Tetesi: Marufuku ya kuzidisha abiria ili kupambana na Corona, Daladala zimeanza kugoma Dar es Salaam

Watu msiopanda daladala mnaonaga rahisi sana, gari ya kutoka tegeta to kkoo abiria wa kwanza kushuka ni moroco utapakia abiria gani tena kuanzia hapo?

Yaani hata kwa akili ya kawaida haiwezekani hata kidogo, mwendokasi ya serikali wenyewe wameshindwa pakia level seat

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni emergence kipind hiki ni cha muda, wavumilie.
 
hapo kwenye kupunguziwa bei ya mafuta ni ngumu sana kwasababu serikali haifanyi biashara ya mafuta na hata kama ingekuwa inauza mafuta hakuna namna ambayo ingeweza kupunguza bei ya hayo mafuta.
Tatizo letu Watanzania ni kutofuata sheria au maelekezo ya serikali hata kwa mambo muhimu kam kujikinga na maradhi ya COVID 19. Kenya waliweza kuzuia matatu kubeba abiria zaidi lakini sisi hapa umekuwa kama wimbo! Juzi nilisafiri kwenda Msho kutoka Arusah, coaster ilijaza abiria wakiwa wamekaa watano watano na wengine walisimama licha ya serikali kutoa maelekezo ya kutobeba abiria wengi zaidi
 
Kwanza sijui kwanini wamehangaika na wenye mabasi.......................... sijui daladala......................

Ni kuitangazia umma tuu ukikutwa umesimama kwenye daladala unapata fain ya Tsh 50elf. sasa uone nani atadhubutu kuingia kwenye gari iliyopo level seat. uamue kutoa 50 au kuchukua uber kabisa maana lazima sisi Watanzania tu learn in a hard way.

Na hapo tueone kama watalalamika sasa hivi abiria hawapandi. Na konda pia alimwe fain kwanini kazidisha abiria
Pa;e moshi kulikuwa na katazo la kutupa takataka ovyo, kwa jinsi watu walivyokuwa wanatozwa faini, ilibidi wajiongeze na Mji ukawa msafi. Kwa hiyo, hata daladal ziwekewe utaratibu huo, abiria akikutwa amesimama katika daladal apigwe faini na dereva pia apigwe faini. Hapo tutatii sheria bila shuruti
 
Haya ndo mawazo ya "kipumbavu" naomba mnisamehe kwa kutumia neno hili, kuna mtu ashawahi kuniambia sikumuelewa kwamba " utajiri huondoa utu,matajiri ni wachache Sana wenye roho za kujali binadamu,wao huwaza pesa tu"

Nilibishana nae sana lakini naanza kumuelewa, yaani nyie mnawaza kupiga PESA tu, what a shame!

Jumatatu nilipanda dala dala kondakta na dereva wake wakaleta mawazo ya kipumbavu kama haya na baadhi ya abiria nadhani siku hiyo hawatasahau hawa kondakta na dereva wake, walijaza gari then nikauliza kondakta hujapata taarifa ya serikali kuhusu Corona? Akanijibu toa umaskini wako ! Dah nilikasirika nikamuacha akawa amepandisha abiria nikamwambia sasa utajuta kwanini unatamani pesa kupitia majanga, nikawambia maabiria wote msiokaa kwenye siti jiandaeni kutoa faini koz mmekiuka utaratibu uliotolewa na serikali mmeshiriki na kondakta,hapo kwa mbele kulikuwa na trafiki walipiga kelele wanataka kushuka nilipata sapoti then nikawambia muache kujitia uchizi, waliomba kushuka wote then dereva nikamwambia lazima mtoe elimu na si vinginevyo wote kimya , nikamalizia hasira zangu kuwafoka with logical reasons na abiria nikawaambia tuacheni kujitoa ufahamu kama wewe umekata tamaa na maisha kakae huko ila siyo kuhatarisha maisha,

Ujinga kabisa!

Acheni kuwaza hela nyie watu, na serikali naishauri isichukue hata punje la ushauri huu ulioutoa, ndorobo wakubwa nyie, nchi inaingia kwenye hatari nyie mnawaza hela tu, stupid!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu,

Serikali imepiga marufuku daladala kusimamisha na kujaza abiria, taratibu ambao haukuzoeleka sana haswa kwa jiji la Dar.

Mimi nikiwa mmoja wa wamiliki wa daladala hizi naishauri Serikali mambo machache haswa katika kipindi hiki cha mpito kwakuwa Serikali imesema daladala itakayosimamisha abiria itapigwa faini laki Tisa au gerezani miaka miwili ifanye hivi ili kubalance situation.

Mfano daladala ikitoka mbezi hadi Temeke umbali wa kilomita 37 Kila abiria analipa 600 na daladala moja inasiti za abiria 26 hadi 22 akifika temeke anakuwa anapata 15600tsh hadi 13200tsh ambapo kwa umbali huo gari inaweza kutumia lita 5 ambapo ambapo ni sawa na tsh 11000.

Sasa Kama gari hadi inafika Temeke imekusanya 15600 za nauli ukitoa mafuta 11000tsh inamaana daladala hi itabakiwa na 4600.

Sasa kwa namna hii je huyo dereva atapataje hesabu na posho yake ya kila siku, bado kuna zile pesa za kupigia kiwi za jamaa zetu wale aliosema mkuu ambapo kwa siku nzima huenda zikafika 10000 tena hizi huwa hazinaga ubishi lazima utatoa tu.

Ushauri wangu, Serikali ipunguze bei za mafuta kwa daladala zote ikiwezekana iwe na vituo vyake vya mafuta na maduka yake maalumu ya vipuri pia Serikali itafute muda ikae na wadau husika lakini sio kufanya maamuzi bila kushirikiana na wadau watakaoteseka ni wananchi wakawaida wanategemea magari haya.
...Mbona unafanya ya Muwamba Ngoma Huvutia kwake??
Sema tu kweli utaeleweka.
Daladala za kawaida zote tunazojua za route ya Mbezi - Mbagala zote ni seat 30. Na sio wote wanaoanzia mbezi wanakwenda Mbagala.
Humu njiani kuna kushuku na kupanda kibao.
Seat moja inapofika Mbagala inakuwa imekaliwa hata na watu watatu!

WKati mwingine Serikali inapaswa kuwa kichwa maji tu na Kusema amri ni hii, anayetaka aendelee kufanya kazi kwa amri hii na asiyetaka akaweke gari lake Uwani afugie kuku!
Hawa hawa wanaotingisha kiberiti wataingia wenyewe barabarani!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...Mbona unafanya ya Muwamba Ngoma Huvutia kwake??
Sema tu kweli utaeleweka.
Daladala za kawaida zote tunazojua za route ya Mbezi - Mbagala zote ni seat 30. Na sio wote wanaoanzia mbezi wanakwenda Mbagala.
Humu njiani kuna kushuku na kupanda kibao.
Seat moja inapofika Mbagala inakuwa imekaliwa hata na watu watatu!

WKati mwingine Serikali inapaswa kuwa kichwa maji tu na Kusema amri ni hii, anayetaka aendelee kufanya kazi kwa amri hii na asiyetaka akaweke gari lake Uwani afugie kuku!
Hawa hawa wanaotingisha kiberiti wataingia wenyewe barabarani!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeongea bila kushirikiana na akili yako.hivi unajua madhara ya watu kutokwenda kazini kwa wiki moja.yaani umeandika upuuzi tupu huku jazba ya waziwazi imekujaaa.nyinyi ndio huwa mnakuwaga na maneno machafu kwenye daladala
 
hapo kwenye kupunguziwa bei ya mafuta ni ngumu sana kwasababu serikali haifanyi biashara ya mafuta na hata kama ingekuwa inauza mafuta hakuna namna ambayo ingeweza kupunguza bei ya hayo mafuta.
Namna ipo, kwa kuvipunguzia kodi vituo vya mafuta na kodi nyingi za vyombo vya usafiri kwa msimu huu na kupanga bei ya dharura,kama baadhi ya chi nyingi zilivyofanya kwa vitu vyote.Sisi tuzingatie kwanza usafiti kisha mengineyo.Wanashindwa mini,mbo8na misaada wanapata
 
Back
Top Bottom