Marubani wa ajali ya Ndege ya ATCL wanaitaji Kupewa pongezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marubani wa ajali ya Ndege ya ATCL wanaitaji Kupewa pongezi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Mar 1, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 35,998
  Likes Received: 6,820
  Trophy Points: 280
  serikali imeombwa kuwapa tuzo maalum Marubani waliokuwa wakirusha ndege ya ATCL iliopata matatizo huko mwanza ambapo walifanikiwa kunusuru uhai wa watu zaidi ya 49
  akiongea kwa masikitiko mh shibuda j amesema serikali aina tabia ya kuwashukuru watu wanaoweza kuokoa roho za watu kwenye vyombo vya usalama na matokeo yake kufanya kazi bila kuwa na morali
  ameshauri serikali ianze kwa kuwapa tuzo marubani walioweza kuokoa roho za watu 49 vinginevyo sa hizi tungekuwa tukiongea mengine,namnukuu mh shibuda,...watu wengi wamekuwa wakituma msg kutoa pole na kuwashukuru marubani kwa uwezo wao waliouwenyesha na kuwataka madereva wa barabarani waige mfano,...wakati huohuo abiria waliokufa kwenye basi la AM kutokea arusha wamefikia 22 toka 10 waliotangazwa mwanzoni,....

  Kwa niaba ya JF tunawapongeza marubani kwa kazi zao nzuri ,tunatambua uwezo wenu mliounyesha ,..muendelee hivyo hivyo kuokoa roho za watu pale mnapoitajika bila kumkumbuka MUNGU kwanza katika Safari yenu Bila yeye hata msingeweza kufanikiwa mlichofanya
   
 2. D

  Dalilah Member

  #2
  Mar 2, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Naunga mkono mia kwa mia wazo hili, ukitilia maanani jinsi walivyo jitahidi na kunusuru maisha ya abiria wote! Nina imani rubani awapo angani, hana macho wala masikio, macho yake na masikio ni ushauri kutoka "control tower" iwapo watamwambia uwanja ni salama basi rubani hana budi kufuata maelekezo hayo bila ya kuhoji zaidi, sasa marubani hawa, ambao kwa habari nilizozipata, mmoja wao ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji Capt. Ibanda, na mwingine ni rubani mzoefu Capt Mwakang'ata, sio tu walitumia ujuzi wao wa hali ya juu, bali walifanya kazi ya ziada kuhakikisha kuwa abiria wote wanasalimika. Hili ni la kujivunia kuwa tuna waTanzania wenye uwezo wa hali ya juu kama hii. Mcheza kwao hutunzwa! na wao hali kadhalika.
   
 3. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,596
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280
  Sioni sababu ya wao kupewa zawadi, labda pongezi za maneno zinatosha.
  Hilo lilikua jukumu lao,na wasingefanya hivo, hata wao wangekuwa wanachungulia kifo.
  Mbona madaktari wengi huwa wanaokoa maisha ya watu hasa wakati wa majanga kama ya kipindupindu na hakuna pongezi wanazopewaga??
   
 4. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #4
  Mar 2, 2010
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hizo ni siasa tu, ndege ilipata matatizo wakati imeishatua MICHUZI BLOG anasema eti maji ya uwanjani ndio yalisababisha iteleze, wizi mtupu ndege na uzito wake izuiliwe na vimaji???????

  SUBIRINI WATALAAM watueleze chanzo cha ajali ndio muwaze hizo tuzo.
   
 5. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 655
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Napenda kutoa msisitizo,

  Tuachane na mambo ya kishabiki. Hawa marubani hawana haja ya kupewa tuzo kwa sababu ni wajibu wake kuhakikisha usalama wa chomba na abiria.

  Sisi tumezoea kupeana sifa za kijinga, za kinafiki, za kisiasa. Mtu akitimiza wajibu wake haitaji kupongezwa. Vivyo hivyo asipotimiza wajibu wake anatakiwa kuadhibiwa.
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Thanx God ile ndege haikuleta shida kwa abiria.

  Pilots WALIOKOA NINI WAKATI NDEGE IKO RIGHT-OFF ile?

  Ni kwamba ndege iliongoza porini, na wao hawakuwa na cha kufanya wakaiacha iende hivyohivyo!...

  Mi nilitegemea uwasifu wale Air-Hostesses kwa kuwatuliza abiria na kuwafanya wakae kimya kwa utulivu bila kuanzisha vurugu!..lau wange'behave tofauti, wangesababisha madhara makubwa sana.
   
 7. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,840
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  its about time tuwe serious, if anything neneni nyumba za ibada mshuku Munfgu na kutoa sadaka ya shukrani, sio habari za kuwapa zawadi watu wanaofanya kazi yao waliosomea ipasavyo. They did what they should have done, sasa zawadi ya nini kwa mtu kufanya kazi yake kwa ufanisi, something we expect of him? Mbona watu wanaoharibu hamsemi waadhibiwe?
   
 8. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2010
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Subirini uchunguzi ufanyike kwanza, pengine ilikuwa pilot error! Hivi mamlaka ya hali ya hewa ya Mwanza haikuwataadharisha marubani wa ATCL kuhusu hali ya hewa kabla ya kutua? Kuna mengi ya kuchunguza.
   
