Marufuku kuvaa Suruali na Sketi za KUbana!!

sijui Mtwara, Mwenge, Morogoro, Tabora, Bukoba, et al (SAUT colleges zote) sijui wameshaanza hii kitu pia??

nadhani na MUM, TUMAINI, ST JOHNS, TEKU NA vingine mbalimbali hususani vya mashirika ya dini vifanye hivyo!!
 
Uongozi wa Chuo Kikuu cha RUCO cha Mjini Iringa kimepiga marufuku wanafunzi wake wa kike kuvaa suruali na Sketi za kubana, badala yake wanafunzi wa kike wametakiwa kuvaa magauni marefu au Sketi zinazovuka magoti na zisizobana!!

Chuo hicho kinamilikiwa na Kanisa Katoliki Tanzania.

aise...hii ni noma...wakuu hebu tupeni update km hii kiti ilifanikiwa pale SAUT
 
sijui Mtwara, Mwenge, Morogoro, Tabora, Bukoba, et al (SAUT colleges zote) sijui wameshaanza hii kitu pia??

nadhani na MUM, TUMAINI, ST JOHNS, TEKU NA vingine mbalimbali hususani vya mashirika ya dini vifanye hivyo!!

Unajua sheria za MUM wewe...
1.Pale wanawake wa dini zote lazma uvae HIJAB/BAIBUI LA KUKUHIFADHI MAUNGO YA MDADA
2. MARUFUKU HATA KUSOGELEA BWENI LA WANACHUO USIOFANANA JINSIA / UNATIMULIWA KAVKAV
3. WAKIKUKUTA KWA USHAHIDI KWAMBA UNAMAHUSIANO YA LINGONO NA MTU ASIE MKEO/MMEO HAINA MJADALA DISCOOO
4. Cheating ya aina yeyote hata kwenye kajitest ileee discooo
5. Kidume ukivaa Kata ''k'' hoooome
6. Ukizipiga au kutukana ukapatikana ushahidi.... Huna chuo
7. Ukikutwa umelewa ama wanywa pombe,. Kuvuta sigareti na ndumu haina mjadala wanakutimua on the spot
Kwa uchaaache this iz all about ''MUM'' muslim university of morogoro/chuo kikuu cha waislamu morogoro
 
dress code ni muhimu kuzingatiwa katika kila jamii. Uelimishaji wa kuendelea kuzingatia maadili ya mavazi ni lazima uendelee kuanzia ngazi ya familia. Naamini haki za kila mtu na utu wake utaheshimiwa. Nachelea tusifikie enzi zile za Tanu Youth League au vijana wa Musarika kule Malawi kuwachania nguo wale ambao wanaonekana wamevaa "kivazi" kinachoonekana si cha kimaadili. Tukizingatia kwamba "UHURU WA MWENZAKO UNAANZIA PALE UHURU WAKO UNAPOISHIA"
 
ngoja tuone.manake kuna watetezi wa haki zisizo haki na uhuru binafsi...
Mimi nadhani hata mademu wenyewe wengi wao siku hizi hawapendi wenzao wanaovaa suruali zile zinazobana sana, kwani wakati mwingine zinawaweka wazi sana hasa wakati wa kushuka na kupanda kwenye magari. Chachandu zote huwa nje pamoja na zile G string zao wanazopenda kuzivaa11
 
Back
Top Bottom