Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Hatua ya mgombea ubunge chama cha mapinduzi (CCM) Jimbo la Nyamagana, Mwanza Lawrence Kego Masha kumwekea pingamizi mgombea wa Chadema kwa madai kuwa si raia imezua utata wa kisheria wa mawaziri kuendelea na nafasi zao hata baada ya Bunge la Muungano kuvunjwa.
Mbali na suala la kutokuwa na uraia, mgombea huyo wa Chadema, Ezekieh Dibogo Weje anadaiwa pia kuwa hakuwasilisha kiapo cha kisheria kuthibitisha yale aliyojaza kwenye fomu kama inavyotakiwa pamoja na kushindwa kujaza fomu za kugombea kama inavyotakiwa.
Sababu nyingine zilizotolewa na Masha ni kuwa mgombea Wenje alidai kuwa ni mkazi wa Burola A wakati si kweli kwani hana makazi katika mtaa huo na kwamba mgombea huyo pia amesema uongo juu ya cheo chake katika Nation Group kuwa ni meneja wakati in afisa masoko pamoja na kushindwa kujaza fomu ya kugombea kama inavyotakiwa.
Masha ni Waziri wa Mambo ya Ndani na hatua yake ya ya kudai kuwa Wenje si raia na kufuatiwa na malalamiko ya Wenje kuwa Masha anamtisha maisha pamoja na kutumia maafisa uhamiaji kwenda kwao Rorya kuchunguza uraia wake imezua hisia kwamba mgombea huyo wa CCM ametumia madaraka yake kufuatilia uraia wa mpinzani wake.
Wenje alisema kwamba Alhamisi iliyopita majira ya jioni alipokea simu ya Masha akimsihi kuondoa jina lake kwenye kinyanganyiro hicho kwa madai kuwa sera za kampuni anayofanyia kazi haziruhusu wafanyakazi wake kujiingiza katika siasa.
Aliniuliza kama nazifahamu sera za kampuni ninayofanyia kazi kwani haziruhusu mtumishi kuingia katika siasa na hivyo kunitaka nifikirie kuondoa jina langu na kwamba angenisaidia kurudishwa kazini. Lakini mimi nilikataa na kumwambia siwezi kujitoa kugombea.
Siku hiyo hiyo saa mbili usiku alinipigia tena simu na kunieleza kuwa atatumia rasilimali zake kuhakikisha ananiwekea pingamizi kwa kuwa mimi si raia. Na kweli maofisa sita wa Serikali (Uhamiaji) walikwenda nyumbani kwetu Rorya na kumbughudhi mama yangu mzazi kwa madai kuwa wanakusanya vielelezo juu ya uraia wangu, alisema Wenje akieleza kwamba alimwomba Masha aache kutumia vyombo vya dola kwa masilahi yake.
Lakini Masha alikiri kumpigia simu mgombea huyo wa Chadema lakini akakana kumtishia pamoja na kutumia maofisa uhamiaji kwenda kufuatilia uraia wakekijijini kwao Rorya na akasema kuwa alimpigia kumshauri kwa nia njema, kwani siasa si ugomvi.
Ni kweli nilizungumza naye kwa simu lakini si kwa ugomvi wala kumtisha. Milimweleza kuhusu sera za kampuni yao kutoiruhusu watumishi wake kujihusisha na siasa na kama anazifahamu.
Pia nilimwambia kuhusu udanganyifu katika fomu zake na kwamba nilikuwa natarajia kumwekea pingamizi na nitamshinda, hivyo bora angeachia ngazi.
Nilimshauri pia kama ndugu yangu, maana siasa si ugomvi, kuwa ukiacha kurudisha fomu nitakuombea usifukuzwe kazi kulingana na sera za chombo chako kwani kitendo cha kujiingiza katika siasa atafukuzwa kazi. Na kweli niliweka pingamizi sasa huko ni kumtishia maisha?
Sijamtuma ofisa yeyote kwenda kwake na hili la uraia nimelipata kutoka kwa wapambe wake. Mimi ni mwanasheria, siwezi kufanya hivyo. alisema Masha.
Ni kutokana na maelezo hayo ya Masha, baadhi ya watu wanadai kuwa ni ngumu kutenganisha kitendo cha maofisa uhamiaji kwenda kufuatilia uraia huo wa Wenje baada ya Masha kumpigia simu kumwomba ajitoe na kwamba angemwekea pingamizi kwani si raia.
Huyu ni Waziri wa Mambo ya Ndani mwenye dhamana ya mambo ya uraia hivyo kitendo cha yeye kuhoji uraia wa mtu na hapo hapo watu wanaenda kwake Wenje kufuatilia vielelezo vya uraia wake, moja kwa moja unaona kuwa kuna uhusiano fulani kwamba huenda ni maelekezo yake kwa idara ya uhamiaji.
Hapa kuna conflict of interest. Pia inapaswa ujiulize ni kwa nini Masha ampigie simu kumwomba ajitoe wakati anajua atamwekea pingamizi?
Ni kwa nini aseme angemwombea aendelee na kazi yake iwapo angejitoa. Ina maana Wenje alikuwa hajui sera za kampuni anayofanyia kazi mpaka aambiwe na Masha? Au Masha alikuwa na uchungu gani kuona Wenje atakosa kazi mpaka amwombee asifukuzwe? Masha ana uhusiano au mamlaka gani kwa mwajiri wa Wenje mpaka aseme angemwombea asifukuzwe kazi? Huyu ni msomi wa Chuo Kikuu hawezi kuamua kugombea bila kujua sera za chombo chake, anasema mkazi mmoja wa jijini Mwanza aliye karibu na sakata hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Watu kadha waliozungumza na Raia Mwema wanasema kitendo cha mawaziri kuendelea na nafasi zao baada ya Bunge kuvunjwa kunaleta mgongano wa masilahi kwani waziri anaweza kutumia nafasi yake kujifanyia kampeni ..
Habari zaidi katika Raia Mwema ya leo. Mwenye complete soft copy ya stori hii twamuomba atuwekee hapa.