Marufuku ya Bweni Shule za Msingi, Serikali imekurupuka

Kumpeleka mtoto mdogo boarding ni sawa na kumtelekeza mtoto wako mataa,zinduka hata Kama una majukumu kiasi gani jitahidi kutenga muda kulea mwanao mwenyewe
 
Hilo la watoto kusoma wikiendi nahisi ni msimamo wa mzazi tu. Binafsi hakuna mwanangu anayesoma wikiendi. Yawe maamuzi ya shule au ya kwake mwenyewe. Haendi na shule zinajua hilo.
Changamoto Bado inakuwepo sababu mtoto wa mwingine atakuja kuathiri jamii. Labda atakuja kuwa mkwe wangu ambaye amekosa malezi ya wazazi
 
Elimu ni biashara ebu tafuta msomi aliyesoma Kama utakuata mtoto wake yupo uko boarding, tunaohangaika na boarding ni sisi ambao elimu tulikkosa gafla mungu katupa vimia mbili Mia tatu basi tunajikuta tunalipa pesa nyingi kwa sifa na somesha na mnanyonywa balaa

Unatapesa unataka mwanao aongee kingereza mbona walimu wapo mtaani wengi tu tafuta mwalimu aje home afundishe watoto kingereza maana kingereza Cha shule watoto wanasoma darasani no vigumu mtoto kuongea kingereza ila akija mwalimu nyumbania akampa misingi ya kingereza akikijua hicho basi uko shule Napo atajua tu
 
Serikali imepiga marufuku kwa shule zinazotoa huduma yela bweni kusitisha kwa watoto wa shule za swali mpaka darasa la nne. Shule zemeelekezwa kufanya hivyo baada ya kumalizika muhula wa kwanza mwaka huu.

Ukiangakia ni kwamba huu ni uamuzi ambao umekee sikiasa na kihisia zaidi. Moja kati ya sababu zilizotokewa ni maadili mabaya na kukosa upendo baina ya watoto na wazazi.
Binafsi Kuna sehem nakubaliana na pengine sikubaliani. Nakubali kuwa kwa Shule za Awali sio sahihi mtoto kuwa mbali na wazazi. Na hiki ndio kipindi kizuri kujenga hayo malezi na upendo Kwa mtoto.

Katika mfumo wa maisha ya Sasa kuna mazingira ambayo unaona mtoto kuwa bweni ni salama zaidi kuliko mtaani. Hapa nitaweka sababu chache.

1. Mfumo wa utafutaji riziki
Wazazi wengi Kwa Sasa tunatumia muda mwingi tukiwa mbali na Nyumbani na wengi hulazimika kurudi Nyumbani usiku.

Wengi huchelewa katika harakati za usafiri, umbali wa maeneo ya kazi au kazi zenyewe zinhitaji kuzifanya mpaka usiku. Serikali iache kuamua kwa kufikiria kuwa wote wanao somesha shule za bweni ni watumishi wa umma. Tupo sisi bodaboda ambao tinajibana kusomeaha watoto shule nzuri.

2. Matatizo ya ndoa
Serikali ilipaswa kufanya utafiti kidogo tu kutoka kwen6 data zake juu ya ndoa zinazo vunjika na hatma ya watoto kimalezi. Watoto wengi wa watalaka hupelekwa Bweni kama kimbilio salama ambapo wazazi wote Huwa na Imani zaidi. Baada ya talaka Kila mzazi Huwa na maisha tofauti kiutafutaji hata mahusiano na kukosa ukaribu na mtoto wa mtalaka.

Kuna visa vingi vya watoto kuuwawa au kufanyiwa ukatili na mama au baba wa kambo. Ni rahisi wazazi kukubaliana mtoto aende bweni ambalo wanaamini anakua sehem salama kimalezi na kielimu.

3. Teknolojia
Mtoto kuwa mtaani inamuweka karibu zaidi na maudhui mabaya yakiyopo kwenye mitandao. Tafiti zinaonesha kuwa zaidi ya 80% ya maudhui katika mitandao ya kijamii ni maudhui ya Ngomo.

Ukizingatia hayo utaona mtoto kuwa mtaani inamuweka karibu na maovu ya mtandaoni. Huko bweni ni rahisi kufanya usimamizi wa pamoja kuliko huku mtaani. Selikali haiwezi kuzuwia.

Mitandaoni utakuta Mashoga, Wasagaji, Makungwi na namna nyingi ya maovu yakiwa yameanikwa bila udhibiti, na serikali haiwezi wala haikemei ili kudhibiti.

Tamthilia kutoka nje
Hizi ni tamthilia toka nje ambazo huoneshwa kwa kutafsiriwa kwa Kiswahili. Utakuta kila nyumba watoto wanakesha usiku wakifiatilia hizi filamu ambazo nyingi zinachukua wasatani wa miezi mitatu. Watoto wanakesha wakifiatilia hizi filamu ambazo nazo unakuta maudhui ni Ngomo na Ushoga.

Hizo ni sababu chache tu ambazo hupelekea wazazi kuamua kupeleka mtoto bweni ili angalau kumkinga na kadhia ya mtaani.

Wizara ya Elimu iache mihemko na kuiga Wakenya. Serikali ifanye utafiti na kushirikisha wadau kabla ya kufanya maamuzi ambayo yanawagusa watu. Hakuna mzazi angependa kulipa gharama kubwa kusomesha mtoto endapo serikali ingetimiza wajibu wake wa kuboresha shule za umma na kudhibiti maadili ya mitandaoni.

Maoni yangu
Shule kuanzia darasa la kwanza waruhusiwe kuwa Bweni au Wazazi wapewe fomu maalum wajaze ili kujua sababu ya kumpeleka mtoto bweni.

Tunamrudhisha mtoto mtaani aje kujifunza nini?
Kama ww ulivyokurupuka kuandika uzi bila kuangalia athari za mapana kwa taifa ,malezi na familia
 
Back
Top Bottom