Marufuku ya watumishi wa uma katika siasa ni kwa upinzani tu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marufuku ya watumishi wa uma katika siasa ni kwa upinzani tu?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ruge Opinion, Jun 2, 2011.

 1. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Katika gazeti la Mwananchii la leo (uk.2) kuna taarifa kutoka Makete, Iringa, kuwa watumishi watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete wamesimamishwa kazi kwa sababu ya tuhuma ya kujihusisha na maswala ya siasa katika uchaguzi mkuu uliopita. Mkurugenzi Mtendaj wa Halmashauri hiyo anadai kuwa hatua hiyo imechukuliwa "baada ya CCM kulalamika kwamba watu hao walishiriki katika kampeni za uchaguzi, kinyume na kanuni za utumishi wa uma". Swali, hivi hilo linakuwa kosa kwa wanaojihusisha na vyama vyote au wale wanojihusisha na upinzani tu? Maana haiingii akilini kuwa CCM wanaweza kulalamikia wale waliowasaidia katika kampeni. Katika mikoa mingi maofisa wa serikali kuu, serikali za mitaa, polisi, usalama wa taifa, n.k. walishiriki katika kukibeba CCM ikiwemo kutumia raslimali za serikali kama magari katika kampeni za CCM. Tunakumbuka hata ndege ya serikali ilivyotumiwa kumzungusha Salama Kikwete akimkampenia mme wake. Je, hao wote watachukuliwa hatua kama hizo? Ushauri wangu kwa CHADEMA (na vyama vingine vya upinzani ambavyo siyo matawi ya CCM) ni kukusanya ushahidi na kufungua kesi dhidi ya maofisa wa serikali walioshiriki katika kampeni za CCM katika maeneo mbalimbali ili haki itendeke kwa wote. Vile vile hao maofisa wa Makete wasaidiwe katika mapambano yao. Vinginevyo 2015 watu watakuwa na woga.
   
 2. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Zanzibar waliitumia sana mbinu hii ya kuwafukuza kazi serikalini waliokuwa watumishi wa umma lakini haikusaidia kuwafanya watu wasiwe wana CUF, sana sana inazidisha chuki na tabaka miongoni mwa watanzania huru. Mtumishi wa umma akiisha rudi nyumbani kwake ana uhuru wa kumchagua na kumpigia kampeni mtu yeyote yule katika nchi ya demokrasia. Wanawaonea wale wasiojua haki zao, ila kwa kuwa limewekwa wazi basi ni dhahiri wahusika watalifanyia kazi.
   
 3. N

  Nanu JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama kuna raslimali za umma walizitumia kisiasa basi wadaiwe na hii iwe na kwa nchi nzima. Watumishi wote wa serikali ambao pia ni watumishi wa Chama pia washughulikiwe akiwamo Chiligati na wenzake!
  Nadhani kuna mambo mengine ya kukurupuka lakini itakuja kuiharibu nchi. Kama mtumishi hajatumia ofisi yake kwa ushabiki wa kisiasa lakini yeye kama mtu ameonyesha mapenzi yake kwa Chama au mtu fulani sidhani kama ni dhambi la sivyo basi watumishi wa umma wasingetakiwa kupiga kura ambayo pia itakuwa ni kuvunja katiba. Nadhani hili liangaliwe kikatiba zaidi ili isiwe silaha ya kuwatisha wananchi na watumishi wa umma ili wahujumu vyama vingine kwa kuibeba chama tawala. Mimi binafsi siamini kama kuna Chama kitatawala Tanzania milele hivyo tuweke misingi ambayo haibagui ili kesho na kesho kutwa ikiwa ndiyo wakati wako wa kuwa mpinzani basi uwe umeweka uwanja mzuri wa kupambana kisiasa.
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Jun 3, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kuna wakati nasema taifa hili limemiss jambo moja tu ili liendelee , tumemiss kuchapana , japo kwa 3years , watakao baki hai wataheshimiana na hakika taifa litatamalaki.
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hawa CCM bwana, wananikumbusha kauli ya CCM kwamba ukitaka mambo yake yakunyookee basi pandisha bendera ya CCM. Wamesahau kuwa yana mwisho na mwosha huoshwa....

  Kwa nini nguruwe awe haramu kwetu tu na si kwao na kwetu?????? Kwa uchokozi huu itakuwa bora wakaoneshwa rangi zoooote zilizoko katika hii dunia!!
   
Loading...