kwenye akaunti zake zilizoko nje ya nchi, jambo ambalo vyombo vya dola na taasisi nyingine za serikali zimearifiwa, lakini bado kimya kimetanda.

  Imefahamika kuwa de Floor alitumia kampuni ya KFL kujipatia mkopo kutoka Benki ya CRDB na fedha hizo alizihamishia kwenye akaunti yake iliyopo Ubeligiji.

  Klaus na Wiebke waliishi Kamanga kuanzia mwaka 1974 hadi 1994 na mtoto wao, Mark Gaetje, alilelewa kwenye eneo hilo la Ziwa Viktoria na hivyo kuusiwa na baba yake kuwa mrithi wa mali zote.

  Kamanga ndipo makao makuu ya Kamanga Ferry Limited yenye vivuko vitatu vinavyofanya safari zake katika eneo hilo la ziwa Viktoria.

  Baada ya kifo cha Klaus Gaetje Julai 2004, Brugitte de Floor aliamuru mwili wake uchomwe moto na kuzikwa Kamanga, tendo lililofanyika haraka na bila kushirikisha familia ya marehemu wala kuufanyia mwili uchunguzi.

  “Baada ya hapo de Floor alighushi wosia wa pili wa Klaus kwa kusaidiwa na mwanasheria wake,” anasema mmoja wa watu walio karibu na Wiebke.

  Tangu hapo de Floor amekuwa anadai kuwa alipewa mamlaka ya kufanya mambo yote ya KFL kwa niaba ya Mark na ametumia fursa hiyo kuwafukuza wafanyakazi wengi wa zamani na kuajiri wageni kutoka nje ya nchi.

  Kutokana na hali hiyo, Mark Gaetje alilazimika kuandika barua, Oktoba mwaka jana, kwa Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Mwanza, kulalamikia hatua ya mama yake huyo wa kambo kughushi cheti cha ndoa ili kufaidi huduma za uhamiaji nchini.

  Lakini pia 11 Februari mwaka huu, Mark aliandika barua kwenda kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), akilalamikia mambo manne, likiwamo la kampuni kukosa mkurugenzi baada ya aliyekuwapo kufukuzwa.

  “Tangu kifo cha baba yangu sijawahi kuhudhuria kikao chochote cha bodi wala kupewa taarifa yoyote na de Floor…Isitoshe, sijawahi kupewa fedha zozote kama mkurugenzi na wala sijapokea habari kuwa de Floor ametumia kibali changu kufanya mambo kwa niaba yangu. Nakanusha kuwa sijampa ruhusa yoyote,” anasema.

  Anaeleza kuwa kama kuna mabadiliko yoyote katika KFL, “Uongozi, anwani au vingine ambavyo vinaathiri kampuni na ambavyo vinadaiwa kufanyika nikiwa mshiriki kati ya mwaka 2004 na sasa, visichukuliwe umuhimu kwa kuwa vitaathiri kampuni ambayo mimi ni mkurugenzi wake,” anasema Mark.

  Akizungumza kwa njia ya simu juzi Jumatatu na MwanaHALISI, Wiebke amesema tayari ubalozi wa nchi yake nchini umeomba hati ya kifo cha mumewe Klaus kutoka Uganda, kutokana na utata mkubwa uliogubika kifo chake.

  Hii ni mara ya tatu mwaka huu waziri Masha kutuhumiwa kutenda kinyume cha utawala bora.

  Januari alituhumiwa kuingilia mchakato wa zabuni ya vitambulisho vya taifa na Februari akatuhumiwa kufanya upendeleo kwa Mwingereza Douglas Hume Claxton kwa kufuta amri ya Mkurugenzi wa Uhamiaji ya kumfukuza nchini.
   
 2. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Swala la msingi hapa ni mirathi!

  Kusoma katika madai ya taarifa hizo wanawake wote wawili na watoto wao wanaweza kuwa wamiliki halali wa mirathi hiyo. Kutumia sheria ya ndoa tanzania, mke wa kwanza anaweza asiwe na haki yoyote juu ya mali iliyopo kwa kuwa walikuwa wameshatalakiana. Ila pia inawezekana akawa anahaki juu ya mali iwapo makubaliano ya talaka hayakufikia tamati. Swala la msingi hapa ni kutambua ndoa yake ya kwanza na kama taratibu zote zilifikiwa kumaliza umoja huo.

