Masaburi na mkutano wa SIRI Courtyard hotel na wahariri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masaburi na mkutano wa SIRI Courtyard hotel na wahariri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Aug 23, 2011.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Wana JF, Meya wa Dar bwana Didas Masaburi baada ya kuelemewa na tuhuma nzito za kashfa ya UDA ijumaa iliyopita alifanya mkutano na wahariri wa vyombo vifuatavyo vya habari kwenye hoteli ya courtyard. Ajenda kubwa ilikuwa kuangalia uwezekano wa wao kupata bakhshishi za pesa including za matangazo ili wajaribu kurudisha upepo juu ya hii kashfa ya UDA

  Sasa inaonekana kuna watu washavunja ranks toka kwenye team yake bwana Masaburi na zile ahadi kemkem zilizotolewa inaonekana wenye vyombo vya habari vyenye kelele sana wamepata zaidi ya wenzao na sasa washaanza kutajana na hiyo milungula ambayo imeandaliwa ili kusawazisha mambo na kupindisha ukweli.

  Wahariri waliohudhuria walitoka:

  UHURU RADIO na GAZETI
  GAZETI LA CHANGAMOTO
  CHANNEL 10
  STAR TV
  RADIO FREE AFRICA
  RADIO ONE
  ITV
  HABARI LEO
  DAILY NEWS
  TANZANIA DAIMA
  MWANAHALISI

  hii inathibitisha kuwa hawa watu wa MAINSTREAM MEDIA ni part of the problem kwani bila haya wanakubali kuitwa kwenye vikao vya kupewa rushwa na kununuliwa misosi pale Courtyard Hotel ili wapate kupindisha ukweli kuhusu hili sakata la UDA na kumpunguzia Presha Meya. Sasa katika hiin war chest ambayo inatazamwa na Bwana Iddi Simba kupitia kwa jamaa yake ni kununua airtime na kampeni zakumsafisha Masaburi, Iddi Simba na uongozi mzima wa ofisi ya mstahiki meya.

   
 2. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #2
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  I see, kumbe ndiyo mambo yenyewe!
  Basi kwa mtindo huu tusitarajie jipya...
   
 3. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kama wote hao walihudhuria sioni usiri unatoka wapi.
   
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  part of the problem...mbaya zaidi hata INVISIBLE hawakumuita ku attand kwani wanaona JF haina influence yoyote ile
   
 5. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,893
  Likes Received: 5,346
  Trophy Points: 280
  tuhakikishie kuwa wameahidiwa rushwa
   
 6. Matango

  Matango JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kuna haja Kwa Jamii Forum kuhudhuria mikutano kama hiyo ili tupate habari kwa kina
   
 7. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kumbe lengo lako lilikuwa kusema hivi....
   
 8. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kama SIRI unaisema mbele ya vipaza sauti, tena vikiwa "ON" basi si siri tena. Labda kama neno siri limebadili maana!
   
 9. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 636
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35

  First i don't understand the whole of your story kwani haieleweki na taarifa ulizoleta hapa zinaonekana na wewe ni mhusika katika hao walioongwa labda "deal zimepishana tu".Pia naomba kuwa tofauti na wewe juu ya Masaburi,sincerely the guy is more better than those who owned UDA and make dead of it.Tusiwe wa kulaumu tu,waliokuwa wanaisimamia UDA walikula ngapi mpaka ikafa na kuanza kuuza rasilimali nyingine eti kusupport?

  Mtu huyu ameweza kuonyesha ukomavu wa uongozi kwa kupitia miradi yote inayoliwa kinyemela na wajanja wachache.Tazama mchina kariakoo analipa milioni mbili laki nne kwa mwezi, wajanja wanawasilisha laki 3 haya tungeyajua bila ya Masaburi?

  UDA tunayoililia ilikwisha tufia mikononi na viongozi hao hao.Bora Masaburi ata kama ni mwizi (sina uthibitisho) kuliko waliojifanya si wezi huku wamefilisi mali zetu.No matter UDA inakuwa owned na nani,sisi tunachotaka ni huduma bora na ya uhakika Dar es salaam japo ubovu wa miundo mbinu unachangia.
   
 10. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Dah hiyo 'title' imenishtua sana baadaye nikakumbuka kumbe ni jina la mtu. Vijana humu jamvini hatari sana yaani wanaweza wakabadili kabisa matumizi ya jina la mtu. Ha ha ha ha ha ha haaa
   
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu ungefanya uhariri wa hii habari. Ni nzito kueleweka
   
 12. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  mayor na aliwaalika kama walikubaliana suala la rushwa basi wote wanafikiria kwa kutumia masaburi yao
   
 13. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  dont judge book by its cover subiri kesho mwanahalisi litaandika nini kuhusu masaburi..
   
 14. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Anaweza kuwa mjinga lakini si mpumbavu kiasi hicho; kuna media hapo ambazo wahariri wake wangevuna heshima zaidi kuanika uozo kama huo kuliko kuchukua vijimilioni vya vocha!!!!! Nashawishika kusema umetumia MASABURI kuanzisha hii thread!
   
 15. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,554
  Trophy Points: 280
  mleta thread namuheshimu sana,msikilizeni!
   
 16. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ili litimie andiko lililonena yaliyofichika hatimae yatawekwa hadharani!
   
 17. S

  Sam Seaborn Member

  #17
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duh!

  Sasa nimeivulia kofia JF hivi nyinyi kuna jambo linaendelea mji huu msilojua?

  Hii habari ina ukweli wa Asilimia 150 na naona mleta habari hakueleza kila kiitu kilivyokuwa. Kule nyumae kile chumba cha mkutano kulifanyika kikao kingine cha watu 5 tu (Meya na watu wake 5). Pesa hazikuahidiwa openly ina nijuavyo kuna wahariri 4 wa magazeti "utaratibu" ushaanza kufanywa japo si moja kwa moja.

  Haya mambo ya Internet kwa kweli yanarahsisha sana issues. Once again JF mko mbele kwenye kutuletea ya jikoni.

  Much respect!
   
 18. U

  Uswe JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nilikuwepo Movenpick kwenye mdahalo wa UDA, baada ya kongamano Kubenea akawa anachat na bwana kisena, yaani kama marafiki flani wa muda mrefu, nikahisi katika toleo linalofata halitakua na kitu na kweli jumatano ilopita mwanahalisi lilikua kimya kabisa kuhusu UDA, kubenea inabidi kuangalia upya mustakabali wa gazeti
   
 19. f

  friendsofjeykey Senior Member

  #19
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Inawezekana ikawa Invisible hana tabia za kujipendekeza na kuwa cheap kwa hawa mafisadi ndio maana hakuitwa.
   
 20. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jerry Slaa alikuwepo au?

  mimi sikuzote nimekuwa nikisema media yetu ni ovyo na mkombozi aliyebaki ni JF peke yake bas!

  sasa nyie JF mnakuwa mnajua vipi haya mambo?
   
Loading...