Marufuku watoto sehemu za starehe wala kuuziwa sigara

Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
186
212
Karibu sana mpenzi msomaji na mdau wa JamiiForums katika Somo la leo ambako tunakwenda kujifunza kuhusiana na ulinzi wa mtoto (Child Protection) hasa katika mazingira hatarishi kwa ustawi bora wa mtoto.

Leo tunaangazia zaidi kifungu cha 17(1, 2, & 3) cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 sura ya 13 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Kisheria mtoto haruhusiwi kuingia katika ukumbi wa muziki, baa au klabu ya usiku. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 17(1) cha Sheria ya Mtoto.

Hivyo mmiliki, msimamizi au mtu anayeendesha sehemu hizo za starehe anatakiwa kumzuia mtoto kuingia maeneo hayo kama sheria inavyoelekeza.

Sheria pia inakataza mtu yoyote kumuuzia mtoto sigara, pombe, madawa ya kulevya au kitu chochote kinacholewesha. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 17 (2) cha Sheria ya Mtoto.

Hivyo, ni kosa kisheria kumuuzia mtoto sigara, pombe au kitu chochote kinacholewesha.

Ndio maana hata katika matangazo ya kibiashara yanayohusu sigara au pombe huwa wanatoa angalizo kwamba "Hairuhisiwi kuuzwa kwa watoto chini ya miaka 18" au kwa lugha nyingine wanasema "Not to be sold to the people under the age of 18."

Mtu anayetenda kinyume na kifungu hiki cha 17(1&2) cha Sheria hii ya Mtoto atakuwa ametenda kosa na atakapotiwa hatiani adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi milioni moja za kitanzania (1 mil.) na kisichozidi shilingi milioni tano za kitanzania (5mil.) au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichozidi miezi 12 au faini na kifungo vyote kwa pamoja kwa mujibu wa kifungu cha 17(3) cha Sheria ya Mtoto.

SASA TUJIULIZE

(a) Malangapi tunashuhudia katika jamii zetu watoto wakionekana katika sehemu za starehe nyakati za usiku?

(b) Malangapi tunaona watoto wakiuziwa sigara, pombe au madawa ya kulevya?

Jibu ni kwamba
Hii inatokea malanyingi sana. Watoto wanaonekana sana wakiwa kwenye kumbi za starehe nyakati za usiku aidha wakiwa peke yao au na wazazi wao.

Lakini pia huwa tunaona watoto wakiuziwa sigara, pombe na mala nyingine hata madawa ya kulevya.

Mbaya zaidi katika yote haya wazazi na jamii kwa ujumla tumekuwa kimya na kuchukulia haya katika hali ya kawaida. Hakuna jitihada zozote zinazofanyika ili kuwalinda na kuhakikisha ustawi bora kwa watoto wetu.

Mambo haya kwa mujibu wa sheria hayaruhusiwi hata kidogo katika swala zima la kulinda maadili na usalama wa mtoto.

Mchango wako ni upi katika kuhakikisha ustawi bora na usalama wa mtoto katika jamii yako?

🇹🇿Tanzania na watoto wenye maadili na ustawi bora inawezekana. Jukumu hili ni langu, ni lako, ni la yule.

It's me
Mr George Francis
A Lawyer and LifeCoach
Contacts: 0713736006
Email: . mr.georgefrancis21@gmail.com

Join us on telegram: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓
706666659.jpg
 
Watoto?
Sehemu za starehe??
Nyakati za usiku??
Sijawahi kuona, labda huwa nimelewa sana!

Hii nchi ni kama hakuna sehemu ya mtoko iliyo friendly kwa watoto. Kama hawauzi fegi, ganja na beer, wanapiga nyimbo zinazowazidi umri. La sivyo, utakuta wanashindanishwa kukata viuno au wanaskiza vijana wanabishania mpira kwa lugha zisizo na staha!
Pamoja na hayo, jamii yetu haina content ya kutosha kwa ajili ya watoto katika mifumo ya kidijitali inayiendana na lifestyle ya watu wengi, hasa wa mijini!
 
Watoto?
Sehemu za starehe??
Nyakati za usiku??
Sijawahi kuona, labda huwa nimelewa sana!

Hii nchi ni kama hakuna sehemu ya mtoko iliyo friendly kwa watoto. Kama hawauzi fegi, ganja na beer, wanapiga nyimbo zinazowazidi umri. La sivyo, utakuta wanashindanishwa kukata viuno au wanaskiza vijana wanabishania mpira kwa lugha zisizo na staha!
Pamoja na hayo, jamii yetu haina content ya kutosha kwa ajili ya watoto katika mifumo ya kidijitali inayiendana na lifestyle ya watu wengi, hasa wa mijini!

Kwa Hiyo ni halali wao kwenda bar

Kuna siku Nilikuwa masai Kama saa tano naona baba na mama sijui wale wamekuja na katoto kamepewa tablet wenyewe wanapiga vyombo

Na siku hizi imekuwa kawaida Mbaba anabeba mwanae anaenda nae Kwa washkaji bar
 
Kwa Hiyo ni halali wao kwenda bar

Kuna siku Nilikuwa masai Kama saa tano naona baba na mama sijui wale wamekuja na katoto kamepewa tablet wenyewe wanapiga vyombo

Na siku hizi imekuwa kawaida Mbaba anabeba mwanae anaenda nae Kwa washkaji bar
Si sahihi kwenda na watoto bar, hasa nyakati za usiku.
Mi nachosema ni kwamba in case una kamtoko ka kwenda lunch au hata dinner mbali na nyumbani inakuwa changamoto sana kupata sehemu ambayo ni rafiki kwa watoto.
Labda uende hotels kubwa. Resraurants wanauza pombe na kucheza nyimbo za kutia aibu.
 
Ndo maana jaji Rumanyika alimfunga lulu wasiojuwa sheria wakawa wanaongea ujinga ati ni mtoto.

Tafisiri ya Ile hukumu inasema mtoto akifanya mambo ya wakubwa atahukumiwa kikubwa Mtoto gani hakosi bar? Mtoto gani anaingia mahusiano na wakubwa? Picha zake mitandaoni sasa ahaaa jaji ikabidi kwanza amfundishe adabu kuwa alistahili kuishi kama mtoto na sio kufanya mambo ya wakubwa kwenye makosa analia ati yeye ni mtoto.
 
Back
Top Bottom