Mr. Purpose
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 1,440
- 2,692
Inafahamika kama Nunchaku. Wengine wa mtaani wanaiita Cheni (kila mmoja uipachika jina lake kwa namna yake). Tupeane experience na mbinu mbili tatu.
Uliijulia wapi na ulijifunzia/Fundishwa wapi na kwasasa uwezo wauonaje katika kutumia silaha.
Nianze, binafsi niliiona kwenye movie ya Bruce Lee kisha kuanza kuifuatilia hapo nikiwa dogo sana kisha nilipoanza mafunzo ya martial arts ndipo nilipojitengenezea yangu mwenyewe kwa kuchonga miti miwili urefu wastani kisha nilitumia mnyororo ule wa kufungua mbwa na kuunganisha kwa misumari na kupata hicho kifaa kisha nikaanza jifunza peke yangu kwa kuangalia movie, internet pia ilihusika kidogo
Nilijigonga mara kadhaa kichwani na maeneo mengine pia wakati wa kujifunza hivyo majeraha ya hii kitu niliyapata sana na vilivyo.
Baada ya kufika chuo niliamua kwenda kujichukulia yangu rasmi sasa maana nilikuwa mzoefu tayari. Mpaka sasa ukiacha mikono na miguu yangu, hii ni silaha ya pili ninyoikubali sana na ninayowez tumia muda wowote popote.
Pia matumizi ya fimbo, jambia na visu kwa wastani ila Nunchaku nikikamata nakuwa comfortable sana.
Tupe experience yako mdau. Una experience gani na Nunchaku??