Tetesi: Marufuku ya kuzidisha abiria ili kupambana na Corona, Daladala zimeanza kugoma Dar es Salaam

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,159
9,241
Wakuu,

Serikali imepiga marufuku daladala kusimamisha na kujaza abiria, taratibu ambao haukuzoeleka sana haswa kwa jiji la Dar.

Mimi nikiwa mmoja wa wamiliki wa daladala hizi naishauri Serikali mambo machache haswa katika kipindi hiki cha mpito kwakuwa Serikali imesema daladala itakayosimamisha abiria itapigwa faini laki Tisa au gerezani miaka miwili ifanye hivi ili kubalance situation.

Mfano daladala ikitoka mbezi hadi Temeke umbali wa kilomita 37 Kila abiria analipa 600 na daladala moja inasiti za abiria 26 hadi 22 akifika temeke anakuwa anapata 15600tsh hadi 13200tsh ambapo kwa umbali huo gari inaweza kutumia lita 5 ambapo ambapo ni sawa na tsh 11000.

Sasa Kama gari hadi inafika Temeke imekusanya 15600 za nauli ukitoa mafuta 11000tsh inamaana daladala hi itabakiwa na 4600.

Sasa kwa namna hii je huyo dereva atapataje hesabu na posho yake ya kila siku, bado kuna zile pesa za kupigia kiwi za jamaa zetu wale aliosema mkuu ambapo kwa siku nzima huenda zikafika 10000 tena hizi huwa hazinaga ubishi lazima utatoa tu.

Ushauri wangu, Serikali ipunguze bei za mafuta kwa daladala zote ikiwezekana iwe na vituo vyake vya mafuta na maduka yake maalumu ya vipuri pia Serikali itafute muda ikae na wadau husika lakini sio kufanya maamuzi bila kushirikiana na wadau watakaoteseka ni wananchi wakawaida wanategemea magari haya.
 
Sasa Kama daladala zikijaza bado raia wanapelea kusafiri hii SI italeta tatizo upya?,au ratiba zibadilike,daladala zianze kazi saa Tisa usiku mpaka saa Saba usiku na nauli ipande kidogo,maana level seat kea nauli ya Sasa,watu watapack magari tu
 
Kwa wakati huu mgumu nashauri polisi pia wapunguza za kubrashi iwe 2000 kwa siku nawewe tajiri punguza hesabu ya siku siyo kila siku mpunguziwe nyie tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo Ni sawa,mfano Venezuela iko karantini,rais w huko amefuta wananchi wanaopanga kulipa Kodi ya pango miezi mitatu na pia serikali inajitolea kulipa mishahara ya wafanyakazi wa makampuni madogo yaliyoathirika na karantini,
Nchi zingine serikali inalipa Kodi za kila mwezi za utilities Kama maji,umeme
 
Kwani aliyetengeneza hiyo daladala akaipa siti 22-26 hakujua? Acha tamaa katika kipindi hiki kigumu. Serikali inatafuta namna ya kupunguza maambukizi we unafikiria mambo ya mapato? Je hujasikia nchi zilizosimamisha kila kitu na watu wote wako quarantined?

Watanzania tuacha ujinga. We unadhani nyakati hizi serikali inapoteza mapato kiasi gani? We ndo unaona hutaki kupoteza? Kama vipi park gari ugonjwa ukiisha urudi barabarani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani ubaya wa hivi virus havifi haraka kwenye surface,tofauti na vile vya HIV Ni vinakufa ndani ya dakika tu.hivi mtu anatoka kamasi akijifuta,vinabaki mkononi,akishika bomba la daladala,anaviachapo na kila atakaeshika Hapo atavibeba mkononi na akigusa mdomo ama pua tu,imo
 
Back
Top Bottom