Masaada tatizo la mwili kupiga shoti

samilakadunda

JF-Expert Member
Oct 13, 2011
1,780
354
Nawasalimu wadau, naomba ushauri ndugu yangu anateswa na hali ya kupigwa shoti mwili Mzima, hali hiyo hutokea kama sekunde 30 , baada ya hapo unakuwa na hali ya kusikia kizunguzungu na kichwa kuuma sana, Naomba msaada wa matibabu na ushauri.
 
Ilishawahi kunitokea nikigusa chuma
Pia hata mimi huwa inanitokea, endapo nikatumia sana PC, niligundua PC au charger ya PC itakuwa na tatizo, maana hata nikiwa natumia halaf akaja kunishika mtu😁😁 atakula spark⚡
 
Pia hata mimi huwa inanitokea, endapo nikatumia sana PC, niligundua PC au charger ya PC itakuwa na tatizo, maana hata nikiwa natumia halaf akaja kunishika mtu atakula spark
Pia nilikuwa natumia sana PC kipindi hicho
 
Hiyo hali nilikuwa nayo, naona iliisha yenyewe.

Na nikiwasimulia watu walikuwa hawanielewi hata. Matumizi ya PC inaweza kuwa chanzo, hasa ambazo zimevuka muda wa matumizi.
 
Kuna kipindi mimi ilikuwa hata kupeana mkono na mtu naogopa maana napigwa shot hadi walioko pembeni wanashangaa nimeruka nini.
Yani ilikuwa nikigusa chuma, ukuta au nikimgusa mtu napigwa shoti. Kinachoshangaza sio mara zote ila ni mara moja moja
Ilishawahi kunitokea nikigusa chuma
 
Nilitegemea majibu ya mleta bandiko yangeanza kutiririka....ila kila mtu anaelezea tena yale yale alivyopigwa shoti.

Kwa sababu mimi mwenyewe nasubiria kujibiwa kupitia hapa,sio kwamba hatujapigwa....


Jee? Mlijinasua vipi hali ikawa vizuri!?

Any way,ngoja tuzidi kuona kama muafaka utapatikana.
 
Nawasalimu wadau, naomba ushauri ndugu yangu anateswa na hali ya kupigwa shoti mwili Mzima, hali hiyo hutokea kama sekunde 30 , baada ya hapo unakuwa na hali ya kusikia kizunguzungu na kichwa kuuma sana, Naomba msaada wa matibabu na ushauri.

Kwenye mifumo yetu ya fahamu, kuna kiasi cha umeme kinachowezesha mfumo wa mawasiliano mwilini kufanya kazi. Hii huusisha pia kiasi cha madini mbalimbali ndani ya mwili.

Kuna uwezekano wa uwezo wa kasoro kwenye mishipa ya fahamu. Kwa sehemu gani ndo kitu kinachohitaji kufatiliwa. mfano: kwa wale wanaopata kifafa, kasoro inayoleta shoti moja kwa moja huusishwa na ubongo.

Kutokana na kwamba hatujakusanya mambo mengine mengi, yanayoweza kupunguza wigo wa tathimini ya ugonjwa husika. Hivyo, ni vyema kufika hospitali na kwa uwezekano mtu wa kwanza kumuona napendekeza awe ni physician/daktari bingwa wa magonjwa ya ndani au daktari bingwa wa mishipa ya fahamu/neurologist.

Historia ya imeanza lini, kuongeza kwa hali husika, vitu vinavyofanya itokee zaidi, mambo mengine au falili zinazoandamana na hali husika, nini hutokea baada shoti, kwa muda gani, maisha yake kwa ujumla, ajali, kazi, matumizi ya dawa zozote, matumizi ya pombe ni vyema kuandaliwa vizuri.
 
Ipo hivi wadau. Mwili una nishati ya umeme kwenye mishipa ya fahamu yaan nerves cells au neurones. Kazi ya hizi nerve cells ni kupasha mwili habari. Moyo wa mwanadamu unategemea umeme unaopatikana ktk nerves ili mapigo ya moyo yawepo daima. Pindi mapigo ya moyo yanavyokwenda chini na kukaribia hatari ya kupoteza uhai hapo ndipo mfumo wa fahamu yaan ubongo, uti wa mgongo na nerve cells zake hupiga mwili mzima shoti kupitia misuli ya mwili yote smooth, skeletal na cardiac muscles za moyo ili moyo urudi ktk hali yake ya kawaida kuendesha mapigo. Kitaalamu inaitwa myogenic movements.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom