Masela wanakufa sana, sio kwa idadi hii kubwa ya wajane duuh!

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,532
Jana 4/4/2019 wajane walifika kwa wingi sana pale Mlimani City wakati napita pale idadi yao ilisababisha hata foleni kubwa na msongamano mkubwa sana eneo lile...kiasi kwamba nikajiuliza kwamba inaonekana masela wanakufa sana. Wanaume kuna tatizo pahala?....hatuli kiasi cha kutosha?...tuna mawazo sana?....ngoma hatutaki kumeza ARV?....kwamba ni mishemishe tu?,...ajali?....au nini ....nini tatizo wanaume mbona idadi ya wajane kubwa sana
wajanepic.jpg
WAJANE-11.jpg
 
Ngoma inaondoa wengi sana.. Kuna jamaa yangu tumemzika majuzi. Kilichomuua ngoma wanasema kifua...

HIV/AIDS is real.. Tujihadhari!

Sent using Jamii Forums mobile app
Me sijawahi kwenda kwenye msiba wakasema jamaa kapotea kwa ngwengwe,.ni kifua,mapafu sijui figo,kisukari n.k hawasemi hiyo kitu...

Aisee kinga ni bora kuliko tiba,watu tunasepa hasa vijana..
 
Jana 4/4/2019 wajane walifika kwa wingi sana pale Mlimani City wakati napita pale idadi yao ilisababisha hata foleni kubwa na msongamano mkubwa sana eneo lile...kiasi kwamba nikajiuliza kwamba inaonekana masela wanakufa sana. Wanaume kuna tatizo pahala?....hatuli kiasi cha kutosha?...tuna mawazo sana?....ngoma hatutaki kumeza ARV?....kwamba ni mishemishe tu?,...ajali?....au nini ....nini tatizo wanaume mbona idadi ya wajane kubwa sanaView attachment 1063017View attachment 1063016
Matatizo yapo mengi sana,ila kubwa ni ni namna ya kusaka hela ili watoto wajambe.
Ila kwangu mimi naona kufa kupo tu so wanaume tugange yajayo. Hebu tuwaoe hawa wajane tuwaokoe na mateso wanayoyapata,ikiwa ni sehemu ya kuwafariji. Hebu tuachane na zile kasumba. Hawa wajane wanahitaji matunzo,ni jukumu letu wanaume kuwatunza hawa wajane.
 
Ila mamen tunadanja duh...mi nahisi sababu ya ubishi hatutaki kutibiwa...waoga wa sindano...uzembe barabarani....bahati mbaya kwenye kazi zetu za shuruba nk...tuishi kwa umakini mortality rate ni kubwa sana kwetu wanaume ingawa sie ndio wachache pia...
 
Sidhani kama wote ni wajane, wengine wamejua kuna fursa hapo, mfano waliotelekezwa, waliogombana na wazazi wenza nk.
 
Oh, yawezekana wengi hawajui maana ya ujane, wanafikiri ni yoyote mwanamke asiye na mme ila ana watoto.

Huwa nasiliza maswali ya Masanja Tv jinsi watz wasivyojua maana ya vitu vingi

Ndio ukweli, yaani ndugu yangu tuseme kweli, jamii yetu ina wajinga wengi sana. Tujitahidi kusomesha hivi vizazi vyetu, watawala hawataki watu waelimike.
 
Back
Top Bottom