Masanja Mkandamizaji huyu huyu amekua na upako wa kuangusha watu?!

Khaa..!!Masanja mkandamizaji amekua na Upako kama wa Askofu Kakobe wa Kuangusha watu hivi??!!
@NgarenaroBoy.
Usishangae mkuu hii nayo ni sanaa tu kama Bongo flava. Kila mtu anaweza kufanya hayo. Ni uamuzi tu
 
msanii ndani ya jumba LA sanaa ghafla amekuwa mwinjilisti...bila shaka hayo maigizo yasingeepukika

*naturally masanja ni msanii na huko atapiga hela hadi yy mwenyewe ajishangae alikuwa wapi.!?

hakunaga hela rahisi na ya bure kama ya walokole;wape miujiza... nao watakupa vyote
 
Natamani chalamila aje na bakora awacharaze,utaona wakavyoinuka hapo utafikiri sio wao waliokuwa wanagalagala hapo chini
 
Watu wanaomchezea MUNGU wameongezeka kwa kasi sana. Hasa kuringana na ongezeko la watu na uhitaji wa watu kuwa karibu na MUNGU,hasa ongezeko la magonjwa yenye ugumu wa kutibika,lakini ndio hivyo,wanaishia mikononi mwa haya majizi
 
Mazee umesahahu miezi michache ilopita kuna trend ilikuja kwa kasi ya watu kuijiangusha ovyo bila sababu japo haikuchukua muda?? Mi nahisi huu ni muendelezo
 
Matayo 7:1-2

Matayo 7:3-5
“Msiwahukumu wengine, msije nanyi mkahukumiwa na Mungu; kwa maana jinsi mnavyowahukumu wengine, ndivyo nanyi mtakavyohukumiwa; na kipimo kilekile mnachotumia kwa wengine ndicho Mungu atakachotumia kwenu. Kwa nini wakiona kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako, na papo hapo huioni boriti iliyoko jichoni mwako? Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako,’ wakati wewe mwenyewe unayo boriti jichoni mwako? Mnafiki wewe! Ondoa kwanza boriti iliyomo jichoni mwako na hapo ndipo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilichomo jichoni mwa ndugu yako.
Mathayo 7:1‭-‬5 BHN
 
Back
Top Bottom