Masahihisho daily news kuhusu mikutano ya siri ya TANU

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,913
30,255
MASAHIHISHO KATIKA DAILY NEWS MAKALA YA MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA

Gazeti la Daily News la leo Jumatatu tarehe 15 November, 2021 ukurasa wake wa mbele kuna picha ya nyumba ya Mwalimu Nyerere aliyokuwa akiishi Magomeni Mtaa wa Ifunda.

Makala inasema mikutano ya siri yote wakati wa kupigania uhuru ilikuwa ikifanyika katika nyumba hii.

Mwandishi amekosea.

Mwalimu alijenga nyumba hii mwaka wa 1958 na kabla ya kuhamia nyumba hiyo Mwalimu alikuwa akikaa nyumba moja jirani na hapo pakiitwa Maduka Sita, Morogoro Road.

Mwalimu alihamia nyumba hii Maduka Sita baada ya kutoka nyumbani kwa Abdul Sykes Kariakoo alipokuwa anaishi baada ya kuacha kazi ya ualimu mwaka wa 1955.

Hata hapo maduka sita Mwalimu alipohamia mwaka wa 1955 hapakuwa na mikutano yoyote ya siri iliyokuwa ikifanyika ndani ya nyumba ile.

Mwalimu alipohamia nyumba hiyo mwaka 1958 hakukaa sana hapo hata mwaka haukufika akahamia Sea View na wakati huo TANU haikuwa inaishi katika enzi zile kabla ya Uchaguzi wa Kura Tatu mwaka 1958.

Zile zilikuwa nyakati za uhasama.

Mikutano ya siri yote ya TAA hadi kufikia TANU ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu.

Nyakati zile zilikuwa nyakati za mapambano.

Screenshot_20211115-221622_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom