Marufuku ya siasa mpaka 2020 iondolewe

mume wa mtu

JF-Expert Member
Aug 11, 2015
653
386
Jambo hili liko wazi na ningeomba tumshawishi aliyeweka marufuku ya kufanya siasa kwamba sasa ni kazi tu siasa ni mpaka 2020 atafakari na ajitathmini kuona kama kweli kauli yake hiyo ina mashiko au lah?

Tumeshuhudia hapa matokeo ya uchaguzi mdogo,ni kwamba moja ya sababu hata kama ni ndogo iliyowaangusha vyama vya upinzani kwenye uchaguzi huu ni kutokuwepo kwa uwanja sawa wa kufanya siasa.

Vyama vya upinzanzani vimezuiwa kufanya siasa hata mikutano ya ndani ilipigwa marufuku mpaka waliopiga marufuku hiyo walipojisikia halafu mara uchaguzi mdogo huu hapa utegemee upinzani ushinde kweli?

Hiyo itakuwa sawa na bondia umfunge mkono mmoja kwenye bomba halafu pambano lianze umpige utoke hapo unashangilia?utakuwa unawalakini.

Kwa mantiki hiyo tumeona kumbe kazi za siasa sio tu uchaguzi ukiisha kwahivyo ningeomba agizo la marufuku shughuli za siasa lifutwe vinginevyo isemwe wazi kwamba vyama vya siasa havitakiwi Tanzania ili watu wajue.
 
Acha maigizo,
Mbowe na Lowasa wanadhurura kila siku mikoani kufanya siasa na chaguzi mbalimbali hadi wakamkata Ole Sosopi,

Unataka ufanye siasa ipi tena??

Au unataka siasa ile ya kuandamanisha na kushindisha juani watoto wa wenzio??
Hata MWL NYERERE alifanya siasa enzi za ukoloni.
 
Kamanda sijui ulikua bado hujazaliwa. Siasa za maandamano zilikuepo. Chama kikuu cha upinzani kilitumia chopa 3 na kikaambulia madiwani wa 3 tu kati ya 25 ambapo ccm irishinda viti 23.
 
Jambo hili liko wazi na ningeomba tumshawishi aliyeweka marufuku ya kufanya siasa kwamba sasa ni kazi tu siasa ni mpaka 2020 atafakari na ajitathmini kuona kama kweli kauli yake hiyo ina mashiko au lah?
tumeshuhudia hapa matokeo ya uchaguzi mdogo,ni kwamba moja ya sababu hata kama ni ndogo iliyowaangusha vyama vya upinzani kwenye uchaguzi huu ni kutokuwepo kwa uwanja sawa wa kufanya siasa.vyama vya upinzanzani vimezuiwa kufanya siasa hata mikutano ya ndani ilipigwa marufuku mpaka waliopiga marufuku hiyo walipojisikia halafu mara uchaguzi mdogo huu hapa utegemee upinzani ushinde kweli?hiyo itakuwa sawa na bondia umfunge mkono mmoja kwenye bomba halafu pambano lianze umpige utoke hapo unashangilia?utakuwa unawalakini.

kwa mantiki hiyo tumeona kumbe kazi za siasa sio tu uchaguzi ukiisha kwahivyo ningeomba agizo la marufuku shughuli za siasa lifutwe vinginevyo isemwe wazi kwamba vyama vya siasa havitakiwi Tanzania ili watu wajue.
Katiba inasema nini kwanza?
Huwezi kupiga marufuku kitu kilicho ndani ya KATIBA.
Hivi ni kusema Upinzani HAWAJIELEWI tu ama ni WAOGA na SHERIA HAWAIJUI!

Si vizuri nchi kuiweka katika ELECTION MOOD/Hali ya KIUCHAGUZI CHAGUZI kila wakati.
Hivi nafikiri ndo iliyoshauriwa isitishwe.

Maana wananchi hawawezi kumaliza uchaguzi halafu waigiziwe gia nyingine na waanze tena siasa siasa kwa muda wote wa miaka 5.
SWALI?
Watalima saa ngapi?
Watazalisha saa ngapi?.
Kila jambo LAZIMA liwe na muda wake.

Hata hivyo kama kuna jambo la kukutana na wanachama wa chama fulani na mtu UKAKAMATWA kwa KUONEWA, jamani SHERIA si ZIPO? MAHAKAMA itatafsiri kama umevunja sheria ama la.
Badala ya kulia lia oh Magufuli amesema oh sijui nani.
Hii NCHI si ni yakufuata Sheria????
And NO EXCEPTIONS/ HAIMBAGUI mtu YEYOTE ili mradi HAVUNJI sheria.
MAHAKAMA ni lazima ITAFSIRI kila jambo kama liko kisheria. Kulaumu laumu hakutasaidia!

Kwani sisi watanzania tuna shida gani? Je ni ufahamu mdogo?
 
Kamanda sijui ulikua bado hujazaliwa. Siasa za maandamano zilikuepo. Chama kikuu cha upinzani kilitumia chopa 3 na kikaambulia madiwani wa 3 tu kati ya 25 ambapo ccm irishinda viti 23.
hujasoma vizuri,mada inasema huwezi kuzuia wengine wasifanye siasa mpaka uchaguzi ufike wakati wewe unafanya siasa muda wote.
 
Wafanye shughuli za maendeleo uone kama kuna atakae wazuia. Siasa za maneno matupu zimepitwa na wakati.

Siasa ya kusubiri rais afanye kitu wao walete kituko. Wasubiri rais aseme neno wao waseme maneno. Siasa hizo hakuna anaezitaka. Hizo tubaki nazo humu humu kwenye mitandao
 
Katiba inasema nini kwanza?
Huwezi kupiga marufuku kitu kilicho ndani ya KATIBA.
Hivi ni kusema Upinzani HAWAJIELEWI tu ama ni WAOGA na SHERIA HAWAIJUI!

Si vizuri nchi kuiweka katika ELECTION MOOD/Hali ya KIUCHAGUZI CHAGUZI kila wakati.
Hivi nafikiri ndo iliyoshauriwa isitishwe.

Maana wananchi hawawezi kumaliza uchaguzi halafu waigiziwe gia nyingine na waanze tena siasa siasa kwa muda wote wa miaka 5.
SWALI?
Watalima saa ngapi?
Watazalisha saa ngapi?.
Kila jambo LAZIMA liwe na muda wake.

Hata hivyo kama kuna jambo la kukutana na wanachama wa chama fulani na mtu UKAKAMATWA kwa KUONEWA, jamani SHERIA si ZIPO? MAHAKAMA itatafsiri kama umevunja sheria ama la.
Badala ya kulia lia oh Magufuli amesema oh sijui nani.
Hii NCHI si ni yakufuata Sheria????
And NO EXCEPTIONS/ HAIMBAGUI mtu YEYOTE ili mradi HAVUNJI sheria.
MAHAKAMA ni lazima ITAFSIRI kila jambo kama liko kisheria. Kulaumu laumu hakutasaidia!

Kwani sisi watanzania tuna shida gani? Je ni ufahamu mdogo?
HAYO ya election mood unayasema wewe,sisi tunasema shughuli za siasa kama anavyofanya muheshimiwa rais kwa wapinzani zinazuiwa kama kusalimia,kuongea na wananchi tumeshuhudia alichofanyiwa LOWASA huko geita tena akiwa katika harakati za kampeni je ingekuwa hakuna uchaguzi?ninachosema haiwezekani usiwapitie wananchi kujua mahitaji na changamoto zao usubiri wakati wa kampeni hawawezi kukuelewa sasa vyama vya upinzani vinazuiwa kufanya hivyo ndio maana nimesema hakuna uwanja sawa wa kufanya siasa.
 
Wafanye shughuli za maendeleo uone kama kuna atakae wazuia. Siasa za maneno matupu zimepitwa na wakati.

Siasa ya kusubiri rais afanye kitu wao walete kituko. Wasubiri rais aseme neno wao waseme maneno. Siasa hizo hakuna anaezitaka. Hizo tubaki nazo humu humu kwenye mitandao
shughuli gani ya maendeleo utaifanya bila kumobilize wananchi?kwa mfano yani aje mwenyekiti wa CHADEMA na mwenyekiti wake wa serikali ya mtaa wa eneo fulani waanze kutandaza mabomba labda ya maji bila kuwashirikisha wananchi hiyo inawezekana?maana ni lazima kabla ya kufanya hivyo uitishe mkutano na wananchi ili mjadili kuhusu mradi husika ndio utekelezaji ufanyike sasa hapo kwenye mkutano ndio wanaojiona wenye nchi hawaitaki
 
Mkuu sema munahitaji siasa za maandamano. Kwani wawakilishi kwenye majimbo wamezuiwa kufanya siasa kwenye maeneo yao?.
 
Acha maigizo,
Mbowe na Lowasa wanadhurura kila siku mikoani kufanya siasa na chaguzi mbalimbali hadi wakamkata Ole Sosopi,

Unataka ufanye siasa ipi tena??

Au unataka siasa ile ya kuandamanisha na kushindisha juani watoto wa wenzio??
Mzee mwenye nywele nyeupe aliwashindisha juani watu pale jangwani kuanzia saa tatu asubuhi halafu saa kumi na moja anawaambia wakitaka kuzifahamu sera zake waende kwenye tovuti.

Kama suala ni kuzijua sera kupitia tovuti, kulikuwa na haja gani ya kuwashindisha juani watoto wa kimaskini wasio hata na uhakika wa mlo mmoja?.
 
HAYO ya election mood unayasema wewe,sisi tunasema shughuli za siasa kama anavyofanya muheshimiwa rais kwa wapinzani zinazuiwa kama kusalimia,kuongea na wananchi tumeshuhudia alichofanyiwa LOWASA huko geita tena akiwa katika harakati za kampeni je ingekuwa hakuna uchaguzi?ninachosema haiwezekani usiwapitie wananchi kujua mahitaji na changamoto zao usubiri wakati wa kampeni hawawezi kukuelewa sasa vyama vya upinzani vinazuiwa kufanya hivyo ndio maana nimesema hakuna uwanja sawa wa kufanya siasa.
Nakubaliana nawe ndo nikasema. MAHAKAMA ipo wapeleke kesi na kutaka TAFSIRI.
Sijasikia wapinzani wakifanya hivyo.

Ni nani amepeleka KESI mahakamani ili apate tafsri?
Maana matamshi ya rais Si SHERIA bali ni EDICT tu.

Kwa mfano Trump leo hawezi kuwaambia chama cha DEMOKRATIKI, "Sitaki kusikia siasa zenu" HAIWEZEKANI. Maana lipo kwenye katiba.

Wanasiasa wetu ni lazima WAJUE HAKI zao badala ya kulalamika.
Mkuu nafikiri umenielewa
 
Mzee mwenye nywele nyeupe aliwashindisha juani watu pale jangwani kuanzia saa tatu asubuhi halafu saa kumi na moja anawaambia wakitaka kuzifahamu sera zake waende kwenye tovuti.

Kama suala ni kuzijua sera kupitia tovuti, kulikuwa na haja gani ya kuwashindisha juani watoto wa kimaskini wasio hata na uhakika wa mlo mmoja?.
Tunaongea habari iliyopo sasa,hatupo kwenye habari za uchaguzi wa 2015.
 
Nakubaliana nawe ndo nikasema. MAHAKAMA ipo wapeleke kesi na kutaka TAFSIRI.
Sijasikia wapinzani wakifanya hivyo.

Ni nani amepeleka KESI mahakamani ili apate tafsri?
Maana matamshi ya rais Si SHERIA bali ni EDICT tu.

Kwa mfano Trump leo hawezi kuwaambia chama cha DEMOKRATIKI, "Sitaki kusikia siasa zenu"
HAIWEZEKANI. Maana lipo kwenye katiba.

Wanasiasa wetu ni lazima WAJUE HAKI zao badala ya kulalamika.
Mkuu nafikiri umenielewa
mahakama nazo zina walakini
 
Rejea - reference. Huwezi kuwa na kesho yenye mafanikio pasipo mfano halisi wa maisha ya jana
Basi sawa,tuendelee kushinikiza mahakama ya mafisadi inakosaje kesi wakati TANESCO inadaiwa zaidi ya bil 300 na wahusika waliogawana wapo,MV dar es salaam haijawahi kufanya kazi na imenunuliwa zaidi ya bil 7....
 
Endelea kusoma vichwa vya habari kila unapokatiza mbele ya wauzaji wa magazeti.
 
Back
Top Bottom