Masanja Mkandamizaji awatembelea majeruhi wa Lucky Vincent nchini Marekani

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Msanii na Mhubiri wa Injili, Masanja Mkandamizaji leo amewatembelea wanafunzi majeruhi wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent nchini Marekani.
Masanja, aliyepata umaarufu katika kipindi cha televisheni cha ze comedy, ameandika katika ukurasa wake wa instagram akionyesha kumshukuru Mungu kwa kuwaona watoto hao akiwa Marekani.

“Mungu amenipa neema ya kwenda kuwaona wadogo zetu waliopata ajali, Sadia na Wilson na kuwepo Marekani kwa matibabu, imekuwa siku njema kwetu sote tumefurahi pamoja nao kula nao na kumtafakari Mungu kwa pamoja,” ameandika Masanja.

Wanafunzi hao walipata ajali ya gari wilayani Mbulu, mnamo Mei mwaka huu wakati wakienda kufanya mitihani ya urafiki katika shule nyingine.
Wanafunzi 32, walimu wawili na dereva walifariki dunia katika ajali hiyo.
Wanafunzi watatu, Doreen Mshana, Saidia Ismail na Wilson Elipokea walinusurika na kupelekwa Marekani kwa matibabu zaidi.

“Lakini pia nimezungumza na wenyeji wao waliofanikisha Safari yao ya Marekani!! Hakika Mungu ni mwema wameendelea kuimarika na wanaendelea vizuri! shukrani kwa madaktari na kila aliyetenga muda wake kuwaombea. Wazazi wao wanawasalimu na wanawashukuru kwa ushirikiano na maombi yenu.” Ameandika Masanja.
pic%2Bmasanja.jpg
 
Naona Masanja na Joti mambo yenu si mabaya!! sasa msaidieni na mwenzenu yule "shemejiii" naona kidogo network yake ya kiuchumi haijakamata!!!!
 
Msanii na Mhubiri wa Injili, Masanja Mkandamizaji leo amewatembelea wanafunzi majeruhi wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent nchini Marekani.
Masanja, aliyepata umaarufu katika kipindi cha televisheni cha ze comedy, ameandika katika ukurasa wake wa instagram akionyesha kumshukuru Mungu kwa kuwaona watoto hao akiwa Marekani.

“Mungu amenipa neema ya kwenda kuwaona wadogo zetu waliopata ajali, Sadia na Wilson na kuwepo Marekani kwa matibabu, imekuwa siku njema kwetu sote tumefurahi pamoja nao kula nao na kumtafakari Mungu kwa pamoja,” ameandika Masanja.

Wanafunzi hao walipata ajali ya gari wilayani Mbulu, mnamo Mei mwaka huu wakati wakienda kufanya mitihani ya urafiki katika shule nyingine.
Wanafunzi 32, walimu wawili na dereva walifariki dunia katika ajali hiyo.
Wanafunzi watatu, Doreen Mshana, Saidia Ismail na Wilson Elipokea walinusurika na kupelekwa Marekani kwa matibabu zaidi.

“Lakini pia nimezungumza na wenyeji wao waliofanikisha Safari yao ya Marekani!! Hakika Mungu ni mwema wameendelea kuimarika na wanaendelea vizuri! shukrani kwa madaktari na kila aliyetenga muda wake kuwaombea. Wazazi wao wanawasalimu na wanawashukuru kwa ushirikiano na maombi yenu.” Ameandika Masanja.View attachment 550029
Ajali ilitokea Mbulu!!! Siyo Rhotia-Karatu tena?
 
Back
Top Bottom