#COVID19 Marufuku hospitali za umma, binafsi kulipisha chanjo ya COVID-19

Kila mtu na hiari yake, anaeona chanjo haifai asicomment tafazali, atulie kimyaa kama hajaiona mada.
Yaani wewe ucomment na wenzio wasicomment? Hicho kitu hakipo!! Usiogope mawazo mbadala! Hakuna anayelazimishwa kuchukuwa mawazo mbadala!! Na wewe weka mawazo yako na watu wasilazimishwe mawazo yako pia!! Vinginevyo anayeona chanjo inafaa asicomment na anayeona chanjo haifai asicomment!! La sivyo wote wacomment!! Amini kuwa kama hoja zako ni nzuri kuhusu chanjo watu wataziamini na hoja zingine watazikataa. Au hauziamini hoja zako kuwa zitashawishi watu wachanjwe? Unaona hoja zako zimezidiwa nguvu?
 
Nafsi zetu zinatusuta kutotimiza wajibu wetu kwa jamii kutokuwafahamisha tulicho na uelewa nacho, kodi za wanyonge wa kitanzania ndo zimetusomesha tukawa na maarifa tuliyo nayo sasa.

Kwa hiyo tunachofanya ni kurudisha fadhila kwa jamii ya watanzania wenzetu, wewe kama una maslahi binafsi kwenye hizi chanjo za majaribio huna uhalali huo wa kunifunga mdomo nisiwaelimishe watanzania wanyonge wenzangu ambao wanahitaji kupata taarifa sahihi zisizo na kificho au kuegemea maslahi yoyote.
Eti kuwaelimisha wanyonge wanzako!!mimi mkulima niwe na maslahi gani , ila watu watachanjwa tena kwa hiari yao tuone sasa!!meko ameshaondoka na dhana zake potofu!!na wote walokuwa naye walishamkimbia na kwenda kwenye ukweli
 
Kwani madaktari na manesi si wapo siku zote? Au sijaelewa point yako mkuu nieleweshe
Yes. Kwa mfano kama ni hospitali za binafsi ukienda hupati huduma bure(hizo za siku zote).

Sasa hospitali hiyo ikipata watu 100 kwa siku wa chanjo ambao inatakiwa/inalazimika iwahudumie "bure" unadhani itakuwaje? Unless kama wamemaanisha "dawa" (chanjo) ni bure but hospitali zinaweza kuchaji service fee kwa kutoa hiyo huduma ya kuchanja.
 
wagonjwa wa,
1.KISUKARI
2.PRESHA
3.MOYO
4.SARATANI
5.UKIMWI
wagonjwa wa maradhi hayo wanapaswa wachue tahadhari sana maana Corona itatumaliza sana.
 
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa angalizo kwa wasimamizi wa chanjo kutolipisha watu fedha kwani chanjo hizo ni bure.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi wakati wa usambazaji wa chanjo hizo kwenda mikoa mbalimbali nchini tukio lililofanyika bohari kuu ya dawa MSD, Kurasini Dar es salaam.

Akitoa rai kwa wasimamizi, Prof. Makubi, amesema utoaji wa chanjo hizo kwenye hospitali za Umma na binafsi utatolewa bila kulipisha gharama za chanjo.

"Naelekeza kwa huu mgao wa Covax Facility ni marufuku Hospitali za umma au binafsi kulipisha Wananchi gharama yoyote katika zoezi hili la chanjo na lifanyike kwa uadilifu na kwa haki kwa walengwa wa sasa." amesema Prof. Makubi.

Ameongeza kuwa, pamoja na serikali kufanikisha upatikanaji wa chanjo hizo na kuanza kuchanja Wananchi, Wizara ya afya inaendelea kuwashauri wananchi kujikinga na UVIKO-19.

"Kwa kuzingatia kanuni za UVIKO-19, tunapaswa kunawa mikono, kuvaa barakoa, kukaa umbali za mita moja au zaidi, kuepuka misongamano na kufanya mazoezi.

Aidha, amesema ugawaji wa chanjo umezingatia taarifa ya visa vya wagonjwa waliohisiwa kuwa na UVIKO-19, idadi ya walengwa kwa kundi la kipaumbele pamoja na idadi ya chanjo zilizopatikana kwa sasa.

Katika hatua nyingine serikali kupitia TMDA, Maabara ya Mkemia Mkuu, Maabara kuu ya Taifa na Vyombo vingine vyote vimehakiki na kujiridhisha usalama na ubora wa chanjo za Janssen kutoka Kampuni ya Johnson & Johnson nchini Marekani.

Prof. Makubi amebainisha kuwa, kutokana na Mwongozo wa Chanjo wa Taifa dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO-19, Shirika la Afya Duniani (WHO), maelekezo ya Covax Facility na upungufu wa uzalishaji wa chanjo toka viwandani, Chanjo hizo kwa sasa zinatolewa kwa kufuata vipaumbele vya makundi yenye uhitaji mkubwa.

"Makundi ambayo yataanza chanjo ni pamoja na: Watumishi wa sekta ya Afya, Watu wazima umri wa miaka 50 na kuendelea na Watu wenye magonjwa. Kama ambavyo Serikali imekuwa ikieleza, uchanjaji kwa makundi yote nchini ni wa hiari au huru kwa kila mwananchi.

Kwa kuwa chanjo zilizopokelewa kwa sasa hazitoshelezi walengwa wa makundi yote nchini, makundi mengine yatapata chanjo katika awamu inayofuata, mara zitakapowasili." amesema Prof. Makubi.

Hadi sasa Serikali inategemea kutoa chanjo kwa makundi yanayolengwa kuanzia Agosti 3,2021, siku ya Jumanne, katika vituo 550 vya kutolea huduma katika mikoa yote ya Tanzania bara ambapo Orodha ya vituo hivyo inapatikana pia katika tovuti ya wizara; www.moh.go.tz.

Wananchi wote walengwa, wanaotaka kuchanjwa kwa hiari yao, huku wakitakiwa; kujihakiki kama wapo ndani ya makundi matatu ya walengwa kwa sasa.

Ippmedia
Chanjo ya NINI BADALA WAZUIE
AJALI ZA BARABARANI WATU WANA KUFA UAMEKOMAA NA korona , wakati korona yenyewe haipo hivi akili za watu wengine ziko vipi huo ujinga wako usiweke tena

Hiyo korona inatusaidia nini siye
 
Back
Top Bottom