 9. M

  MkeMwema2010 Member

  #9
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kushukuru Mungu tu kua tatizo halikutokea wakiwa angani, hata hivyo kuwashukuru kwa kazi nzuri ni jambo la muhimu na la busara sababu wangekua wazembe pia labda ndugu zetu wangepoteza maisha, wao ndio marubani wanajua zaidi sisi tutaongea na makelele mengi lakini pengine bila utaalamu zaidi baada ya maji kuingia kwenye engine labda watu wangepoteza maisha tu.
   
 10. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kama hivyo atadereva wa AM coach kama yuko hai nae apewe pongezi kwani ameokoa watu wengeni waliobaki ukiondoa hao 22 waliofariki
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 41,946
  Likes Received: 37,199
  Trophy Points: 280
  Midege mibovu, vifaa vya kuongozea ndege navyo chakavu.
  Kweli marubani wetu wanafanya kazi kwenye mazingira magumu sana.
  Hakika wanahitaji pongezi
   
 12. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  mzee umewasahau wafiwa (wahanga la ajali ya basi la AM!
   
 13. K

  Kinnega Member

  #13
  Mar 2, 2010
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata mmiliki na viongozi wa jamvi hili, kina Invisible, hawawezi kusema kitu "kwa niaba ya wana JF."

  Kuna wengine, kama mimi, ninadhani hawa marubaini inawezekana walifanya uzembe wa kulazimisha kutua sehemu yenye hali ya hewa iliyochafuka; labda ingebidi waende K.I.A au warudi DAR.

  Au inawezekana kweli hawakujua kwamba hali hairuhusu kutua, yani walipotoshwa na waongoza ndege; na kama hivyo ndivyo basi wawe wazalendo, wapige filimbi, waseme "jamani eeeh, shirika letu la ATC lilitaka kuua watu kwa uzembe wa waongoza ndege." Hapo ndo nitaseme marubani wanastahili pongezi.

  Aidha, si wote tunaoamini katika uhusika wa Mungu katika maajali yanayotumaliza Watanzania kila kukicha. Inawezekana kwa hilo amejitoa, na si ajabu hayupo kabisa!

  Kwa hiyo, bwana Impossible, unapotuongelee wote kwa ujumla wetu JF kupongeza watu ATC, mimi nitoe!
   
 14. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  :confused::(
   
 15. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 35,998
  Likes Received: 6,820
  Trophy Points: 280

  WAMEPEWA GO AHEAD WATUE HALI SHWARI


  Subirini uchunguzi ufanyike kwanza

  UNAIJUA TCAA VIZURI

  USANIIALIAZATION MTUPU HAKUNA KIPYA UTAKACHOSIKIA
   
 16. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 35,998
  Likes Received: 6,820
  Trophy Points: 280
  mkuu tukiwa tunaendelea kutafuta chanzo mpaka sasa tumepata na kusikia sauti za waongoza ndege na marubani wakijulishwa watue uwanja uko salaama
  ...mengine tutawapa baadae baada ya uchunguzi
   
 17. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  aminia mkuu,maajali mengi yanaokokeka mazee mbona zawadi hzitolewi?angalieni MV arena hapo kigamboni kila siku inazimika ndani ya maji mbona manahodha hawapewi zawadi?Ndege yenyewe ni mbovu kwa nini wasitengeneze tuuuuuuuuuuuuuuuuuu zawadi zawadi kuna watoto na kina mama kibao mahospitalini bora hizo zawadi wanunue vitendea kazi...
   
 18. Mgeninani

  Mgeninani Senior Member

  #18
  Mar 4, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna watu wamefanya vt vikubwa kwelikweli hat biscut na haya mambbo ya media ndo sasa yanatuletea sakata la Jerry Muro!
   
 19. senator

  senator JF-Expert Member

  #19
  Mar 4, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Wabongo tumezoea kutoa Rambirambi na sio Pongezi kwa ushujaa wa mtu..Yaani mpaka yatokee maafa ndo tunaanza kujipanga na kuwa serious....Binafsi kama msafiri wa Angani hao marubani imekuwa kama kudra ya mwezi mungu kwa jinsi inavyoonekana ndege ilitua kwa kutokea upande wa ziwani na sio huu upande mwingine,Ni kweli tungekuwa tunazungumza mengine kama ingeserereka mpaka kwenye ziwa..
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 35,998
  Likes Received: 6,820
  Trophy Points: 280
  Si mnileetee jamani hizo zawado
  nipeleke kids organizaition walezi wa watoto yatima
  mpate baraka....hiyo ndio kazi yao ukisema hivyo
  dk silaa nae atatakiwa apewe zawadi,....
  Anna kilango zawadi
  rostam zawadi -kwa kuweza kuchota mabiliion miaka yote na upumbafu wa watanzania
  lowassa apewe zawadi kwa kukubali kujiuzuru

  wengi wwengi sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

  hizi sawadi nileteen mimi nkagawe kwa yatima
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...