Masha achukua fomu Nyamagana

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
Jumanne, Agosti 28, 2012 05:48 Na John Maduhu, Mwanza

WAZIRI wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha amechukua fomu ya kuwania kiti cha Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Nyamagana na kutamba kuwa yeye ni kiongozi wa vitendo.

Masha ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa jimbo la Nyamagana, aliyasema hayo jijini Mwanza wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema ameamua kuchukua fomu ya NEC, kwa ajili ya kuiwakilisha Wilaya ya Nyamagana na kutumia nafasi hiyo, endapo akichaguliwa kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo aliyoiacha.

Alisema alipokuwa mbunge wa Nyamagana, alifanya kazi kubwa kuinua elimu na kutoa ajira kwa vijana.

Alisema kuna baadhi ya wanasiasa, wamekuwa wakitumia umaskini wa wananchi kwa kuwatolea lugha tamu na nyepesi kwa ahadi lukuki, ili wawachague.

"Kila nikipita hapa jimboni Nyamagana nimekuwa nikifarijika namna wananchi wanavyonisimamisha kila mahali na kunipongeza Masha ulifanya kazi nzuri sana utusamehe ni upepo tu ulipita,kwangu hiyo ni faraja kwani wananchi wanajua nini nilichokifanya katika kipindi changu cha miaka mitano nilipokuwa Mbunge",alisema.

"Nina uhakika naunmgwa mkono na wana ccm wengi katika jimbo la Nyamagana na hili ninanipatia faraja ya kuendelea kuwatumikia kwa kuniamini,katika uchaguzi ndani ya CCM katika kura za maoni niliongoza kwa kupata kura nyingi hata kura nilizopata katika uchaguzi mkuu ni nyingi kamwe nisingeliweza kukataa maombi ya wana Nyamagana zaidi ya 30,000 ambao walionyesha imani kwangu hivyo katika kuwashukuru nimekubali kuwania NEC kwa ajili ya kuwawakilisha tena",alisema Masha.

Katika Wilaya ya Geita, Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Mkoa wa Mwanza(NCU), Leonard Bugomola amechukua fomu kwa ajili ya kuomba kuwania nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri kuu ya taifa(NEC),wilaya hiyo.

Toa Maoni yako kwa habari hii
 
vipi tena masha, au umepata hasara biashara yako ya kuzoa taka dar? pia nilisikia ktk kipindi cha makutano kuwa unamtoto wa kike na umejifunza hadi kubadili nepi?
 
Lowassa kamwambia akachukue form ili akifanikiwa waomgeze nguvu huko NEC dhidi ya Membe!!
 
Politics is a war and quite as dangerous. In war you can only be killed once,but in politics many times.
Sir Winston ChurchillI believe this time utaenda kufanya utakaso na kutengeneza mazingira mazuri zaidi kisiasa kuliko ilivyokuwa mwanzo maana sasa umeshajua tamu na chungu!

Hizi ni strategic movement za mzee mamvi.... Lowassa ni expert kwenye politics...
 
Politics is a war and quite as dangerous. In war you can only be killed once,but in politics many times.
Sir Winston ChurchillI believe this time utaenda kufanya utakaso na kutengeneza mazingira mazuri zaidi kisiasa kuliko ilivyokuwa mwanzo maana sasa umeshajua tamu na chungu!

Actually Mao ze Dong alisema na nanukuu..'politics is war without firing a weapon,war is politics played by firing weapons'.
 
Sikio la kufa halisikii dawa, wewe masha juzijuzi tu umeondoka mwanza kwa aibu, na fedheha kubwa leo hii unarudi tena? haya sasa nenda ukavunjike guu maana hautaki kusikia la mkuu.
 
Upepo gani? Aseme ukweli kuwa nguvu ya umma ilimzidi kasi.

Back
Top Bottom