Masele Mbunge wa CCM Shinyanga Mjini, awaambia wananchi kuwa kuna baa la njaa nchini

Wanabodi,
Asubuhi ya leo kupitia kipindi cha matukio RFA kinachorushwa hewani mida ya saa moja asubuhi, nilisikia taarifa kuhusu upungufu wa chakula mjini Shinyanga, ripota alirusha kiclip kinachosemekana ni cha mbunge wa Shinyanga mjini Mh Stevie Masele kuwa hawezi kuwa mnafiki kwa kusema hakuna njaa wakati wananchi wanateseka. Alienda mbele zaidi kwa kusema anamwomba mkuu wa wilaya kuomba chakula serikalini ili bei ya chakula ishuke.

Nimetafakari sana,huyu mbunge ni mbunge wa Shinyanga mjini kwa tiketi ya CCM, ni kujilipua, ndo uwakilishi au kaamua kama " I have nothing to loose?"
Nisingeshangaa angekuwa ni mbunge wa opposition,maana tumezoea kuwasikia wakiongea bila kuficha,sasa huyu anakenda kinyume na mwenyekiti wake wa taifa tena bila wasi wasi kabisa maana aliongea na media zikiwepo na bila chenga wakarusha redioni.
Ndo wabunge tuwatakao, ndo wabunge wanatoa vilio vya watu waliowachagua lakini je, ndo wanaokubarika kiprotokali?
 
Leo mbunge wa ccm masele alikuwa na mkutano wa hadhara mjini shinyanga amesema nchi inakabiliwa na njaa Kali sana nae anashangaa kuona serikali ipo kimya.
e6054abbeb79940be0b0399d714a4963.jpg
16f6f660a18a420cee342b4a23287977.jpg
Masele ni mmoja wa wabunge wa CCM waliopaswa kuwa declared ni mashujaa wa taifa hili, he calls a spade a spade.

Steven Masele atamkwe Shujaa wa Taifa! Ni kweli Balozi wa Uingereza ni Jasusi. To Hell with...!
Paskali.
 
Tembea uone, sehemu kubwa ya TZ hali sio nzuri.
Debe la mahindi limeshafika Tsh 30,000 kutoka sh 12,000.
Hii ni indicator kuwa hali ya chakula sio nzuri sehemu nyingi
Sikatai mkuu hali si nzuri sana. Ila WAWEKE MIKAKATI, Maana njaa KUBWA ni MWAKANI hasa kama mvua sitachelewa zaidi.
 
Ana gadhab za kukosa uwaziri huyu hakuna lolote.....
Unaonekana una uchizi wewe,uwaziri kaukosaje kwani aligombea uwaziri!Ni sawa na ww tuseme unaweweseka umeukosa ukuu wa wilaya wilaya ilhali hata sifa haunazo.
Kwa hiyo hadithi yako inatufundisha nini ...kwamba kule kuna shibe au?Mbaya zaidi muda huu upo mtandaoni kama walivyo great thinkers wengine. ama kweli msafara wa punda nyumbu nao wamo.
 
Sikatai mkuu hali si nzuri sana. Ila WAWEKE MIKAKATI, Maana njaa KUBWA ni MWAKANI hasa kama mvua sitachelewa zaidi.
Unataka nani aweke hiyo mikakati?Je unaposema eti NJAA KUBWA IPO MWAKANI unamaana wananchi wana chakula cha kujitosheleza mwaka huu wote,mwakani ndo kitawaishia?
 
Ana gadhab za kukosa uwaziri huyu hakuna lolote.....
Ila kuna wakat mzahaa ni maangamizi yaani kwakuwa kakosa uwaziri ndo aseme ukweli kuwa kuna njaa! ww huoni ukweli kuwa kuna njaa ?na alichosema ni kweli?kuwa kuna njaa we mpumbavu sana tena inawezekana ni kati ya watu wanaotaka kutangazwa na naibu waziri wa afya kigwangara.
 
Unataka nani aweke hiyo mikakati?Je unaposema eti NJAA KUBWA IPO MWAKANI unamaana wananchi wana chakula cha kujitosheleza mwaka huu wote,mwakani ndo kitawaishia?
Nina maana chakula kidogo kilichoko tunaweza kukitumia vizuri.
Hiyo haimaanishi ninakataa kwamba sehemu zingine hazina uhaba wa chakula.
 
kwan haja kamatwa? h kaul c sawa na ile ya zitto mpaka akawindwa kama kandez na akapotea kama kidenz msitun?
 
Nina maana chakula kidogo kilichoko tunaweza kukitumia vizuri.
Hiyo haimaanishi ninakataa kwamba sehemu zingine hazina uhaba wa chakula.
Nashukuru mkuu labda swali lingine la kizushi...Tuna akiba ya chakula kiasi gani kulinganisha na idadi ya watu uliyotumia kusema icho kidogo kitatutosha adi mwakani?
 
Mbunge huyu HAJAKOSEA na wala HAJAMDHARAU rais Magufuli.
Ila ANAOSHA MIKONO yake kwa wananchi wake waliomchagua.
Na HASA anapoliangalia ENEO lake na hali ILIVYO.

ISITOSHE si NCHI NZIMA iliyo na NJAA.
Mahali palipona njaa TUZUNGUMZE bila WOGA.Maana ITATUOKOA
Kwa hiyo aliposema Tundu lisu kuwa nchini kuna njaa alikosea?

Tuna Rais wa aina yake kwa kwel
 
Kwa hiyo aliposema Tundu lisu kuwa nchini kuna njaa alikosea?

Tuna Rais wa aina yake kwa kwel
Tundu Lisu kama Mtanzania tena kiongozi ni haki yake KIKATIBA kusema analoona maana tuna uhuru wa kujieleza katika katiba yetu.
 
Back
Top Bottom