Masanduku 16 yamekamatwa yakiwa na kura zilizopigwa Arumeru Mashariki

quote_icon.png
By Mungi

kwani mtu aliyenipigia hajawahi kudanganya.

uwezo wako wa kufikiri ndo utakuwa umeishia hapo..

nipe uhusiano uliopo kati ya hajawahi kunidanganya na uwezo wa kufikiri!

Shirikisha ubongo mkuu!
 
mnaosema damu lazima imwagike karibun arumeru mmwage yenu kwanza, there is only 3 option in probability, win, droor, or loose na ukishakuwa mshindani kubali both options ingekua kuna aliejihakikishia ushindi kusingekua na haja tume ya uchaguz kutumia a lot of cash to finance uchaguz ingekua wastage of resources
 
Hizi taarifa nimezipokea kwa njia ya simu, ikanifanya ni browse jf kujua kama kuna mwingine mwenye taarifa hizi.
Inaonekana ni kweli, kwani mtu aliyenipigia hajawahi kudanganya.

Mungi, kama ni kweli basi CCM wanaleta maafa Arumeru, God forbid.
 
Mungi, kama ni kweli basi CCM wanaleta maafa Arumeru, God forbid.

sasahivi naelekea Tengeru, nikifika nitaendelea kuwajuza kilichotokea kina ukweli kiasi gani. lakini aliyenipigia ni mheshimiwa sana wa Magamba, hana taarifa za kizushi, labda kama ameanza leo.
 
sasahivi naelekea Tengeru, nikifika nitaendelea kuwajuza kilichotokea kina ukweli kiasi gani. lakini aliyenipigia ni mheshimiwa sana wa Magamba, hana taarifa za kizushi, labda kama ameanza leo.
Ok, tunasubiria updates mkuu.
 
mnaosema damu lazima imwagike karibun arumeru mmwage yenu kwanza, there is only 3 option in probability, win, droor, or loose na ukishakuwa mshindani kubali both options ingekua kuna aliejihakikishia ushindi kusingekua na haja tume ya uchaguz kutumia a lot of cash to finance uchaguz ingekua wastage of resources
You are mentally impaired.
 
Haya mambo yataisha lini lakini na wanao fanya hayo wanachukuliwa hatua gani au tuchukue sheria mkoni kama tunavyo wachom vibaka
 
