Masanduku ya Kura yakamatwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masanduku ya Kura yakamatwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by The King, Oct 31, 2010.

 1. T

  The King JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Masanduku ya Kura yakamatwa Sunday, 31 October 2010 14:04
  Mwananchi

  Israel Mgussi na Geroda Mabumo ,Dodoma

  HALI ya uchaguzi mkuu jimbo la Dodoma mjini imetia dosari baada ya kukamatwa kwa masanduku ya kupigia kura yakiwa na karatasi za kura kwenye nyumba ya mtu binafsi nje kabisa na kituo cha kupigia kura.

  Masanduku hayo mawili yaliyokuwa yamesheheni karatasi za kura ndani yalikamatwa juzi mtaa wa Majengo mjini Dodoma majira ya saa mbili usiku kwenye nyumba ya Mwalimu Walburga Tarimo ambaye pia ilifahamika kuwa ndiye atakayekuwa msimamizi wa kituo cha uchaguzi cha Makole kata ya makole.

  Mwananchi ambayo ilifika eneo la tukio ilishuhudia upekuzi ulioongozwa na Afisa upelelezi makosa ya jinai wa wilaya ya Dodoma mjini(OC-CID) Jonathan Shanu ambapo masanduku hayo mawili yalibainika na kuchukuliwa moja kwa moja hadi kituo cha polisi cha kati pamoja na mtuhumiwa kwa ajili kutolea maelezo.

  Baada ya kufika kituo cha polisi cha kati masanduku yalifunguliwa ili polisi na mashuhuda waweze kujiridhisha kama karatasi zilizokuwamo ndani zilikuwa zimeshawekwa alama zinazoonyesha kuwa kura zimeshapigwa au hapana.

  Hata hivyo baada ya masanduku hayo kufunguliwa karatasi zilizokuwamo ndani zilikutwa bado hazijatiwa alama ya vema wala alama yoyote inayoonyesha dhamira ya kumpigia mtu fulani kura na zaidi ya hapo mtuhumiwa alisema kuwa yeye alilazimika kurudi na masanduku na vifaa vyote vya kupigia kura kutokana na kukosekana kwa ulinzi katika kituo cha kupigia kura.

  “Mimi sikufahamu kuwa hili ni kosa na nililazimika kurudi na vifaa vyote hivyo vya kupigia kura kwa sababu giza lilishaingia katika kituo cha kupigia kura na hapakuwepo na ulinzi wowote wa askari hivyo kwa usalama wangu na wa vifaa niliamua kurudi navyo nyumbani.”,alisema mwl.Tarimo ambaye ndiye msimamizi wa kituo cha uchaguzi Makole .

  Haikuweza kufahamika sababu ambazo zilifanya mtuhumiwa ashindwe kuwasiliana na msimamizi wa uchaguzi au kwa vyombo vingine vya usalama ingawa ilibainika kuwa katika kituo husika kulikuwepo na askari ambaye alikuwa amepangwa kutoa ushirikiano wa kiulinzi na usalama katika kituo tajwa.

  Kwa upande wake msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Dodoma mjini Suzane Bidya alisema yeye hana taarifa juu ya kukamatwa kwa masanduku hayo na kusisitiza kuwa hakuna sheria inayomruhusu mtu yoyote kwenda kulala na vifaa vya uchaguzi nyumbani kwake.

  “Mimi sina taarifa hizo,hata hivyo muulize huyo mama nani kamruhusu kwenda na masanduku na hivyo vifaa vya kupigia kura nyumbani kwake,akueleze maana mimi sijatoa ruhusa hiyo na wala sina ruhusa ya kumruhusu mtu kwenda na vifaa vya kupigia kura nyumbani kwake sasa yeye kwanini aende navyo nyumbani.”,alisema Bidya.

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Steven Zelothe alipotakiwa azungumzie tukio hili alisema kuwa hakuna taarifa inayohusu tukio hilo ambayo imeshamfikia.

  Aidha baada ya mtuhumiwa kuhojiwa na kufanyika kwa uhakiki wa karatasi zilizokuwemo ndani ya masanduku hayo,yalichukuliwa na kupelekwa kwenye kituo husika cha kupigia kura chini ya ulinzi wa polisi,huku OC-CID Dodoma mjini Jonathan Shanu akisema kuwa maelezo yameshachukuliwa lakini yeye hawezi kutoa maelezo yoyote kwa sababu yeye sio msemaji wa Polisi.

  Mbali na dosari hiyo upigaji kura katika vituo mbalimbali vya majimbo ya Dodoma mjini,Bahi na Chamwino imeendelea vizuri huku kukiwa na hali ya utulivu na upigaji kura wa amani.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Haya sasa..wanaadhirika mchana peupeee!
  Watayaonyesha yooote!
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  kweli hii nchi inahitaji ukombozi, sehemu zingine uchaguzi unahahirishwa kwa kukosa karatasi, huku kwingine mtu mzima kabisa anaamua kushiriki kwenye uharifu wa kuwaangamiza watanzania wenzake
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Naogopa sije kuwa hizi geresha za kupoteza lengo ,kamata kamata ya polisi na kuwajibika kwao kikazi ni kuhamisha mawazo ,lazima tuwe macho ,hapa inawezekana kabisa ikawa panachezwa draft na mkizubaa jamaa wanakula dabo !!!
   
 5. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hayo yote ni mipango ya mungu ya kukubali maombi ya wengi ya kuleta mabadiliko
   
 6. e

  ejogo JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2010
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mambo hayo !!
   
 7. S

  Singo JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Ndio maana naamini kuwa tume si huru na si huru kweli kweli. Mungu aingilie kati
   
 8. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hapo hapana kitu!.Ni matukio tu.
   
 9. C

  Charles Joseph New Member

  #9
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda tusubili mwisho wa dunia ufike
   
 10. C

  Charles Joseph New Member

  #10
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwa hizo ndizo tamaduni ndani ya demokrasia za woga kwa nchi nyingi za kiafrika
  Hatutaweza kuacha uhalifu huu hadi mungu aingilie kati
   
 11. l

  lonesome Senior Member

  #11
  Nov 1, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 195
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  haayo masanduku yaliyokamatwa ni kwa sehem tu hiyo ambayo imekamatwa lakin wat abt those places ambapo hayakukamatwa? hivi mnadhan kuna serikal ambayo ktk EAST AFRICA itakubali kuachia madaraka kwa njia ya karatas? ni ngumu sana...ila lazima mjue tu kuna watu wanajifunza mambo haya jins gan ambavyo wananyanyasika. kuburuzwa,kukandamizwa na kuonewa...kuna siku watachoka tu watu hawa...na when we think its peace and safety...then political violence will fill our country...there..nobody will remain safe....and this will take a long time mpaka kuja kutulia...kwan wahenga pia walisema. AMAN HAIPATIKAN MPAKA KWA NCHA YA UPANGA...tanzania hamna aman bado...ni tu kuwa tumeufunika moto kwa nyasi mbichi ...hatujajua kuwa zile nyasi huwa zinapopata moto zinakauka..baadaye....
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 418,988
  Trophy Points: 280
  Panapofuka moshi panaficha moto....................
   
Loading...