Marufuku. Bodaboda Kupaki au kuonekana kwenye Taasisi za Fedha

Mwana Ilala

JF-Expert Member
Jan 29, 2013
1,287
486
Jeshi la Polisi limetoa Rai hiyo kwa vyombo vyote Vya Bodaboda kutokuonekana kwenye Maeneo ya Taasisi za Fedha.

Je!? Rai hii Itapunguza vitendo Vya kiuhalifu vinavyosababishwa na hawa Wahalifu wanaotumia Usafiri wa Bodaboda kutekeleza vitendo vyao Vya Uhalifu!?

ImageUploadedByJamiiForums1457103047.212326.jpg

ImageUploadedByJamiiForums1457103117.645994.jpg
 
Utakupumbuka hata Land Cruisers mkonga zilizuiwa kuingia Bank kwa kuhofia uwezo wa kasi ya kusema miaka ya 80 - 90s,lakini leo yako wapi,zinaingia kama kawaida.

Haisaidii kitu kabisaaa,ila kuingia katikati ya Mji hasa kwenye Majiji aisee ni Kero saana,Mie mwenyewe namiliki bodaboda kadhaa ila aisee kuingia katikati ya jiji hivi vidude vinakera sana
 
Kama itapunguza au la huwezi kuwa na uhakika ila jambo la uhakika ni kuwa, kutumia hizi boda kwa ujambazi wa mabenki unarahisishia majambazi kwasababu ni usafiri potable zaidi na unarahisisha kupenya sehemu korofi kama vichochoro na misongamano ya magari, pia ni rahisi hata kwa wahalifu kujichanganya na watu maana unaweza itelekeza tu hiyo pikipiki ukapotea zako.....kwa maantiki hiyo nadhani ni sahihi kupiga marufuku hii kwani inawarahisishia zaidi majambazi zoezi la uporaji
 
Mimi naona ni wazo zuri sana.

Iwapo itaonekana hata Bodaboda moja labda imemfuata mtu au kumshusha mtu itakuwa rahisi sana kusaidia upelelezi, iwapo la kutokea litakapotokea
 
Nadhani hiyo ni njia rahisi ya polisi kutokutumia kichwa kuzuia uhalifu. Pikipiki ngapi zinatumika kufanya uhalifu kwa siku? Watu wakiiba kwa internet watazuia matumizi ya internet...
 
Nadhani hiyo ni njia rahisi ya polisi kutokutumia kichwa kuzuia uhalifu. Pikipiki ngapi zinatumika kufanya uhalifu kwa siku? Watu wakiiba kwa internet watazuia matumizi ya internet...

Ndio walinda usalama wetu hao. Akili zimefika mwisho.

Ajali za barabarani zikizidi watapiga marufuku kumiliki magari.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom