Ni brand ipi ya battery ya gari kwa sasa ambayo iko imara?

nyambari

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
355
171
Masada wana jamvi ni brand ipi ya battery ya gari kwa sasa ambayo iko imara na itaweza himiri kusukuma woofer 1000 watts bila tatizo?
Nilikuwa natumia acdeldo N40 ila naona ishakuwa kimeo.
Tafadhali nipate brand pendekezwa pamoja na bei elekezi.
Asante.
 
Binafsi napendekeza uangalie
1. Index...hizi ni za India...nilinunua dry ikadumu miaka miwili na miezi nane ikafa...bei niliuziwa 140000 Arusha.

2.Atlas...hii ndiyo natumia kwa sasa..inatoka Korea..nayo ni dry..hii kwa sasa ina mwaka na miezi sita tangu niinunue...bado haijaanza kunisumbua....hata nikipaki gari wiki nzima nikija ni jino moja tu . Hii nilinunua 120000 Arusha

NB..zote ni N40.

Kuwa makini nasikia Atlas fake zimeshaenea sana mjini.
 
Back
Top Bottom