  Pili, mkewe wa pili, hata bila hicho cheti cha ndoa chenye utata, alikuwa na haki juu ya mali ya mumewe kwani kuishi naye zaidi ya miezi sita ndani ya sheria zetu inahesabika kama wenza. Kosa hapo labda itakuwa ni intention ya kugushi cheti cha ndoa! Swali ni kwamba kama alikuwa mke halali hata bila cheti, kwanini agushi cheti cha ndoa? (kama kweli kimegushiwa - fact of which need to be established). Je kunaagenda ya siri?

  Tatu, kwa mazingira ya kawaida baba alipaswa kuacha mirathi kwa mtoto wake wa kwanza pia.Cha msingi ni kuangalia hali halisi ya mazingira baina ya mahusiano ya baba na mtoto ilikuweza kuestablish circumstance evidence kwamba baba huyu alikuwa na kila sababu ya kumuachia mwanawe urithi! Kwanini hakuacha!

  Pa kuanzia!

  1. JE kunawaraka wa mirathi ulioachwa? Mwanasheria wake alikuwa nani?
   
 3. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Duh. Utajiri unavyosakwa. Njia nyingine zinatisha kama ikithibitika kwamba yaliyotajwa yametendeka. Maandiko yanasema Ole wake anayeibia wajane na mayatima!
   
 4. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  I think this is beyond utajiri! It is about the rule of law, conspiracy, current politics.

  Ukisoma article vizuri utagundua hili sio swala juu ya mirathi peke yake, ila zaidi inaongea swala la kifo cha ghafla, kugushi vyeti vya ndo, utumiaji wa madaraka mbovu.
   
 5. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Masha inatakiwa awe mbali sana na hii kampuni yao ya IMMMA, vinginevyo itamfikisha pabaya. Cases za mirathi ni ngumu sana maana unaweza kukuta jamaa alioa kihalali kimya kimya bila ya ile familia yake nyingine kujua.

  Lakini inaelekea Masha mwepesi mno wa kuingia kwenye mitego bila kujijua. Awe mwangalifu mno na hizi scandals maana zikianza kuingia huwa hazitoki.
   
 6. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Yaani Masha duu?? Sijui tamaa yanini yarabi? Sasa aibu gani hii?
   
 7. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  PH heshima yako.

  nimekupata uzuri. hayo uliyoyasema nimeyakweka katika mstari mmoja hapo juu. Additionally, Pressure ya kutoka kwa hao wajerumani kwenda kwa serikali yetu, basi tutasikia mengi.
   
 8. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ni mapema mno kupima uhusika wa masha katika kesi hii. Lakini swala la yeye kuhusihwa tu sio zuri maana msomaji anabaki kujiuliza maswali makuu manne!

  1. Je alijua kuhusu kifo! Alishiriki kwa namna moja ama nyingine?

  2. Je mahusiano yake yeye na mjane yakoje?

  3. Je alijua kuhusu cheti cha ndoa? Alishiriki?

  4. Je kunachochote anachofaidika kwa kumsadia mjane huyu ama anatimiza wajibu tu?

  Ila mpaka sasa! taarifa zilizopo ni ndogo sana kumuhukumu, na kwa mtizamo wangu mimi, sidhani kama masha anaweza kujiingiza katika uruhani kama huu.
   
 9. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145

  PH, Kuongezea hapo, kama hiyo tuhuma za yeye na familia yake kunufaika na hiyo mirathi (Viwanja) kama ikithibitishwa mahakamani mbona atakuwa amejivua nguo.
   
 10. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Aha! Vyote ni vya kusubiri tu maana hizi kesi zinazohusishwa watu wa nje sanyingine zinakuwa na mambo chungu mzima kwahiyo hali halisi ni kwamba inaweza isifunue mambo mengi. Na kama kweli kesi inahoja za msingi basi watayamaliza kidiplomasia, na haki za walio nyanganywa kurudishwa!
   
 11. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2009
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  kumbe Masha bado yupoyupo!! 2010 hiyoooo....
   
