Msaada tafadhali, kwa anaefahamu taratibu za kabila hili

Akilimali tz

Member
Feb 7, 2021
9
9
Wana jamvuni salaam,

Katika pitapita yangu nilibahatika kupata mtoto na binti wa kisukuma, kwa mujibu wa maelezo yake alidai kuwa ujauzito wa huyo mtoto mi ndo muhusika sikuweza kataa kwa sababu yeye ndo anafahamu ukweli upoje.

Cha ajabu baada ya kujifungua sikushirikishwa kuhusu jina la mtoto wakampatia jina ambalo silifahamu kuanzia la mtoto hadi ubini siyatambui nilipojaribu kuhoji nikaambiwa kwa utaratibu wa kabila lao mtoto anayezaliwa nje ya utaratibu huo ndo huwa utaratibu wao.

Baada ya hayo kujiri nikashindwa kabisa kutoa ushirikiano juu ya malezi ya huyo mtoto kwa 100% kimsingi sijielewi nipo sahihi au sipo sahihi naombeni msaada kwa anae fahamu utaratibu wa Kisukuma.
 
Kuna watu watakuja kukung'ong'a kua umeandika vibaya ila mimi naona jinsi ulivyo pambana kuwasilisha.

Kwenda kwenye mada :huyo mtoto sio wako unapigwa stukaaa.
 
Kuna watu watakuja kukung'ong'a kua umeandika vibaya ila mimi naona jinsi ulivyo pambana kuwasilisha.

Kwenda kwenye mada: huyo mtoto sio wako unapigwa stukaaa.
Mwambie tu ukweli mkuu kabebanisha sana maandishi na yeye tunaomba kujua ukweli wa elimu yake mkuu.
 
Mkuu pole ila kama ulivyokwisha ambiwa hapo mwanzo achana nae hapo huna mtoto.

1. Kama mtoto kapewa jina kutokana na mila na desturi zao manake wewe huna kitu ukitaka kutumia nguvu kumchukuwa yatakayo fwata siamini kama ni mazuri.

Ushauri wangu koz umesema toka mwanzo uliacha toa ushirikiano basi endelea kukaa pembeni kwa usalama zaidi.
 
Asante mkuu
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom