Martha Karua ajitokeza hadharani kumuunga mkono Tundu Lissu

joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
26,117
46,613
- Karua amemtaka mgombea wa urais Tanzania Tundu Lissu kuendelea kujikakamua kuwinda kura
- Hayo ni baada yake kupigwa marufuku na tume ya uchaguzi nchini humo kuendelea na kampeni zake
- Lissu anapania kumtimua Rais Pomba Magufuli kwenye uchaguzi utakaofanywa wiki tatu zijazo

Kiongozi wa chama cha Narc Kenya Martha Karua anataka Rais wa Tanazania John Pombe Magufuli apate kichapo kwenye uchaguzi ujao wa urais nchini humo.

Karua anapigia debe mgombea wa chama cha Demokrasia na Maendeleo maarufu kama CHADEMA.

Martha Karua amuunga mkono mgombea wa upinzani Tanzania

Martha Karua ameonekana kumuunga mkono mgombea wa upinzani Tanzania. Picha: Standard

Mgombea wa CHADEMA ni Mbunge wa Singida Tundu Lissu na anajipasha moto kumtimua mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kiko serikalini.

Kupitia kwa mtandao wake wa Twitter, Karua aliwataka Lissu na kikosi chake kuendelea kuwa ngangari na kupambana na Magufuli.
Aliyasema hayo huku upinzani ukipitia hali ngumu baada ya tume ya uchaguzi nchini humo kuwapiga marufuku kufanya kampeni.
Tume hiyo ilisema ilichukua hatua hiyo baada ya Lissu mwenye umri wa miaka 52 kudai kutoa matamshi ya chuki dhidi ya Rais Magufuli.

Tarehe ya uchaguzi imesalia wiki tatu tu na hatua hiyo ilionekana kama pigo kubwa kwa upinzani katika kipindi hiki cha kujitafutia kura.

"Baada ya majadiliano marefu na maafisa wa chama cha CHADEMA na baada ya kuangalia sheria zilizoko, na kwa kutumia nguvu za kisheria zilizopo, kamati imeamua kumpiga marufu ya kufanya kampeni kwa siku saba kuanzia Oktoba 3," tume hiyo ilisema.

Lissu hata hivyo alipuuza hatua hiyo akisema ataendelea na kampeni zake kama awali huku akidai tume hiyo inaegemea upande mmoja.

Jumanne Oktoba 6 alijipata pabaya na maafisa wa polisi baada ya kuzuiwa kuondoka Dar es Salaam.

Source: TUKO
 
mwandishi ni takataka....

anyway hii inaonesha nguvu ya tanzania katika siasa na uchumi ktk ukanda huu wa greatlakes hata kuwavutia watu,nchi mbalimbali kutamani kuusika na mchakato kwa namna 1 au nyingine

wapambane tuu😁😁 goodluck
Mungu ibariki🇹🇿
 
- Karua amemtaka mgombea wa urais Tanzania Tundu Lissu kuendelea kujikakamua kuwinda kura
- Hayo ni baada yake kupigwa marufuku na tume ya uchaguzi nchini humo kuendelea na kampeni zake
- Lissu anapania kumtimua Rais Pomba Magufuli kwenye uchaguzi utakaofanywa wiki tatu zijazo

Kiongozi wa chama cha Narc Kenya Martha Karua anataka Rais wa Tanazania John Pombe Magufuli apate kichapo kwenye uchaguzi ujao wa urais nchini humo.

Karua anapigia debe mgombea wa chama cha Demokrasia na Maendeleo maarufu kama CHADEMA.

Martha Karua amuunga mkono mgombea wa upinzani Tanzania

Martha Karua ameonekana kumuunga mkono mgombea wa upinzani Tanzania. Picha: Standard

Mgombea wa CHADEMA ni Mbunge wa Singida Tundu Lissu na anajipasha moto kumtimua mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kiko serikalini.

Kupitia kwa mtandao wake wa Twitter, Karua aliwataka Lissu na kikosi chake kuendelea kuwa ngangari na kupambana na Magufuli.
Aliyasema hayo huku upinzani ukipitia hali ngumu baada ya tume ya uchaguzi nchini humo kuwapiga marufuku kufanya kampeni.
Tume hiyo ilisema ilichukua hatua hiyo baada ya Lissu mwenye umri wa miaka 52 kudai kutoa matamshi ya chuki dhidi ya Rais Magufuli.

Tarehe ya uchaguzi imesalia wiki tatu tu na hatua hiyo ilionekana kama pigo kubwa kwa upinzani katika kipindi hiki cha kujitafutia kura.

"Baada ya majadiliano marefu na maafisa wa chama cha CHADEMA na baada ya kuangalia sheria zilizoko, na kwa kutumia nguvu za kisheria zilizopo, kamati imeamua kumpiga marufu ya kufanya kampeni kwa siku saba kuanzia Oktoba 3," tume hiyo ilisema.

Lissu hata hivyo alipuuza hatua hiyo akisema ataendelea na kampeni zake kama awali huku akidai tume hiyo inaegemea upande mmoja.

Jumanne Oktoba 6 alijipata pabaya na maafisa wa polisi baada ya kuzuiwa kuondoka Dar es Salaam.

Source: TUKO
Ni nani huyu kwani?
 
Kwa Kenya ni aidha Uhuru Kenya au Raila Odinga waliobakia wote takataka tu, na hao magiants wawili wote ni pro Magu, ...
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom