Marufuku kuwakarimu wakaguzi hesabu - CAG

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,955
22,133
Marufuku kuwakarimu wakaguzi hesabu - CAG



na Deogratius Temba




MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amewataka wananchi kutowakarimu kwa namna yoyote wakaguzi wa hesabu za serikali wanapofika katika maeneo yao hasa ya vijijini kukagua hesabu.

Akizungumza katika kipindi cha ‘Tuambie’ kinachorushwa na Televisheni ya TBC1, Utouh alisema wananchi hawaruhusiwi kuwakarimu malazi, chakula wala kitu kingine chochote wakaguzi kwani ofisi yake inawagharamia mahitaji yote muhimu kwa kiasi cha kuwatosha.

“Ninatangaza tena na wananchi wote wanisikilize, hawa wakaguzi hawana ruhusu ya kupokea kitu chochote kutoka kwa wale wanaowakagua au wananchi, ninawapa mahitaji yao yote ya msingi na hawatakiwi kupewa fedha na mtu mwingine,” alisema Utouh.

Alisema atafuatilia kwa siri na akibaini kama kuna wakaguzi wanaofanya hivyo atawashughulikia kwani ni kinyume cha sheria za maadili ya ukaguzi.

Akizungumzia suala la kukithiri kwa uchafu katika miji mingi nchini, alisema kuna wasiwasi kuwa baadhi ya zabuni za kufanya usafi au kukusanya taka chafu mjini hazizingatii vigezo stahiki.

Alisema zabuni hizo ni tatizo, kwani vikundi vingi au makandarasi wanaopewa hawana uwezo wa kufanya kazi hizo.
 
Dah sasa kumbe walikuwa wanakirimiwa hii kali inawezekana wakawa wanacheza hapa na pale sio
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom