Masaki na Oysterbay kuna nini mbona hakuna hata Mbu, Inzi, Paka wala Mbwa wanaokatiza kama siku zote?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,976
2,000
Kuna Mtaa mmoja ulikuwa ukipita muda wowote ule utakaribishwa na ' Mijibwa ' hadi utakoma ila tangia jana Usiku hadi muda huu najiuliza hao Mbwa wameenda ' Likizo ' au Wazungu wetu wawili wa Tandale na Kwa Mnyamani waliondoka nao ile Saa 11 alfajiri?

Mnao kaa huko Masaki na Oysterbay hebu tuambieni Sisi wa ' Uswahilini / Uswazinyo ' kulikoni mbona tunasikia hakuna cha Inzi, Paka wala Mbu anayekatiza hovyo huko? au Rais wa Marekani na Dunia Donald Trump anatarajia kufanya Ziara ya ' Kushtukiza ' nchini Tanzania hivyo wale Wazungu wake wanaimarisha Ulinzi hadi kule Ubalozini Kwao?

Kuna nini huko?
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,976
2,000
Msako sio wa kitoto, hata kama huyo mbu anakipisi cha bangi kaficha kwenye msambwanda, atakitoa tu

Wanasaka nini Mkuu? Manake Mimi mwenyewe japo nipo huku Makazi Kwangu Kisiwani Puerto Rico ila nina Watanzania Marafiki zangu wapo huko Kwenu Dar es Salaam na wanaishi Masaki na Oysterbay wanasema kama ' Ulinzi ' wanaouona leo na hata jana ungekuwepo Siku zote basi Wananchi wengi wa maeneo hayo wasingekuwa wanaporwa hovyo Simu zao, Pochi zao na hata Laptops zao.

Hebu naomba wale wana JamiiForums wanaoishi huko waweze kutueleza ukweli juu ya hili tafadhali.
 
Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,256

Jaribu kumcheki kwa simu RC Makonda, atakupa jibu kamili, maana nae anaishi huku pia.
 
babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
8,005
2,000
Zamani mitaa hiyo ilikua balaa hukatizi.
Kuna dokumentary baada ya uhuru jamaa walihamia mpk na ng'ombe, bata,mbuzi, bustani ya maua wakapanda mchicha na majani ya maboga.
Watu wangu hawa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom