Marufuku ya Magufuli kufanyia semina Mahotelini kwapunguza ufuska wa Maofisini

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
Semina za mahotelini zilikuwa zinachangia sana ufuska wa maofisini kati ya wafanyakazi.Semina zilikuwa jipu la watu kubebana mara ingine kwa ajili ya ufuska kwa kisingizio cha semina.
Semina hizo za mahotelini zilichangia pia kuongezeka nyumba ndogo za kike na kiume kwa gharama za serikali na pia kulichangia maongezeko ya ukimwi,watoto wa nje ya ndoa nk

Kupiga marufuku kumesaidia kupunguza ufuska wa maofisini kwa kuwa wengi hawako tayari kukodi vyumba kwa gharama zao kwenda kuufanya huo ufuska kwenye hoteli za gharama walikokuwa wanaweka hizo semina.

Chezea Magufuli

Hapa kazi tu
 
Heshima ya kazi imerudi! Saa 1.30 ofisi zimejaa! Na kila mtu anafanya kazi yake ipasavyo maana kila mtu anaogopa kutumbuliwa!
 
Heshima ya kazi imerudi! Saa 1.30 ofisi zimejaa! Na kila mtu anafanya kazi yake ipasavyo maana kila mtu anaogopa kutumbuliwa!

Aaaaaaaah, duh, Upo wakati mwaka 2015 mwanzoni nilienda ofisi moja ya halmashauri ya mji Fulani kwa shughuli ya kununua kiwanja kama ilivyokuwa imetangazwa na halmashauri hiyo...nilipofika (kwenye saa 3.30 hivi) niliambiwa mhusika ametoka kidogo amekwenda kunywa chai na kuambiwa nisubiri....nilisubiri kwa karibu saa 1 na dakika 43 baadaye akaingia dada mmoja mnene wa wastani na akakaa akaelekea kwenye meza niliyokuwa nimeelekezwa kuwa mwenyewe ametoka kidogo kwenda kunywa chai. Basi nikamwambia yule dada shida zangu lakini kabla ya hapo nilimwambia kuwa nimesubiri sana na kuambiwa alikwenda kunywa chai...majibu yake yalikuwa: Ni kweli kaka nilikwenda kunywa chai, afya kwanza hakuna cha ajabu. Wakati anasema maneno hayo alikuwa anakula apple. Duh, nikajisemea kimoyomoyo, ipo kazi...
 
Semina za mahotelini zilikuwa zinachangia sana ufuska wa maofisini kati ya wafanyakazi.Semina zilikuwa jipu la watu kubebana mara ingine kwa ajili ya ufuska kwa kisingizio cha semina.
Semina hizo za mahotelini zilichangia pia kuongezeka nyumba ndogo za kike na kiume kwa gharama za serikali na pia kulichangia maongezeko ya ukimwi,watoto wa nje ya ndoa nk

Kupiga marufuku kumesaidia kupunguza ufuska wa maofisini kwa kuwa wengi hawako tayari kukodi vyumba kwa gharama zao kwenda kuufanya huo ufuska kwenye hoteli za gharama walikokuwa wanaweka hizo semina.

Chezea Magufuli

Hapa kazi tu
Kila mtu sasa hivi asubuhi asubuhi huyo.
 
Back
Top Bottom