 12. Enigma

  Enigma Senior Member

  #12
  May 14, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 108
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Bandugu wenye uwezo mkubwa katika luga naomba mnisaidie kutafsiri hiyo article juu kwenda katika kiingereza ili niweze kuipeperusha katika mbawa zangu na kuipeleka mpaka sehemu husika. natanguliza shukurani nyiiiingi
   
  Last edited: May 14, 2009
 13. Enigma

  Enigma Senior Member

  #13
  May 14, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 108
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  wakulu Kapinga, uwiano maalum, bluray, mag3, Kuhani, mzee mwanakijiji, nyaningabu, invisible, pundit, Zemu, Fundi mchundo, kellyo1 na mwingine yeyote yule tafazali nisaidieni bandugu
   
 14. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2009
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Huyu dogo alikuwa madarasa kadhaa nyuma yangu, na ilikuwa familia poa kabisa, very good people. Navyokumbuka dingi yake alikuwa anampenda sana kijana wake, na haiwezekani asimwachie mali yote kijana wake. Jinsi jamaa alivyoijenga biashara yake, halafu mtu aje achukue hivi hivi tu bila mtoto wake kufaidi, aisee siamini wala haiwezekani.
  Halafu hii ya kufa kwa utata na kuchomwa moto sikuijua. This smells like a big stinker!! This woman is a gold-digger man, with maximum killer instincts na lazima anamwaga pesa kubwa kwenye hii ishu.
   
 15. K

  Kokolo JF-Expert Member

  #15
  May 15, 2009
  Joined: Mar 20, 2008
  Messages: 487
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Kuchomwa moto ilikuwa ni kupoteza ushahidi, maana wangefukua na kufanya uchunguzi kwa kina na kugundua kwamba alipigwa na sumu ya mamba kwa kuwekewa kwenye wisk. Huyo mama atakuwa ni suspect #1, kwa kusaidiwa na Masha hili kupora mali ya huyo Mzee, huyo mzee alikuwa ni hard worker, mpaka kufika hapo alipokuwa, huyu mama tamaa ya pesa akamwondolea mbali mzee wa watu, nafikiri huyo mzee alikuwa ameshampa account zote za benki na huyo mama kuchungulia tu, akaunda kikosi cha kumumaliza huyo mzee, na kikosi kingine cha akina masha kumalizia kwenye masuala ya legal- urithi wa mahali na kutorosha pesa kwenda nje. Masha ni suspect #2. Huyo Mzee alivyokuwa anapenda kijana wake sidhani kama angempa urithi huyo mama wa pili.
   
 16. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #16
  May 15, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145

  "Kenge haachi mila zake mpaka atoke damu puani na masikioni!"
   
 17. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #17
  May 15, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hii hatari sasa Masha!!!umezidi
   
 18. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #18
  May 15, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Na haiwezekani eti vyote ni bahati mbaya kwake, haka ni kafisadi kanako ibukia kwa nguvu zote, ila sasa hadi hii ya kutoa uhai wa mtu kwa ajili ya tamaa ya mali is more than I could imagine!
   
 19. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #19
  May 16, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Tanzania sasa tunahitaji mfumo kama wa America wa kuchagua viongozi wa ngazi za juu kama mawaziri na makatibu wakuu. Lazima kwanza iwepo kamati maalumu ya kuchunguza tabia na rekodi za mtu na jinsi gani anaweza kutumikia watu. sasa kama Kikwete anatuwekea watu kama hawa, na anashindwa kuwachukulia hatua stahiki kwa kila ovu wanalolifanya? tumueleweje? kama ni makosa ya kibinadamu, kwa masha yameshapitiliza. Anachofanya sasa kimo ndani ya dhamira yake. Je watawala wetu kama wanatuonyesha ndio wako hivi, tufanyeje?
   
 20. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #20
  May 28, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye anapaswa kusimamia utekelezaji wa Sheria (Law Enforcement) anapotuhumiwa kuhusika na uvunjwaji wa sheria, wajibu wake wa kwanza (kama kweli yeye ni msafi) ni kujiuzulu kwa muda, kukaa pembeni ili kupisha uchunguzi huru wa tuhuma hizo ufanyike. Akipatikana hana hatia, haki itatendeka. Akipatikana na hatia, haki itatendeka vile vile.

  Tukumbuke mfano alioutoa Mzee Wetu, Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Awamu ya Pili, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, alipojiuzulu uwaziri wake baada ya kutokea shutuma dhidi ya wizara yake yalipotokea mauaji ya vikongwe kule Shinyanga.

  Huu ndio ukomavu wa kisiasa na uwajibikaji wa kiongozi.

  Masha ana ubavu wa kukaa pembeni?

  ./Mwana wa Haki
   
Loading...