[Marufuku mifuko ya plastiki] Tunaouza Maji ya Kandoro tutafungia wapi?

Wakati wa Nyerere mifuko ya rambo haikuwepo na ilikuwa marufuku, saruji ilikuwa kwenye mifuko ya karatasi, mahindi mchele sukari vilikuwa kwenye magunia.

Kaja sijui prof sijui dr kashauri biashara huria wakati huo ndio sinema ya rambo ndo iko kwenye chati ndo maana ikaitwa mifuko ya rambo.

Tulipiga kelele tukasema hizi rambo zitaua mashamba ya mkonge na kiwanda chetu cha mgololo tulichokijenga kwa gharama kubwa, tukaambiwa tuna wivu wa kike.

Tusiishie kwenye rambo tu hadi sandarusi zipigwe marufuku. Mbona cement ya pakistan inafungashwa kwenye mifuko ya karatasi na inapanda melini?

Sukari nayo ifungashwe kwenye ''indian cloth'' kama wakati wa nyerere.
 
Maji ya kilimanjaro soda za kwenye plastic nazo zipigwe marufuku tu, watumie chupa za glass au mabox kama ya azam fruit au vijot,

tukitumia chupa za glass kiwanda chetu cha chupa cha mikocheni kitafufuka na kile cha mwanza glass tutakimalizia kwani tutakuwa na soko la uhakika la chupa zetu
 
Back
Top Bottom