Masahihisho:Wafadhili watoa asilimia 69 ya matarajio

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,498
3,465
Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesema kwa kipindi cha Julai mwaka jana hadi Januari 2019 imepokea Sh1.03 trilioni kutoka kwa wadau wa maendeleo zilizotolewa kama msaada na mkopo.

Kiwango hicho ni sawa na asilimia 69 ya Sh1.48 trilioni ambazo ziliahidiwa na washirika hao wa maendeleo kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo katika kipindi cha miezi saba kati ya Julai 2018 na Januari 2019. Mtandao wa Mwananchi uliandika kimakosa kuwa asilimia hizo ni 6.7.

Hayo yamesemwa jana Jumanne, Machi 12, 2019 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango wakati akiwasilisha mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

“Kati ya kiasi kilichotolewa, misaada na mikopo nafuu ya Kibajeti ilikuwa Sh125.4 bilioni na miradi ya maendeleo Sh782.0 bilioni. Mifuko ya Kisekta ilipokea Sh127.4 bilioni,” alisema.

Katika mwaka huo wa fedha Serikali ilitenga Sh12 trilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo zikijumuisha Sh9.8 trilioni ambazo ni fedha za ndani na Sh2.1 trilioni za nje.

Dk Mpango alisema Sh2.7 trilioni zilitolewa na Serikali kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo hadi kufikia Januari 2019.

Waziri huyo alisema Sh3.8 trilioni zilitumika kulipa mikopo iliyotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Serikali imeshatenga na inatarajia kutoa kiasi cha Sh1.4trilioni kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo wa kufua umeme kwa kutumia nguvu ya maji ya Mto Rufiji (MW2,115),” alisema.

Aidha katika bajeti ya Mwaka 2018/2019 Washirika wa Maendeleo wanatarajiwa kuchangia Sh2.68 trilioni ambayo ni asilimia 8.2 ya bajeti yote (Sh32.48 trilioni).

Misaada na mikopo hii inajumuisha misaada na mikopo nafuu ya miradi ya maendeleo Sh2.0 trilioni, mifuko ya pamoja ya kisekta Sh125.9 bilioni na misaada na mikopo nafuu ya kibajeti Sh545.8 bilioni.

Tunasikitika kwa habari ambayo ilichapishwa katika mitandao yetu jana na kuonyesha kuwa wahisani wamechangia asilimia 6.7 mpaka Januari. Sh144 bilioni ambazo tulizitumia katika habari hiyo ni fedha ambazo wahisani wamechangia moja kwa moja katika miradi ya maendeleo, hazijumuishi misaada na mikopo mingine.

Kumradhi
 
daah kazi kweli kweli, ko hivi vitabu kabla ya kuvigawa hawakuvipitia??
IMG_20190313_152629.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama Mabeberu yametoa 69% ina maana serikali imechangia 31% tu, dah haya mabeberu hayakwepeki.
Nawe ni mbumbumbu tu, hiyo ni 69% ya hela iliyohaidiwa na wahisani na sio ya bajeti yote jumla. Bajeti ya Tz ni 30trilioni huko, pesa ya wahisani ni 2.4trilioni.
 
Kama Mabeberu yametoa 69% ina maana serikali imechangia 31% tu, dah haya mabeberu hayakwepeki.
Elewa kinachoandikwa sio unakimbilia kureply uharo wako ni aibu! Wahisani kutoa 69% ina maanisha kama serikali ilihitaji trillion 2 wangepata zote sawa na kusema wahisani wametoa 100% ya kile serikali ilikihitaji kutoka kwao lakini kwakuwa wametoa Trilion 1.6 basi sawa na 69% ya kile kilicho hitajika toka kwao ila kwasasa bajeti ya Tanzania kiujumla wahisani wanachangia wa 8.2 tu ya bajeti yote, It means 98% ya bajeti yetu kwasasa ni fedha kodi yetu wananchi.
 
Kama Mabeberu yametoa 69% ina maana serikali imechangia 31% tu, dah haya mabeberu hayakwepeki.
Mbona unapenda kujitoa ufahamu, kwenye bajeti waliahidi kuchangia asilimia 2 ya bajeti yote, yaani katika trioni 32 wao wangetoa 2.5 tirion.....lakini kwenye hiyo trilioni 2.5 wametoa asilimia 69...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom