Masanduku Yenye Kura Feki: Adui Yetu ni Nani?!

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,168
8,142
Habari ambayo imeenea hivi sasa kwenye mitandao ya kijamii ni kukamatwa kwa masanduku yenye kura feki! Wengi wetu tunaamini huu ndio mwanzo tu wa lile bao la mkono ambalo tulipata kusikia likihubiriwa! Pamoja na yote hayo, je hivi ni kweli tunafahamu malengo ya hayo masanduku?

Kila kituo kina ulinzi na mawakala wa vyama! Now assume Kituo X chenye mlinzi na mawakala wa vyama vyote. Hivi ni kipi ambacho ni rahisi kati ya kununua mawakala wa vyama hasimu AU kuingiza mi-box mikubwa yenye kura feki kinyemela-- mi-box ambayo inaonekana wazi na mtu yeyote? Hizi kura hazipigwi gizani... na kabla kituo cha kupigia kura hakijafunguliwa na upigaji kura kuanza, eneo zima linakaguliwa ikiwa ni pamoja na chumba chenyewe. Sasa haya masanduku yenye kura feki yanaingiaje humo hadi kura zake kujumlishwa pamoja na kura zingine halali?Ikiwa hawa mawakala wetu watashindwa kuyaona masanduku yenye kura feki yakiingizwa kwenye masanduku halali; je kweli wataweza kuona uhesabuji wa kura zilizo halali? Kisheria, kabla ya idadi ya kura zilizopigwa kutangazwa; mawaka wa vyama vyote wata-sign kuafikia wa kura hizo... je, hizo kura feki zilizo kwenye masanduku zitasainiwa na mawakala gani?!

Kama issue ni kura, ni kwanini basi mtu asiweke hizo kura feki kwenye bahasha na kwenda kuzipenyeza kupitia wahusika waliohongwa kwenye kituo husika badala ya kupita na masanduku ambayo popote utakapotia mguu yataonekana?

Kwenye media moja ya nje imeandika; bila kujali nani atashinda kwenye uchaguzi huu; lazima machafuko yatatokea! Watu tukaichana live ile media lakini kwa mtindo huu ni kweli machafuko yanaweza kutokea! Watu hatutaki kuangalia uwezekano mwingine wa matukio haya ambayo ukiangalia kwa makini wala hayana nia ya kuiba kura bali kuvuruga uchaguzi na hatimae kuleta maafa akilini! Sina shaka zipo njia mzuri tu za kuiba kura lakini ni mwendawazimu peke yake ndie anaweza kuiba kura kwa kuingiza masanduku feki ambayo yanaweza kuonekana yeyote! Narudia... kama lengo ni ku-tally kati ya hard votes/karatasi za kura na idadi itakayoandikwa, bado kuna better way ya kufanya hivyo badala ya kutembea na masanduku barabarani! Na kama ikiwa ni kweli hayo masanduku yanakamatwa mengine yakiwa kwenye magari; hao wanaokamata wanajuaje kwamba hayo magari yamebeba ma-box kama sio hao wabebaji wali-stage ili wakamatwe? Na ikiwa wali-stage ili wakamatwe; kwanini walitaka wakamatwe kama sio kudhihirisha kwamba walibeba masanduku ya kura?
 
Nani kama Ben Saa8 hapa Tanzania kumwamuru mkuu wa majeda kujitokeza ndani ya cku 7 la cvyo....na akagwaya na kutii na kujitokeza kwa mkwala tu mzito wa maandishi.

Ben Saa8 2025 Bliv me
 
hueleweki kawaulize nec mbona masamnduku yao yamekamatwa mtaani??

na mbona karatasi za kura zinakamatwa kwenye magari ya serikari ???

na mbona kura zina tik ya mgombea wa ccm??
 
Ukawa wanaweweseka wanajua kabisa wanashindwa kwa hiyo wanachotafuta ni public sympathy. Wanazusha matukio kwa uongo ili waonekane kuwa wameonewa.
 
Akili kubwa imetumika katika hii post.

Watu wanatafuta huruma na kichochezi cha fujo.
 
Ni wazi NEC, IKULU, Mahakama na Polisi kushinikiza watu wasilinde kura kitu ambacho kipo kisheria huenda walijua kitu juu ya haya yanayoendelea.
Aliyemuelewa Yeriko Nyerere kuwa "Watanzania hawahitaji amani bali wanahitaji haki" anaweza kujua kitakachokuwa kinatokea leo kuanzia mida ya alasiri.
 
Ukawa wanaweweseka wanajua kabisa wanashindwa kwa hiyo wanachotafuta ni public sympathy. Wanazusha matukio kwa uongo ili waonekane kuwa wameonewa.

Nyie maharamia mnatafuta ushindi kwa njia haramu.uongo gani thibitisha.
 
Habari ambayo imeenea hivi sasa kwenye mitandao ya kijamii ni kukamatwa kwa masanduku yenye kura feki! Wengi wetu tunaamini huu ndio mwanzo tu wa lile bao la mkono ambalo tulipata kusikia likihubiriwa! Pamoja na yote hayo, je hivi ni kweli tunafahamu malengo ya hayo masanduku?

Kila kituo kina ulinzi na mawakala wa vyama! Now assume Kituo X chenye mlinzi na mawakala wa vyama vyote. Hivi ni kipi ambacho ni rahisi kati ya kununua mawakala wa vyama hasimu AU kuingiza mi-box mikubwa yenye kura feki kinyemela-- mi-box ambayo inaonekana wazi na mtu yeyote? Hizi kura hazipigwi gizani... na kabla kituo cha kupigia kura hakijafunguliwa na upigaji kura kuanza, eneo zima linakaguliwa ikiwa ni pamoja na chumba chenyewe. Sasa haya masanduku yenye kura feki yanaingiaje humo hadi kura zake kujumlishwa pamoja na kura zingine halali?Ikiwa hawa mawakala wetu watashindwa kuyaona masanduku yenye kura feki yakiingizwa kwenye masanduku halali; je kweli wataweza kuona uhesabuji wa kura zilizo halali? Kisheria, kabla ya idadi ya kura zilizopigwa kutangazwa; mawaka wa vyama vyote wata-sign kuafikia wa kura hizo... je, hizo kura feki zilizo kwenye masanduku zitasainiwa na mawakala gani?!

Kama issue ni kura, ni kwanini basi mtu asiweke hizo kura feki kwenye bahasha na kwenda kuzipenyeza kupitia wahusika waliohongwa kwenye kituo husika badala ya kupita na masanduku ambayo popote utakapotia mguu yataonekana?

Kwenye media moja ya nje imeandika; bila kujali nani atashinda kwenye uchaguzi huu; lazima machafuko yatatokea! Watu tukaichana live ile media lakini kwa mtindo huu ni kweli machafuko yanaweza kutokea! Watu hatutaki kuangalia uwezekano mwingine wa matukio haya ambayo ukiangalia kwa makini wala hayana nia ya kuiba kura bali kuvuruga uchaguzi na hatimae kuleta maafa akilini! Sina shaka zipo njia mzuri tu za kuiba kura lakini ni mwendawazimu peke yake ndie anaweza kuiba kura kwa kuingiza masanduku feki ambayo yanaweza kuonekana yeyote! Narudia... kama lengo ni ku-tally kati ya hard votes/karatasi za kura na idadi itakayoandikwa, bado kuna better way ya kufanya hivyo badala ya kutembea na masanduku barabarani! Na kama ikiwa ni kweli hayo masanduku yanakamatwa mengine yakiwa kwenye magari; hao wanaokamata wanajuaje kwamba hayo magari yamebeba ma-box kama sio hao wabebaji wali-stage ili wakamatwe? Na ikiwa wali-stage ili wakamatwe; kwanini walitaka wakamatwe kama sio kudhihirisha kwamba walibeba masanduku ya kura?

Mkuu ninavyoona linapo kuja swala la kura feki mwenye nazo atatafuta upenyo wa kuzichomeka na hasa ndo hao utakao sikia wakidai kura zihesabiwe upya!!, la msingi ni kuwa mawakala wawe makini na idadi ya waliyo jitokeza kupiga kura, narudia tena walio jitokeza kwani ndo control yao
 
Kwani wakirudia kuhesabu utaratibu unabadilika??!??
 
Ni wazi NEC, IKULU, Mahakama na Polisi kushinikiza watu wasilinde kura kitu ambacho kipo kisheria huenda walijua kitu juu ya haya yanayoendelea.
Aliyemuelewa Yeriko Nyerere kuwa "Watanzania hawahitaji amani bali wanahitaji haki" anaweza kujua kitakachokuwa kinatokea leo kuanzia mida ya alasiri.

Kulinda kura maana yake nini haswa?????
Ije hiyo alasiri. . . . . .
Na uwepo hapa
 
hueleweki kawaulize nec mbona masamnduku yao yamekamatwa mtaani??
na mbona karatasi za kura zinakamatwa kwenye magari ya serikari ???
na mbona kura zina tik ya mgombea wa ccm??

1. Yako wapi yaliyokamatwa??!! Yapo kituo gani cha polisi na namba ya jalada ni ipi??!!!
2. Sasa ulitaka yabebwe na gari za chama??!! Au wakubebeshe mgongoni??!!
3. Zilikuwa na tiki ya mgombea gani, jimbo lipi na zilikuwa ngapi??!! Tukio kama hilo enzi hizi hizo kura zisipigwe picha??!!!
 
......kwa nini wapenzi wa ccc wanasapoti sana upuuzi huu?.....
kitu kinakamatwa tena katika gari la serekali kitu batili dhahiri!
shame,shame,shame!
SURA ZAO WATAZIFICHA WAPI KIMATAIFA?
 
Lowasa aliwaahidi kazi yenu ni kupiga kura tu mengine muachieni yeye ....sasa shida ya nini wakati mnaye Mr. Magician?
 
Hakuna kura feki,kilichopo ni ukosefu wa Subira na Imani tu kwa baadhi ya watu.
Mabox na karatasi lazima zisambazwe, Nchi ni kubwa hii wakati mwingine ilibidi hivyo vitu visafirishwe mapema.
Sasa wasiokuwa na subira wakiona hivyo wanadhani eti kura bandia zimetumwa
 
Ukawa wanaweweseka wanajua kabisa wanashindwa kwa hiyo wanachotafuta ni public sympathy. Wanazusha matukio kwa uongo ili waonekane kuwa wameonewa.

Lakini kama zinakamatwa kwenye nagari ya sirikali ukawa inaingiaje huko, sijaelewa sijui tumwachie Mora.
 
......kwa nini wapenzi wa ccc wanasapoti sana upuuzi huu?.....
kitu kinakamatwa tena katika gari la serekali kitu batili dhahiri!
shame,shame,shame!
SURA ZAO WATAZIFICHA WAPI KIMATAIFA?

Tatizo mna maneno sana na kila anayewahoji basi lazima awe CCM??!!!
Kwani kubebwa na gari ya serikali kuna shida gani au hata NEC hujui maana yake???
Kitu batili kiende polisi. . . .Hayo yaliyokamatwa yako kwa majalada namba zipi na vituo gani??!!!

Ni jambo kubwa mnalotaka kulieleza ila haliiingii akilini
 
Back
Top Bottom