Marufuku ya kuuza nafaka nje ya nchi: Wakulima wanatendewa haki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marufuku ya kuuza nafaka nje ya nchi: Wakulima wanatendewa haki?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by JamboJema, Jul 4, 2011.

 1. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Ijumaa ya Tarehe Mosi mwezi huu wa Julai nilikwenda mpaka wa Tanzania na Uganda eneo la Mtukula. Nikiwa naelekea huko pale maeneo ya Kyaka, kama kilomita 35 hivi toka Mtukula niliyaona maroli mengi yakiwa yamesheheni nafaka mbalimbali yakiwa yamepaki hapo Kyaka.

  Nilipouliza kulikoni nikaambiwa magari hayo yalikuwa yakipeleka mazao hayo Uganda lakini mamlaka za Tanzania zimezuia kufanya hivo kwa maelekezo kutoka serikalini kwamba chakula hakiruhusiwi kutoka nje ya nchi kwani kuna njaa nchini.


  Ninachoshindwa kuelewa ni kwa nini wakulima wabanwe namna hiyo katika kutumia kilicho chao kihalali? Mbona mfanyakazi hapangiwi aufanyie nini mshahara wake?

  Kwa nini mkulima asiachwe kuuza mazao yake kule anakoona kuwa atapata profit na kurudisha gharama zake za kilimo?
  Ninavyodhani ni bora, iwapo say, Uganda bei ni kubwa na serikali inania ya dhati kuzuia njaa nchini, basi ichangie gharama ya hicho chakula ili mkulima alipwe sawa na kama angeuza Uganda, na si kumzuia.

  Nawasilisha
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Wana mamlaka gani ya kuzuia kuuza nje? Kama mkulima anapata bei nzuri nje kuliko soko la ndani kwa nini asiuze nje? Ni jasho lake kama vile ambavyo wenye nyumba wanavyoamua kupangisha kwa Dola badala ya shillingi na kufanya zikalike na tabaka fulani tu, mbona hao hawashukiwi na serikali? Badala yake serikali inamkimbilia mkulima mlalahoi.
   
 3. n

  nrango Senior Member

  #3
  Jul 4, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wauze nje wakuze pato lao,serikali inanunua mazao bei ndogo sana.
   
 4. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  I think you are right, Ngambo Ngali!
   
 5. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  kibaigwa soko la mahindi sh 25 000 gunia,mkulima akiuza uganda au kenya sh 70 000 kwa gunia.serikali haitaki mkulima apate faida bali hasara.wakati anatayarisha shamba,kulima,mbegu mbolea kupalilia kulinda kuvuna govt haikuwepo imekuja wakati wa mauzo tuu na kumpangia wapi auze na kwa bei gani.si haki hata kidogo
   
 6. F

  FUSO JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,856
  Likes Received: 2,333
  Trophy Points: 280
  kama tulizoea mahindi muda huu wa mavuno June to Sept kuwa chini kilo huuzwa kati ya Tsh 250 - 300. Sasa hivi kilo moja ni Tshs 490 bei ya jumla.

  Mahindi yanaenda Kenya kwa wingi sana Kama mkulima tukimruhusu auze anapotaka basi na sisi tusilalamike kununua sembe kwa Tshs 1200. kumbukeni mipanga imeshafunguliwa - Kenya, Uganda, Rwanda na Tz, Ushirikiana umeshaanza rasmi.

  Mi naona tumruhusu mkulima atafute soko la ndani ili kuokoa baa la njaa, tusije nunua kilo ya sembe tshs 3000.
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Wanaharakati wajitokeze kutetea hawa wakulima, na mali zao. Wanaonewa sana.

  Ibara ya 23 (1) ya Katiba inasema:
  Kila mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa aina yoyote, anayo haki ya kupata ujira unaolingana na kazi yake, na watu wote
  wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao watapata malipo kulingana na kiasi na sifa za kazi wanayoifanya.

  Katiba haisemi huo ujira inabidi upatikane hapa nchini au nje kwa hiyo kama mkulima anaona jasho lake linalipika vizuri zaidi Uganda wacha apeleke asikatazwe asilani.
   
 8. MAVUNO

  MAVUNO JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2011
  Joined: May 29, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  what is international trade? and what for?
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  serikali onevu sana hii haina msaada kwa mkulima hata kidogo. bei ya mazao ya mkulima ni ndogo saaana mkulima anapunjwa anaingia gharama kubwa sana lkn mwisho wake ni huo wa kuzuiwa kuuza nje kwenye bei nzuri. mkulima atabaki maskini miaka yoote chini ya serikali hii ya CCM.
   
 10. papason

  papason JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Huu ujanja ujanja wa kuzuia mahindi, mpunga, mtama, dagaa, sato,matembele, nsansa, maharage,kunde n.k visiunzwe nje ya nchi ni namna ya tuu ya hii serikari dhaifu kabisaa ya CCMm kulinda kundi kubwa la wavivu na wajanja ili wapate chakula kwa bei ya kutupa isiyo reflect gharama halisi za uzalishaji, yaani mambo mengine yanatia hasiraa kweli kweli

  Nafikiri inaeleweke wazi kuwa asilimia 80% ya watanzania ni wakulima tunaoishi huku vijijini na hatuna mtu yoyote anayetutete,a yaani tumeachwa kama mayatima hakuna anayetujali, haiwezekani wajanja waendelea kununua mazao yetu kwa bei ile ile ya 1970s wakati ndani ya miaka mitano karibu kila kitu kimepanda kwa zaidi ya asilimia 60% ( mbolea, diesel, sukari, chumvi, nauli) ukweli ni kuwa mkulima wa Tanzania ndiye anayenyonywa kuliko kiumbe mwingine yeyote yaani katika lugha lahisi mazao yetu yanaporwa kiulaini kabisaa!! wakati ata sisi wakulima tuna watoto wetu wanaotakiwa kwenda shule, tena bado tunaishi maisha duni kabisaa

  Binafsi ningependa nione serikali inayothamini wakulima wake inayowatafutia masoko ya bidhaa zake nje ya nchii, na sio inayotuambia wakulima watanzania limeni na soko lenu ni ndani ya mipaka ya nchi hii… huu kama sio utumwa ni nini? IPO SKU KITAELEWEKA TUU..

  Kwa kuanzia serikari ingeacha nafaka na bidhaa zingine za wakulima kuuzwa nje nchi.. Ndioo iwaache wafanya biashara wapigane vikumbo kwa wakulima then automatically bei ya vyakula itapanda hivyo kuchochea mabenki na wenye mitaji mikubwa kufanya investment kwenye sekta ya kilimo BADALA YA KUPIGA ILE TUNE MBAYA KABISAA YA KILIMO KWANZA
   
 11. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nchi yetu bwana uwa inafusahisha sana viongozi wetu wanasema 70% ya Watanzania ni Wakulima, halafu mahindi hamna, ulaya yenyewe wakulima hawazidi 20% hamna njaa
   
 12. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  I like the conclusion, it reflects the reality
   
 13. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Mkulima wa kizungu aliyelima Tanzania akipata tani zake 1,000 na kuamua kupakia mazao yake kwenye container na kusafirisha kupitia bandari za Tanga au Dar Es Salaam kwenda South Africa au hata Zimbabwe, hiyo ni sawa kabisa, ila mbantu na vigunia vyake mia akipakia kwenye Fuso na kupeleka mpakani Tanzania na Uganda ni Kosa la Jinai.

  Kweli hii ni Kilimo Kwanza, unategemea mbantu anunue trekta kwa bei mbuzi anayopewa hapa tanzania, trekta lenyewe la Kihindi na linauzwa na wanajeshi pale mwenge mwanajeshi ambaye hajui kilimo wala nini.

  Acha tucheze ngoma na kukata viuono kusherehekea miaka 50.

  Huu ndio uhuru
   
 14. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  baada ya serikali kushindwa kununua mahindi yaliyokuwa nje na baada ya kunyeshewa na nvua serikali imeondoa marufuku hiyo na sasa mahindi ( hata yaliyoharibika) yanaweza kuuzwa nje pamoja na kunyeshewa mvua.
   
 15. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Observation yako ni sahihi kabisa.Infact hatua hii inafanya wakulima wetu wazidi kuwa maskini.Nani asiyejua kwamba soko la ndani ni dogo kwa hiyo prices are bound to be low kama tutasema tuuziana wenyewe?Sasa mkulima atarudije shamba? Mimi ina nishangaza sana.Mchango wa serikali katika production process ni mdogo sana.Why they should poke their noses at marketing only is difficult to tell.Watu hawa wamesoma shule tulizosoma sisi,wengine hata tumesoma pamoja,lakini wengi wameacha taaluma zao na mambo wanayofanya ni kinyume kabisa.Sijui ni kitu gani kimewasibu.Inasikitisha sana.
   
Loading...