Masasi, Mtwara: Watu 11 Wafikishwa Mahakamani kwa Uhujumu Uchumi na kuisababishia hasara Serikali ya zaidi ya Tsh. Milioni 13

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,804
11,963
Na Hamisi Nasri, MASASI

WATU 11 wa wakazi wa wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Masasi mkoani humo kwa kosa la uhujumu uchumi na kuisababishia hasara serikali ya zaidi ya sh.13 milioni.

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani na ofisi ya taifa ya mashtaka ya mkoa wa Mtwara kwa kushirikiana na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Masasi mkoani hapa wakikabiliwa na kosa la uhujumu uchumi.

Akisoma mashtaka ya watuhumiwa hao 11 mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo ya wilaya ya Masasi, Rehema Machumu, wakili mwandamizi wa serikali ofisi ya taifa ya mashtaka mkoa wa Mtwara, Wilbrod Ndunguru.

Alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao wamefikishwa katika mahakama hiyo kwa kosa la uhujumu uchumi kwa kujipatia jumla ya fedha sh.13.2 milioni kinyume cha sheria.

Alieleza mahakama hiyo kuwa watuhumiwa wote kwa pamoja wanatuhumiwa na kosa la uhujumu uchumi kinyume cha sheria ya kuzia na kupambana na rushwa sura ya 329 iliyofanyiwa makerebisho mwaka 2019 na kusababisha harasa kwa halmashauri ya wilaya ya Masasi ya zaidi ya sh.13.2 milioni kinyume na sheria ya uhujumi uchumi iliyofanyiwa makerebisho mwaka 2019

Wakili huyo mwandamizi wa serikali alieleza kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo la uhujumu uchumi kwa kughushi nyaraka za serikali na kujipatia kiasi cha fedha kwa kiwango tofautitofauti

Alidai kuwa kati ya mwaka 2013 hadi 2016 washtakiwa walighuli nyaraka za serikali na kulipwa fedha za fidia isivyo halali na kuisababishia hasara halmashauri ya wilaya ya Masasi ya zaidi ya sh.13.2 milioni kosa ambalo ni uhujumu uchumi.

Alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao walilipwa fedha kama fidia wakijifanya kuwa ni waathiriwa wa mradi wa maji wa Masasi-Nachingwea (MANAWASA) huku wakitambua kuwa wao sio walengwa wa malipo ya fidia katika mradi huo.

Hata hivyo washtakiwa hao wote kwa pamoja wamekana makosa yao na kupelekwa rumande baada ya kukosa dhamana kutokana na mahakama hiyo ya wilaya kutokuwa na mamlaka ya kutoa dhamana kwa makosa ya uhujumu uchumi.

Kesi hiyo namba 7 / 2021 imetajwa kusikilizwa tena Mei 18 mwaka huu katika mahakama hiyo ya wilaya ya Masasi mkoani hapa.
 
Habari haijajitosheleza. Tueleze hao wananchi wanatoka maeneo au viijiji gani. Ni akina nani?
 
Wa mabilion ndio ishu ya DPP hawa wachimba chumvi wanaweza kwenda ujue maana huko wilayani ndiko hukumu za ajabu zinatokea...
 
Back
Top Bottom