Wachangiaji wengi wa kupinga mageuzi na kushabikia utawala mbovu wamejiunga hivi karibuni kwa nia ya kupotosha mijadala humu. Nimechunguza wale ambao wamekazana na upotoshaji wamejiunga kuanzia March mwaka huu. Tujaribu kutojibizana nao ili tusiende nje ya mijadala, kwa vile wanafanya hivyo kwa makusudi kabisa.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amewataka wananchi kuzuia magari yatakayoingia baada ya kupiga kura, kutokana na tarifa aliyopata kuwa kuna kura zaidi ya 10,000 zimepigwa nje ya Jimbo la Arumeru Mashariki na wanatafuta jinsi ya kuziingiza.
Aliyasema hayo jana wakati akimnadi mgombea wa Ubunge wa Chama hicho, Joshua Nassari, kwenye kijiji cha Kikatiti, Nkoaranga, Sing'isi, Ngarenanyuki na King'ori.
Alisema amepata taarifa za uhakika kuwa kura tayari zimepigwa na wanatafuta namna ya kuziingiza Arumeru.
Dk. Slaa alisema mbali na kuziingiza kura hizo, pia amepata taarifa kuwa kuna polisi 300 wanaletwa kwenye vituo vya kupigia kura, badala ya kuleta mgambo na askari polisi 95 watavalishwa nguo za kiraia na watafanya kazi za kulinda kura za CCM.
"Sasa kama hawa askari wanakuja kusaidia ushindi CCM, kwa kweli narudia Tunisia ya Arumeru itaanzia hapa na patachimbika," alisema Dk. Slaa.
Alisema kuwa kutokana na wizi huo, lazima kura zilindwe na hata polisi wakipiga mabomu hawataogopa, watawapiga ili dunia ifahamu Tanzania Dk.Slaa aliagiza kuwa wapiga kura wote watakaopiga kura katika vituo vyao, wasogee mita 102 wapige kambi na wakiona gari linaleta kura feki wakamate na waite walinzi wa Chadema ili kulinda kura zao.
Alisema kuwa safari hii hawataruhusu kamwe kufanyiwa mchezo na wala hawatakwenda mahakamani bali wao ndio watakaokwenda mahakamani kudai ushindi.
Alisema kuna njama za kumtangaza Sioi kwa nguvu ili Chadema wakimbilie mahakamani, wakifahamu muda utakwisha kwa kuwa miaka michache ili watushinde, jambo hilo hawatalifanya bali watalipinga hapo hapo mpaka kieleweke.
Pia alisema kuna shahada feki zimeandaliwa eneo la Ngarananyuki, ili wapewe mabalozi wakapige kura, katika vituo kwa ajili ya kuhakikisha Sioi anashinda, pia hilo hawatakubaliana nalo.
Alisema tayari wameshafundisha mawakala wao jinsi ya kutambua shahada feki na halali, na wakigundua hawataruhusu kupiga kura mtu na patachimbika, hawatakuwa na huruma na mtu
Kuhusu Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, alisema hana muda wa kumjibu, ila anamshanga kuja Arumeru kumnadi Sioi, mkwe wake, hivyo hana uchungu na watu wa Arumeru, bali ana uchungu wa mkwe.
Alisema Lowassa ameahidi kuhamisha maji Meru na kuyapeleka Monduli, akidai kuwa kule kuna watu, hivyo Meru hakuona kama kuna watu, ila sasa anatambua kuwa kuna watu na kuanza kumnadi Sioi.
Alisema kuwa Lowassa anamnadi mkwe wake kwa manufaa yake na huku akidai ataleta maendeleo Meru, wakati ameshindwa kuleta maendeleo Meru wakati akiwa Waziri Mkuu.
Dk. Slaa alisema kuwa pia anawashangaa wabunge wa Arusha wanakiri kuisahau Meru, na kuahidi kuwa watakaa kikao baada ya uchaguzi kumalizika ili walete maendeleo, kitu alichodai ni uongo wa mchana kweupe.
Naye Joshua Nassari, alihamasisha watu kulinda kura na bila woga kujitokeza katika vituo kulinda kura zao, ili atangazwe kuwa Mbunge.
 
mnaosema damu lazima imwagike karibun arumeru mmwage yenu kwanza, there is only 3 option in probability, win, droor, or loose na ukishakuwa mshindani kubali both options ingekua kuna aliejihakikishia ushindi kusingekua na haja tume ya uchaguz kutumia a lot of cash to finance uchaguz ingekua wastage of resources

hiyo 'droor' haina tofauti na kiingilishi cha baba Mwanaasha, to manufacture tea
 
Hivi hawa ccm wanataka kutufanya sisi wote ni wajinga ,wakubari kuwa Tanzania ya miaka ya 8o imeisha yaleo tofauti na yakwao walipo kuwa wanaweka picha moja ya mtu wanemtaka na kivuli, leo sio watu wanabadilika kimsingi hatukubali hadi hizo kula zichomwe mbele za watu wote tuone watasababisha maafa yasio namaana Tanzania ya leo na watu wake wanjitambua sana tuuu
 
vijana wa nape hao mkuu, wanapost thread za kizushi halafu wanasepa. ni kama kuku anavyokunya barabarani.

nape anavijana wenye akili kama za mwanaasha

Mungi hapa kwenye nyekundu naomba usema ulimi umeteleza
 
mnaosema damu lazima imwagike karibun arumeru mmwage yenu kwanza, there is only 3 option in probability, win, droor, or loose na ukishakuwa mshindani kubali both options ingekua kuna aliejihakikishia ushindi kusingekua na haja tume ya uchaguz kutumia a lot of cash to finance uchaguz ingekua wastage of resources

"draw" is the correct spelling for droor
 
Back
Top Bottom