Masalia kuchomwa kesho, wakazi watakiwa kuondoa hofu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
ESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), linatarajia kuchoma masalia na baruti ya mabomu yaliyobaki katika kambi ya Jeshi Gongo la Mboto.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Makao Makuu ya JWTZ iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam ilisema, masalia hayo yatachomwa kwasiku mbili ambapo ni kesho na keshokutwa.

Na yataanza kuchomwa kuanzia saa 3. asubuhi hadi saa 6 mchana, katika kambi hiyo ya Gongo la Mboto.

Hivyo wananchi wametakiwa kutokuwa na hofu, kwani hakutakuwa na madhara ya aina yoyote katika zoezi hilo na kutakiwa waendelee na shughuli zao za ujenzi wa taifa kama kawaida.
 
Hadi watu wafe ndiyo waone kuwa kuna umuhimu wa kuyateketeza hayo mabomu yao yaliyo-expire. Wabongo bana
 
Back
Top Bottom