Marudio ya Mitihani ya NTA Level 5 kufanyika kuanzia Desemba 13

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,216
2,000
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUVUJA KWA MITIHANI YA UTABIBU

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ina jukumu la kusimamia na kutathmini sera na miongozo mbalimbali ikiwemo ya rasilimali watu katika Sekta ya Afya nchini. Wizara inatambua umuhimu wa rasilimali watu yenye weledi na umahiri kwa ajili ya usalama wa afya za wananchi.

Mitihani ya muhula wa pili kwa mwaka wa masomo 2020/2021 ilifanyika kitaifa kuanzia tarehe 16 Agosti, 2021 hadi 30 Septemba, 2021. Wizara ilipokea taarifa ya kuwepo kwa viashiria vya kuvuja kwa mitihani hiyo siku ya mwisho ya ufanyikaji wa mitihani ya nadharia (theory examinations), na hivyo kulazimika kuunda Kamati ya uchunguzi iliyojumuisha wataalamu kutoka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama.

Kamati hiyo imefanya uchunguzi kuanzia tarehe 06 Septemba, 2021 hadi tarehe 30 Novemba, 2021 na kukabidhi taarifa hiyo kwa Katibu Mkuu (Afya) mnamo tarehe 03 Disemba, 2021. Katika uchunguzi huo kamati imebaini kwamba mitihani ya mwaka wa pili (NTA level 5) ya programu ya Utabibu (Clinical Medicine) ilivuja. Mitihani ya programu zingine zote haikuvuja.

Chanzo cha kuvuja kwa mitihani hiyo kimebainika na vyombo vya ulinzi na usalama vinakamilisha taratibu za kumfungulia mashtaka Mkufunzi aliyethibitika kufungua mitihani, kupiga picha na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii. Vile vile, chuo kilichohusika na kuvuja kwa mitihani hiyo kitachukuliwa hatua kulingana na sheria, kanuni na taratibu zilizopo ili iwe fundisho kwa vyuo au taasisi zingine.

Aidha, kupitia taarifa hiyo, Kamati ya uchunguzi imetoa mapendekezo mbalimbali kwa Wizara ya Afya na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) yatakayosaidia kuimarisha usalama wa mitihani. Napenda kuwajulisha kuwa Wizara ya Afya inakamilisha maandalizi ya mitihani ya wanafunzi wa utabibu wa ngazi ya tano (mwaka wa pili) ambayo ilifutwa baada ya kuthibitika kuwa ilivuja.

Mitihani hiyo itafanyika kuanzia tarehe 13 Disemba, 2021 pamoja mitihani ya marudio kwa wanafunzi ambao hawakufanya vizuri katika mitihani ya awali. Ratiba za mitihani kwa kozi zote za afya zimetumwa vyuoni. Wizara inawaelekeza wanafunzi kuwa watulivu na kuendelea kujiandaa na mitihani hiyo. Aidha, Wizara inawaagiza wakuu wa vyuo pamoja na wasimamizi watakaoteuliwa kuhakikisha kuwa mitihani inafanyika kwa mujibu wa taratibu na miongozo iliyopo ili kuhakikisha usalama wa mitihani.


Dkt. Aifello W. Sichalwe
Mganga Mkuu wa Serikali
 

Halaiser

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
3,469
2,000
Hatimae Wizara ya Afya yatoa mrejesho wa mtihani uliovuja wa Clinical Medicine.
20211208_061426.jpg
20211208_061413.jpg
 

balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
6,513
2,000
Hii mitihani wakabidhiwe Necta wasimamiwe na Walimu wa Shule za Msingi na Msimamizi Mkuu awe mwalimu wa Sekondari

Hawa Uhuru umeshinda wanatakiwa wawekwe kati

Wanmekosa uaminifu
 

Halaiser

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
3,469
2,000
Hii shida sana hadi mitihani ya madaktari inavuja sasa hao wanaofanya c watakua madaktari vilaza ndyo maana cku hz mtu anafika hadi level za intern halafu kumuweka mgonjwa cannula au catheter hawezi madaktari wa cku hz ni wa michongo
Kweli kabisa Mkuu.
 

Ng'wale

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
4,502
2,000
Hii shida sana hadi mitihani ya madaktari inavuja sasa hao wanaofanya c watakua madaktari vilaza ndyo maana cku hz mtu anafika hadi level za intern halafu kumuweka mgonjwa cannula au catheter hawezi madaktari wa cku hz ni wa michongo
Hivi vyuo vinatoa madaktari!?

Hata katika Universities Daktari ni MD (Medical Doctor). Ni yule aliyesoma Degree of Doctor of Medicine au yule wa Degree ya Doctor of Dental Surgery (DDS). The rest siyo madaktari.
 

G4N

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
842
1,000
cku hz mtu anafika hadi level za intern halafu kumuweka mgonjwa cannula au catheter hawezi
Kwahiyo mtu akiweza kufanya haya ndiyo daktari? Mbona manesi kibao wenye certificate tu wanayafanya haya?

Tukubaliane tu kwamba elimu ya Tanzania ina shida, ndiyo maana hakuna tofauti Kati ya daktari bingwa na daktari wa kawaida, daktari na nesi, daktari na daktari feki.

Wengi mnajiita madaktari lkn hakuna kitu kichwani zaidi ya kumiliki makaratasi (vyeti).
 

Larry barrice

Senior Member
Sep 17, 2021
114
250
Hivi vyuo vinatoa madaktari!?

Hata katika Universities Daktari ni MD (Medical Doctor). Ni yule aliyesoma Degree of Doctor of Medicine au yule wa Degree ya Doctor of Dental Surgery (DDS). The rest siyo madaktari.
Ummmh huu ujinga umeutoa wapi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom