'Marshall Plan' - Restoration and Recovery Plan for Tanzania

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Waraka wa Mchungaji kwa Watanzania

Ndugu Mtanzania,

Naomba kuwasilisha kwako waraka huu ukiwa ni mwamsho na na hamasa kwetu kama Wananchi na Taifa ili kulikwamua taifa letu kutoka katika hali mbaya ya kiuchumi tuliyonayo inayoenda sambamba na kuzorota kwa Uongozi na Utawala bora.

Matatizo ya Tanzania yamegawanyika katika makundi makubwa mawili ambayo ukiangalia kwa kina, yanaoana na kila moja kinategemea mwenziwe. Matatizo haya ni Uchumi (Umasikini, Ujinga na Maradhi) na Uongozi (Utawala holela, Uzembe, Rushwa, Uvivu, uwajibikaji).

Naomba upokee waraka huu kupima nafsi yako na wale watakao kuja kwako kuomba kura yako wakati wa uchaguzi, uwe ni wa Serikali ya Mitaa, Wabunge au Urais. Nakusihi utumie mwamko na hamasisho hili kujihoji nafsi kuwa wewe binafsi una nafasi gani na nguvu zako zina nafasi gani ili kuleta msukumo utakaoleta maendeleo ya kweli na kulikwamua Taifa kutoka kwenye shida zinazotuzingira na kutudumaza. Kutumia waraka huu, jiulize kwa makini ni nini maana ya Maendeleo na ni maendeleo ya namna gani Watanzania wanayataka na yatawasaidia vipi wao na vitukuu vyao.

Miaka 9 iliyopita niliandika haya yafuatayo hapa chini kama ningekuwa mgombea Uchagusi Mkuu 2000. Nayarudia tena kwa kuwa ni katika haya kumi (10) ndivyo Mipango ya Maendeleo kwa mujibu wa mawazo na maoni ya Mchungaji (pamoja na kuwa si mtaaluma katika Uchumi na Uongozi )yanaweza kutumika kama nyenzo na dira kutukwamua kama Wananchi binafsi, jamii na hata Taifa.
  • Kurudisha na kuimarisha Heshima, Utu na Uadhi ya Mwananchi na Taifa la Tanzania
  • Kurudisha na kuimarisha Heshima, Wajibu na Hadhi ya kazi na kufanya kazi kwa Watanzania wote, vijijini na mijini
  • Kuelimisha Wananchi haki zao kama raia, wajibu wao na sehemu yao katika Taifa na Serikali yao kupitia Katiba, Serikali Kuu, Bunge na Mahakama
  • Kuimarisha Ufanisi na Ustawi wa Jamii katika kupiga vita Ujinga, Umasikini, Njaa na Maradhi
  • Kuhakikisha kuwa Katiba, Sheria na Kanuni zilizowekwa zinatekelezeka kutokana na nyakati zilizopo, zinafuatwa ipaswavyo na vyombo vyote husika; Serikali, Bunge, Mahakama na Wananchi wenyewe. Aidha kuweka maamuzi na mipango ya Serikali wazi kwa wananchi wote ili kuhakikisha uadilifu na uwajibikaji wa Serikali haufanyiki kwa siri na na kuwapa wananchi wote haki kwa kuwa wao ndio waliotoa dhamana ya kuwepo kwa Serikali na kuruhusu Uongozi uliopo uongoze nchi
  • Kubuni mbinu za kiuchumi ili kumpunguzia mzigo mwananchi wa kawaida hasa wale wa kipato cha chini na wakulima ili kujenga nguvu kubwa ya taifa kuwa katika Tabaka la kati (middle class)
  • Kuhakikisha kuwa njia kuu za Uchumi na uzalishaji mali zinaboreshwa na kutumika kwa manufaa ya kila Mtanzania na taifa la Tanzania linanufaika kwanza
  • Kuhamasisha na kuhakakisha kuwa Uzalishaji mali (kilimo, viwanda, uvuvi, ufugaji, biashara, madini , utalii, biashara, sanaa, michezo, huduma na maofisini) unafanyika kwa dhatgi, kisayansi, kiushindani, kiuwajibikaji, kiufanisi na kwa ubora wa hali ya juu kwa kutumia tija, kuongezeka kwa juhudi na maarifa ya uzalishaji mali huu
  • Kuhakikisha kuwa huduma za msingi zinaboreshwa na kupewa kipaumbele na kufikishwa kwa wananchi ili kujenga maendeleo ya kweli kwa jamii na Taifa;- Afya, Elimu, Maji safi, Chakula, Uchukuzi na Nishati
  • Kuhakikisha kuwa vita dhidi ya Rushwa, Ubadhirifu, Udini, Ukabila, Uzembe, Ufisadi, Uhujumu, Uvivu, Uzururaji na Kutowajibika au kutokujituma kwa watendaji wa Serikali na taasisi zake (wakuteuliwa au kuchaguliwa), waajiriwa , wafanyakazi na wakulima ni vita vya Taifa zima na linahitaji ushiriki na kushirikisha Wananchi wote. Wananchi wote bila kujali kabila, rangi, jinsia, umri, elimu au mwelekeo wa kisiasa ni wajibu wao kushiriki katika vita hii
Vipengele hivi kumi (10) si vigumu sana kutuumiza kichwa. Ni mambo ya kawaida ambayo tumekuwa nayo lakini kwa miaka karibu 20, tumeondokana nayo na kuishia kuzunguka kama punguani. Tumeshindwa kuwa makini katika Uongozi kitu ambacho kimezalisha uzorotaji na kudumaa kwa uchumi pamoja na takwimu zote zinazosema kuwa uchumi wetu unakua.
Uchumi wa Tanzania utakuwa pale ambapo Mtanzania ataacha kutafuta makombo ili aweze kumaliza siku moja anayoamka akiwa hajui kesho ikoje.

Kutokana na udhoofu wa Uchumi na kuzorota kwa Uongozi, hadhi yetu na kujivunia kwetu kuwa Watanzania kama tulivyozoea kujivuna na kuimba "Tazama ramani utaona nchi nzuri... Nasema kwa kinywa na kufikiri nchi hiyo nzuri ni Tanzania" imeshuka na hatujiamini tena. tumekuwa wanyonge na kukubali kuburuzwa na viongozi wetu na hata wafadhili.

Tunahitaji kujirudishia Uzalendo na hadhi yetu kama Taifa. Tukubali makosa tuliyofanya kwa kukusudia au bila kudhamiria. Hiyo itakuwa hatua ya kwanza ya kutafuta suluhisho la matatizo yetu na kujirudishia hadhi yetu na ya Taifa letu.

Msahafu na maandiko yanasema, "asiyefanya kazi na asile". Watanzania tumesahau nidhamu na wajibu wa kufanya kazi. Tumeendekeza malalamiko na manung'uniko, huku tukipunguza tija na juhudi kulilia motisha. Kama tutageuza nguvu zetu hasi kuhusu uchapaji kazi na kuzifanya chanya kuongeza uzalishaji mali na kuachana na kutegemea misaada, basi nafasi yetu ya kuwa na maendeleo ya kudumu yanayoendelea yatakuwa makubwa na hata viongozi wetu ambao wamekosa dira na mwamko wa kutuongoza wataona aibu tutakapoamka kudai haki zetu kutokana na jasho letu.

Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuangalia Kazi kwa mtazamo wa kimaendeleo na chanya. Bila kufanya kazi, kwa ufanisi, juhudi na uhodari, hatutaweza achana na umasikini na unyonge. Iwe ni mijini kwenye maofisi, biashara, viwandani, mashambani au migodini. iwe kazi za kuajiriwa au kujiajiri, ni lazima tuheshimu kazi na kazi ziwe ni zile halali za kutupa mapato.

Hadhi na utu wa Uzalendo na Utaifa na Taifa letu, vitakuwa havina maana kama Mtanzania hatajua wajibu na haki zake Kikatiba, hatajua na kutumia Sheria na kanuni za nchi kujilinda na kujiongoza. Viapo vyetu vya utii visiishie kuwa ni viapo hewa kwa ajili ya kuapa. Tunapoapa kulitumikia Taifa na kuimba wimbo wetu wa Taifa "Mungu Ibariki.." ni lazima tuwe wakweli na wenye Uzalendo wa kweli ndani ya moyo. Kuelewa haki yetu Kikatiba kutaongeza ufanisi wetu na hasa wajibu wetu kama Raia katika kuweka Sheria za kuilinda nchi yetu na kuwa makini kuchagua viongozi wa kutuongoza kama Taifa.

Wajibu wetu mwingine ni kuhakikisha kuwa kazi yetu haishii katika kulinda katiba na kujua haki zetu kama Watanzania, bali ni kufuata sheria hizo na kuzithamini. Tuwe mstari wa mbele kufuata sheria na kanuni tulizonazo na tuwakosoe na kuwafikisha kwenye sheria wale wote ambao kwa makusudi au bila kukusudia wamekiuka sheria au kanuni. Tusiwaonee haya wale wanaopindisha sheria au kuvunja sheria biola kujali sehemu yao katika jamii. Kama Waziri anapinda Sheria ni wajibu wetu kama jamii kumwajibisha. Kama mbunge anavunja Sheria, ni wajibu kumfikisha mbele ya vyombo vya dola ili haki na hukumu kwa kuvunja Sheria ifanyike.

Sheria na kanuni hazikuwekwa zifuatwe na wananchi pekee. Watawala na Viongozi hawana kinga ya aina yeyote ya kuwaepusha kufuata kanuni,sheria au katiba. Sheria na katiba ziliundwa ili zifuatwe na kila raia na mkazi wa Tanzania.

Wakati wa Azimio la Arusha tulitamka kuwa ili tuendelee tunahitaji Watu, Ardhi, Siasa safi na Uongozi Bora. Tukatamka kuwa tunataka kujenga Taifa huru la Kijamaa na lenye Kujitegemea. Tukasisitiza kuwa vita dhidi ya Ujinga, Umasikini, Njaa na Maradhi vitashinda kama tutatumia Juhudi na Maarifa katika kazi zetu na maisha yetu.

Kazi tuliyonayo sasa si tofauti na ile ya mwaka 1967, ni ile ile na sana sana ni kulenga Nyenzo kuu za maendeleo yetu kama Taifa na kibinafsi kwa kupitia milango miwili. Ili tujikwamue kutoka hali hii mbaya tuliyonayo kama Taifa, ni wajibu wa kila mmoja wetu kuwajibika na kuwa na nia ya kweli kuyafanya yafuatayo;
  1. Kujenga Uchumi imara na madhubuti. Hili litatusaidia katika vita dhidi ya Umasikini, Ujinga, Maradhi na Njaa
  2. Kuwa na Uongozi mahiri na fanisi. Utawala na uongozi wa nchi unahitaji na unategemea Uongozi mahiri kutekeleza sera na mipango, wenye ufanisi kuhamasisha uzalishaji mali na uwajibikaji na wenye kuwa wanyenyekevu na kuheshimu dhamana walizopewa
Uchumi wetu hauwezi kujengeka kwa kutegemea misaada au wawekezaji kutoka nje kuja na kusukuma gurudumu la uzalishaji mali ili kutuongezea kipato. Aidha uchumi wetu hautajengeka kuwa madhubuti kwa kuanzisha mipango mipya au kufanya makosa yaleyale ya kale yaliyofanyika wakati wa Azimio la Arusha, Mipango ya kufufua uchumi 1985-2000 au mipango ya kuchochea Uwekezaji na kuvutia wageni washike hatamu za Uchumi ya 1992-2010.

Uchumi utakaoleta matunda ya kweli na ya maana ni uchumi utakaotokana na juhudi za wananchi katika shughuli zote za uzalishaji mali. Tunahitaji tuwe na mipango inayoeleweka na rahisi kufanikisha safari hii ya kujenga uchumi kwa kutumia mazingira yetu, rasilimali zetu na kwa faida yetu.

Moja ya njia zitakazotumika kuimarisha uchumi ni kubadilisha mfumo wa mapato ya Serikali na kudhibiti matumizi.

Kwa kuanzia, Serikali itabidi kupitia mikataba yote na kuongeza viwango vya kodi na ushuru (taxes, duty and royalties) zinazopatikana kutokana na wazalishaji mali wawekezaji. Kiwango cha asilimia 3% tunachotoza kwa shughuli za uchimbaji madini, gesi, makaa na hata huko mbeleni madini ni kidogo sana. Serikali ifuatilie kwa makini mapato halisi ya makampuni yote yanayojishughulisha na shughuli za uzalishaji mali na kuhakikisha kuwa Serikali inapata malipo ya kweli na yanayowiana na uzalishaji na mapato ya makampuni haya.

Serikali ipitie majedwali na ripoti za mapato ya kifedha (financial statements and bapance sheets) ya makampuni haya katika nchi zilikoandikishwa. Mfano pamoja na kuwa kampuni ya Barrick inatozwa asilimia 3% kama kodi kwa Serikali ya Tanzania, ni ukweli usiofichika kuwa Serikali na taifa la Tanzania linapunjwa. Mpango wangu utahamasisha kuchangua vitabu vya kampuni hii katika soko la mtaji la kimataifa kama NYSE, na kuangalia ni mapato kiasi gani ambayo wameyaorodhesha.

Mapendekezo ya kubadilisha viwango hivi vya mapato ya Serikali yanayotokana na uzalishaji mali wa makampuni mageni na hata enyeji, utahakikisha kuwa misamaha yote ya kodi na ushuru ambayo imetumika kama chambo cha kuvutia uwekezaji na kufanya biashara inafutwa au itapewa kipindi kifupi mno ili kupunguza hujuma na dhuluma. Mapendekezo ya kuongeza mapato yatakuwa ni kuongeza viwango vya kodi za mapato kwa makampuni haya kutoka 3% hadi kufikia 20% katika kipindi cha miaka mitano tangu sheria ianze kutumika.

Umiliki wa sekta za madini, uvuvi, utalii uhakikishe kuwa Watanzania kwa kupitia mashirika ya ndani yanakuwa naUshirika yanakuwa na 40% ya umiliki ili kuhakikisha kuwa Taifa haliendelei kunyonywa. Matarajio ya mpango huu ni kuwa Wawekezaji wenye utu watakubaliana na kufanya kazi na Serikali na Taifa kwa manufaa ya pande zote mbili.

Mapato haya ya kutokana na ongezeko la kodi, ushuru na umiliki yataliongezea Taifa pesa za kuweza kuondokana na misaada na mikopo ambayo imetulemaza na kutufanya kuwa tegemezi na masikini. Kuongezeka kwa mapato kutokana na kodi na ushuru kutapunguza ule mzigo wa Serikali kutegemea mazao ya chakula na biashara katika kupata fedha za uendeshaji. Mapato haya yatakuwa moja ya nyenzo kuu za kujenga uchumi kwa kutumika katika kuboresha sekta za Elimu, Afya, Miundombinu na Nishati.

Itaendelea...
 
Last edited by a moderator:
Inaendelea...

Aidha, Serikali itabidi iweke mkazo katika kubana matumizi na kuhakikisha hakuna ufujaji wa mapato au kuvuka viwango vya bajeti. Ripoti ya Mkaguzi mkuu wa mahesabu ya Serikali ya mwaka 2006-2007 inaonyesha matumizi na udhibiti mbaya wa pesa za Serikali zote za matumizi na maendeleo.

Kupunguza na kubana matumizi haya kutafanikiwa kwa kupunguza ukubwa wa Serikali, kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kudhibiti matumizi holela ya mapato, malipo hewa au malipo yasiyo na vithibitishi. Masalio yote ya pesa ambazo hazikutumika katika mwaka wa fedha yarudishwe Hazina na yasitafutiwe matumizi, bali zitumike kwa shughuli za maendeleo.

Moja ya mambo ambayo yamegeuka kuwa utamaduni katika Serikali na ajira Tanzania ambayo huongeza marudufu matumizi ambayo yanachochea ubadhirifu ni kuwepo kwa ongezeko la masurufu na malipo ya ziada kwa ajili ya kushiriki kwenye makongamano, semina, kusafiri nje ya kituo cha kazi au kuwa mjumbe wa kamati maalum.

Serikali inapoteza pesa nyingi kwa kugharamia "mishahara" ya ziada ambayo inalipwa ili watu watimize wajibu wao. Mfano hakuna sababu kwa wajumbe wa kamati za bunge au tume za Rais kama ile ya EPA kulipwa masurufu ya kazi (allowance) huku wanapokea mishahara na kuwepo kwa katika Kamati au Tume ni moja wa wajibu na majukumu yao ya kazi.

Misafara ya ndani na nje ya nchi inapaswa kupunguzwa na Serikali itabidi ifute masurufu yanayolipwa wafanyakazi wake au wa mashirika ya umma kwa kushiriki katika vikao au safari nje ya vituo vyao vya kazi. Wajibu wa Serikali kwa mtumishi anayesafir nje ya kituo cha kazi ni kuilpia nauli, chakula na mahali pa kulala na si mshahara au marupurupu.

Misafara na kusafiri daraja la kwanza ni gharama kubwa. Hakuna ulazima wa misafara na uwakilishi wetu hasa nje ya nchi uwe wa kila mtu na kila kitengo. Ukiondoa Raisi, Makamu wake, Waziri Mkuu, Spika na Jaji Mkuu, viongozi wengine wote wasafiri katika madaraja ya kawaida na si first class. Rais anaposafiri, hasa nje ya nchi hahitaji kuongozana na msururu wa Wafanyakazi, viongozi au wapambe. Asafiri na wale ambao ni muhimu kwa mujibu wa madhumuni ya safari hiyo.
Serikali yetu imeshindwa kuwa makini na kuongeza matumizi yasiyo ya msingi ili kuhimili shinikizo na kutimiliza wajibu wa kisiasa. Mfano mzuri ukiwa ni ile Semina ya viongozi wakati awamu ya nne iliposhika madaraka kule Ngurdotu na zile safari za Mawaziri na watendaji wa Serikali mikoani kutuliza fukuto la vita vya Ufisadi, kwa kutumia kisingizio cha kutangaza na kuelimisha umma kuhusu bajeti.

Serikali pia inabidi kuachana biashara ya kuwa "wenye nyumba" au Teksi.

Ukiondoa Raisi, Makamu wa Raisi, Waziri Mkuu, Spika, Jaji Mkuu, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Wakuu wa majeshi ya Ulinzi na Polisi, viongozi wengine wote wa Serikali, majaji, mahakimu, makatibu wakuu, wakurugenzi, wakuu wa wilaya , wabunge na wengineo wote, watabidi waingie gharama kutokana na mishahara yao kulipia gharama za nyumba na usafiri wao kwenda na kutoka kazini. Serikali inaingia gharama kubwa kutunza nyumba hizi na magari ambazo si za muhimu. Dhana ya kuufuma na kupata kila kitu kwa bure inabidi iishe. Serikali ipunguze madaraja ya Watendaji wake ambao wanastahili kupewa na kuishi katika nyumba za serikali na kutumia magari ya Serikali.

Kama Taifa tunaingia gharama kubwa sana kwa kuwapa viongozi "marupurupu" ya kuwa na magari mpaka matatu ya kazi, madereva, mafuta kwa hata safari binafsi, kuwa na nyumba za serikali huku watendaji hawa wakilipiwa umeme, maji, simu na hata chakula.

Taifa letu halijawa na utajiri mkubwa kiasi hicho kuendekeza ufahari ambao ni ufujaji wa mali na mapato.Tanzania ni nchi masikini, lakini tunajiendesha kwa majigambo na tunatumia fedha hovyo bila woga na kujiuliza tunapata wapi pesa kujiendesha. Pendekezo litakuwa ni kuwapa mikopo kununua magari, kuwalipisha kodi za pango la nyumba na kuhakikisha kuwa wanalipia bili zao za umeme, maji, simu, watumishi wa ndani na chakula chao.

Itaendelea....
 
Inaendelea...

Uchumi utaanza kujengeka kwa kuanza kujenga misingi bora ya maarifa na hii ni kupitia sekta ya Elimu.

Elimu

Mfumo wa elimu wa Tanzania unabidi kubadilika na kuhakikisha kuwa tunajenga mfumo wa elimu ambao unachochea ubunifu, unarahisisha uzalishaji mali na unawiana na maendeleo yetu. Kuna haja ya kuachana na mfumo wa Elimu ya kufaulu na kuhakikisha kuwa kinachofundishwa kinaeleweka na kinaweza kutumika ipaswavyo na wanafunzi wote, kuanzia chekechea, shule ya msingi, sekondari, vyuo vya fani stadi na hata elimu ya juu.

Mpango wa Rev. Kishoka kuboresha Elimu ni kuhakikisha kuwa mitaala na silabasi za kufundishia zinalingana na mahitaji ya jamii. Kipaumbele kitakuwa si kuongeza shule ili kuongeza maarifa na taifa la walioelimika, bali ni kuwa na elimu ya kiwango cha juu, elimu ambayo itafundishika kwa urahisi na kuweza kutumika kwa vitendo kadri wanafunzi wanavyoendelea kujifunza.

Mkazo utakuwa ni kuwa na walimu wenye uwezo wa kufundisha na wenye mapenzi katika fani ya ualimu. Waalimu watapewa kila nyenzo zinazohitajika kuhakikisha kuwa kazi zao zinafanyika kwa ufanisi na mafanikio na matunda ya kazi zao yanaonwa na kupokewa na jamii nzima.

Katika mpango wangu, kila Wilaya itapaswa kuwa na Shule si chini ya mbili za Sekondari na chuo cha ufundi ambazo zitakuwa chini ya mamlaka za Tamisemi. Kila mkoa utapaswa kuwa na shule za sekondari ya elimu ya juu si chini ya 4, Vyuo vya ualimu, uuguzi na utabibu, kilimo, uvuvi na mifugo, , biashara na uhasibu, ufundi (mithili ya Dar Tec), sanaa utamaduni na michezo.

Katika elimu ya juu ya kiwango cha Chuo kikuu, msukumo utakuwa wa kuwa na chuo kikuu kwa kila mkoa ifikapo mwaka 2050. Katika hili, uchochezi wa kupanuka kwa sekta ya kilimo utajumuisha watu binafsi, taasisi za kidini na jumuiya za maendeleo za mikoa.

Jukumu la Serikali kuu litakuwa ni kuratibu mfumo wa elimu na si kuendesha kila kitu kuhusiana na Elimu. Chini ya mpango huu, Serikali Kuu itasaidia kwa kipindi cha miaka minne kwa shule na vyuo kujijenga na uendeshaji wake na baada ya hapo, jukumu litakuwa katika Serikali ya mitaa na jamii kuhakikisha kuwa wajibu wa kuziendesha shule na vyuo hivi havitegemei Serikali kuu pekee.
Serikali kuu itakuwa tayari kutoa msaada na ushauri. Serikali kuu itajenga mfuko na mfumo mpya wa mikopo ya Wanafunzi na kuachana na bodi ya mikopo ya Wanafunzi iliyoko sasa hivi ambayo ni kero kwa wananchi na wanafunzi.

Matarajio ya mpango huu wa elimu ni kuwa kwa kusogeza mchakato mzima wa elimu kwa mamlaka za mikoa, zitasaidia ile dhamira ya kusukuma madaraka mikoani, wananchi wa mikoa na wilaya watapata fursa sawa na wale walioko katika mikoa mingene ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikinufaika kwa kuwepo kwa kila aina ya shule na vyuo.

Msisitizo utakuwa katika elimu ambayo itazalisha watu ambao wako tayari kufanya kazi. Fani kama uhunzi, uashi, useremala, ufundi mchundo, bwana shamba, bwana maji, fundi umeme, magari, na ujenzi zitaongeza idadi ya watu wenye ujuzi si wa asili na kuvumbua binafsi, bali kwa kupata mafunzo na nyenzo za kuboresha vipaji asili katika fani hizo.

Tutakapoweza kuwa na msingi bora wa elimu ambayo utaongeza maarifa na kuchochea juhudi za kila mmoja wetu na kuhakikisha kuna ushiriki wa kila mmoja na kila mmoja ana nafasi ya kuwa bingwa katika fani yake, masuala kama ukosefu wa ajira au kukosekana kwa walio na utaalamu katika fani mbali mbali utapungua.

Lakini hatutaweza kufanikisha azma ya kuwa na mfumo na elimu bora ikiwa maslahi na vitendea kazi vya waalimu na shule zetu vitaendendelea kuwa duni na dhaifu, huku Serikali ikifumbia macho na kusukuma wajibu huo kwa Wananchi, Waalimu na uongozi wa shule na vyuo hivi. Suala la maslahi ya waalimu nitaliongelea kwa mapana na marefu katika kipengele cha Ujira, Mishaharana maslahi ya Wafanyakazi.

itaendelea...
 
inaendelea...

Afya

Hakuna jamii yoyote itakayoweza kuendelea bila kuwa na mipango madhubuti ya kiafya. Rev. Kishoka plan italenga katika kuhamasisha afya kwa kutumia kinga na si kusubiri matibabu. Kila wilaya itakuwa na hospitali ya wilaya, yenye waganga na wauguzi wa kutosha walio mahiri na wenye nyenzo tosha kufanya kazi zao kwa uhodari na ufanisi, na kila Mkoa utakuwa na hospitali kuu ya mkoa ambayo itakuwa ni ya rufaa na uwezo kama hospitali za Muhimbili, Mawenzi, Arusha , KCMC au Bugando.

Nia na mwongozo utakuwa si kutibu tu bali ni kutoa kinga na kuhamasisha kinga, kila wilaya itapaswa kuwa na mipango madhubuti ya afya ambayo itashabihiana na malengo ya Serikali kuu katika mipango ya kuimarisha afya. Serikali itatumia ushawishi kuhamasisha sekta na taasisi binafsi hasa za kidini kuanzisha na kusambaza Hospitali katika mikoa na wilaya. Serikali itawekeza nguvu na mkazo katika bajeti zake kuhakikisha kuwa katika kata na tarafa kunakuwa na zahanati ambazo zitaweza kutoa huduma ya kwanza na za kawaida kwa wananchi wa maeneo ya kata na tarafa hizo.

Elimu ya afya bora itahamasishwa katika ngazi zote za elimu, na jamii kwa ujumla. Mipango ya lishe na chakula bora, uzazi na malezi bora, mimba kwa watoto na wanafunzi, chanjo muhimu kwa watoto, vita dhidi ya kipindupindu, malaria, kwashiakor, huduma kwa walemavu na wazee, utapiamlo na ukimwi vitakuwa ni vitu ambavyo vitakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha tunajenga kinga na tuna uwezo bora wa kutibu pale inapiobidi kutibu.

Maji safi ni sehemu ya Afya ingawa tunaweza kusema maji yanahitaji sehemu yake maalum. Kama kigezo cha afya, suala la maji safi na umuhimu wa maji safi utaendelea kufundishwa kila ngazi, mashuleni, vyuoni, kwenye kata, tarafa wilaya na mkoani.

Taifa lenye maarifa kutokana na elimu nzuri na afya njema, ni taifa ambalo litakuwa tayari kuwa na juhudi na mwamko kufanya kazi kwa juhudi ili kujikwamua kutoka umasikini na utegemezi.

itaendelea...
 
...excellent reverend,atleast una idea nini cha kufanya tukikupa nafasi,ila plan zako nyingi zinaonekana ni centralized kitu ambacho naamini ndio kimetuletea umaskini na wengine kuwa miungu mtu kwenye nchi yetu,angalia mfano wa wachaga walioamua kujenga shule zao binafsi tangu wakati wa Nyerere wako mbele kuliko mikoa mingi iliyokuwa inasubiri serikali na ndio maana leo wanalalamikiwa wameshika nafasi zote za juu ,its good to encourage & support efforts za wananchi ila sio kuwaambia wafanye this & that,mimi sio mchaga lakini nawazimia sana hawa jamaa kwa moyo wao wa kutafuta na kujiendeleza
 
inaendelea...

Kilimo

Asilimia 80 ya Watanzania wanaishi vijijini na wanategemea Kilimo, Uvuvi na Ufugaji kama vyanzio vuya mapato ili kujipatia maendeleo. Kilimo chetu ni cha kujikimu, tunalima japo kidogo kututosha kwa leo na kesho, lakini msukumo wa kulima chakula cha kutosha hata mtondogoo na wiki mbili zijazo hatuna.

Hii inatokana na sera na nyenzo duni katika uzalishaji mali katika kilimo, uvuvi na ufugaji. Chini ya mpango huu, msukumo wa kuchochea mapinduzi ya kilimo utafanywa. Zile nguvu za sera ya Kilimo cha Kufa na Kupona zitatumika kuhamasisha Wakulima kutumia utaalamu wa kutumi pembejeo za mbolea, kuachana na majemb e ya mkono na kuanza kutumia maksai au matrekta, kutumia mbegu bora na kutunza mazao yao kwa kujenga maghala imara.

Serikali itarudisha ruzuku katika zana za kilimo na shughuli za kilimo. Serikali itatoa msamaha wa ushuru na kodi kwa vitendea kazi vya kilimo kwa muda wa miaka mitano ikiwa ni uchochezi kwa wakulima, wafugaji na wavuvi, kujipatia nyenzo bora kwa unafuu ili kuimarisha shughuli za uzalishaji mali.

Kwa kupitia wizara ya Kilimo na taasisi za kilimo na vyuo vya kilimo, ubwana shamba, mifugo au uvuvi, Serikali itatoa changamoto kwa ushindani wa kilimo cha chakula na biashara na kuhakikisha kuwa kila kata na tarafa zina mabwana shamba wa kutosha ambao wanaelewa kazi zao na wanaweza kufundisha wakulima, wafugaji na wavuvi mbinu mpya na za kisasa za kilimo.

Pamoja na kuwa binafsi sikubaliani sana na matumizi ya mbegu maalum (Genetically Modified), Serikali itapaswa kutoa msukumo kwa maeneo maalumu ya kufanya majaribio ya kutumia mbegu hizi ili kuona na kupima uzalishaji mali, athari na masoko kutokana na mazao yanayotokana na mbegu maalum.

Kilimo cha matunda, maua, viungo vya kupikia (spices), ufugaji wa kuku, ng'ombe wa nyama na maziwa, mbuzi wa nyama na hata maziwa na hata ufugaji na kuzalisha farasi ni vitu ambavyo vinaweza kwa uwezo mkubwa kutuongezea kipato na si kudhania kuwa kilimo ni lazima kiwe cha mahindi, nyanya, kahawa na maharage pekee.

Mkazo utakuwa katika uzalishaji chakula cha kutosha kulisha Tanzania na hata kulisha Afrika Mashariki na Kati nzima. Mbinu bora za ukulima wa kisasa ikiwa ni pamoja na kuwezesha Wakulima kupumzisha ardhi hata kwa mwaka mmoja vitafanikiwa ikiwa wakulima watafundishwa na kusukumwa kuachana na kilimo cha kujikimu (subsistance).

Tanzania imejaliwa kuwa na vianzio vingi vya maji, mabwawa, mito na maziwa. Haya ni tosha sana kuhakikisha tunakuwa na mfumo bora wa umwagiliaji maji ikiwa kuna shida au kutotabirika kwa mvua.

Aidha katika shughuli za kilimo, hamasisho la kulima misitu ya mbao litawekwa kwa wananchi ambao wako kwenye mikoa ambayo ina rutuba ya kuzalisha misitu ya mbao. Mbinu za kitaalamu za sayansi kutoka kwa mabwana shamba wetu zitatumika kufanikisha lengo hili.

Taifa letu linabidi lirudi katika ramani ya kuzalisha Chai, Tumbaku, Kahawa, Pamba, Pareto, Katani, Korosho, Karafuu kwa ubora na kuwa katika ngazi za juu za uzalishaji wa mazao haya ya biashara. Msukumo hautakuwa kuzalisha kwa ajili ya kusafirisha nje tuu, bali utatumika kama kichochezi cha kuanzishwa viwanda vya kusindika (process) na kuzalisha zao la mwisho na mauzo yetu nje ya nchi yatakuwa ni bidhaa ambazo ni tayari kwa matumizi na si kwenda kwenye viwanda Ulaya, Marekani au Asia kuboreshwa na kuuzwa kwa mtumiaji.

Motisha kutoka Serikali kuu utahitajika ili kuanzisha wakulima wa mashamba makubwa (farmers) na kuwakusanya wakulima wadogo wadogo (peasants) kufanya kazi kwa ushirika ili kuimarisha jamii. Makosa yaliyotokea wakati wa Sera ya Vijiji vya Ujamaa, Vyama vya ushirika yanapaswa yaepukwe.

Vyama vya Ushirika vya wakulima, wavuvi na wafugaji, viundwe na wakulima wenyewe na viongozwe na wakulima na si wanasiasa au kufanywa ni vyombo vya siasa. Dhamana ya kuvijenga vyama vya ushirika wa Wakulima ni ya wakulima wenyewe. Shughuli za Kilimo, Uvuvi na Ufugaji havitakuwa jukumu la wakulima pekee, bali viwe na uratibuwa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Mifugo, Chama cha Wakulima TFA, Vyuo vya Kilimo kama SUA, TAFICO, Ranchi za Taifa bodi za mazao za Ushirika kama KNCU na Mamlaka za mauzo kama Kahawa, Tumbaku na Pamba.

Ukulima wa kisasa si jambo la kutuchukua miaka 10 kuanza kufanyiwa kazi, ni jambo la kuanza kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo na Serikali isilipuuzie au kutokulipa umuhimu na kipaumbele.
Tanzania bado inategemea 50% ya mapato yake yatokane na Kilimo na 80% ya wananchi wake ni wakulima, wafugaji na wavuvi. Neema tulizonazo ni nyingi kwa Taifa kuhangaika tunapokosa mvua kutokana na tishio la njaa. Hili lisitokee tena, nafasi ya kusahihisha yaliyopita tunayo, na sababu tunazo.

Lengo kuu litakuwa kwa Taifa kuweza kujitosheleza kwa Chakula na kuachana na mtindo wa kuagiza kila kitu mpaka pilipili. Ili kusisimua uzalishaji mali wa Chakula, Serikali itaweka udhibiti mkali katika uagizaji wa Chakula. Mbinu moja ya kuhamasisha uzalishaji mali wa kilimo utakuwa ni kutoa Ruzuku kwa Wakulima na zana za Kilimo, kuwa na kodi nafuu kwa bidhaa zinazozalishwa ndani na kuongeza marudufu viwango vya kodi na ushuru kwa vyakula vya kuagizwa ili kulinda uchumi wa ndani na mkulima.

Ikiwa Mataifa makubwa yaliyoendelea yanamlinda Mkulima wa nchi yao, iweje sisi "masikini" tushindwe kumlinda Mkulima wetu kwa kumpa unafuu wa kuzalisha Chakula na kumlinda kiushindani na vyakula vya kuagizwa?

itaendelea....
 
inaendelea..

Miundombinu na Nishati

Sasa hivi moja ya vikwazo vya kusambaa kwa maendeleo nchini ni kutokana na kuwa na miuondombinu mibovu na utegemezi wa mafuta na mvua katika kupata nishati.

Tangu mkoloni ajenge reli ya kati na Mchina kutusaidia na TAZARA, hatujawekeza msukumo wa kupanua au kuboresha mfumo wetu wa reli. Hali kadhalika hali ya barabara zetu na vyombo vya majini ni mbaya kwa kuhatarisha usalama na mwenendo mzima wa maendeleo.

Katika mpango huu wa Mchungaji, Serikali iweke mipango na malengo ya kuhakiksha kuwa ujenzi na upanuzi wa barabara kuu unafanyia katika kipindi cha miaka 30. Lengo litakuwa ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2050 kila mkoa na wilaya Tanzania itakuwa imeunganika katika mfumo mkuu wa barabara bora na imara ambazo ni za lami na upana wa kutosha ili kurahisisha usafirishaji na uchukuzi.

Aidha Reli zetu za Kati, Arusha na TAZARA zipanuliwe na kurekebishwa ili kuhakikisha kuna ufanisi wa usafiri wa watu na mizigo. Kwa kuwa kuna lengo la kuunganisha jumuiya ya Afrika ya Mashariki na Kati na hata kupitia SADC kwa kuwa na mfumo mzuri wa uchukuzi kupitia Barabara na Reli, Serikali kwa kutumia wataalamu wa ndani na wa nje na wahisani itaweka mpango kabambe wa kufufua na kujenga barabara kuu na reli ambazo zitakuwa za viwango vya kimataifa na kurahisisha mtiririko wa maendeleo na huduma si kwa Tanzania pekee bali hata kwa majirani zake.

Katika nishati, nia ni kuachana na utegemezi wa mafuta na mvua kuzalisha umeme. Tanzania imejaliwa kuwa na mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme, lakini kutokana na kutotabirika kwa mvua na hali ya mazingira duniani ambayo yamepunguza mvua na vina vya maji, kuna haja ya kuwa na mpango wa kutumia na kuzalisha umeme kwa kutumia upepo na mionzi ya jua.

Lengo litakuwa ni kuhakikisha kuwa kwa kutumia sheria mpya za ushindani za EWURAS, vyanzo vipya vya nishati vinahamasishwa na kupewa kipaumbele. Maeneo tambarare kama Dodoma na Singida, yana uwezo mkubwa sana kuzalisha umeme wa upepo ambao unaweza kulisha zaidi ya 30% ya mahitaji ya umeme kwa Taifa. Hali kadhalika umeme wa jua, tuna maeneo mengi na hasa vijijini ambako kama tutaweka kipaumbele na jitihada, basi kila nyumba ya Mtanzania ifikapo mwaka 2050 itakuwa na umeme, uwe ni wa maji, upepo, jua au mafuta.

Kuwepo kwa nishati ya kutosha isiyochechemea itasaidia uzalishaji viwandani na kuboresha uhifadhi wa mazao na vyakula katika ghala kwa kuwa kutgakuwa na umeme wa kuaminika.

Ni katika sekta hii, Serikali itatoa vichocheo kwa wawekezaji wa ndani na wan je ambao watakuwa na uwezo katika kipindi cha miaka 5 kuthibitisha wana uwezo wa kuzalisha Umeme wa nguvu za jua na Upepo. Serikali itatoa msamaha na kurejesha 75% ya kodi iliyolipwa katika miaka mitano ya kwanza ikiwa miradi hii itakuwa tayari imeshafanya kazi bila wasiwasi katika miaka 7 ya kwanza tangu shughuli nzima za uzalishaji nishati zianze.

Kusambaa kwa nishati vijijini hakutasaidia hifadhi za chakula pekee, bali kutasaidia hata kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji miti ili kutengeneza makaa na kupata kuni za kupikia.

Serikali itapendelea ushindani wa uzalishaji umeme vijijini uendeshwe sin a watu binafsi pekee, bali mashirika ya maendeleo ya wilaya au mikoa kuchukua jukumu hili na ikiwezekana hata mashirika haya yawe ya ushirika wa wanavijiji.

itaendelea...
 
inaendelea...

Viwanda, Mashirika, Huduma na Biashara

Makosa ya Azimio la Arusha ni sawa na yale mapinduzi ya viwanda ambayo yalifanywa na Stalin kule Urusi na hata Mao wa China na ile sera ya Great Leap Forward. Aidha makosa ya wakati wa kubinafsisha viwanda miaka ya 1990-2008 ili kuachana na kuendesha viwanda kutokana na ufanisi mdogo na kuingia hasara hayatarudiwa.

Tumejifunza kuwa tunataka kuwa na viwanda, lakini kilichotushinda hapo awali ni kukosekana utaalamu, motisha, ubunifu na tija katika kuendesha viwanda hivi. Viwanda kama Machine Tools, Mgololo, Ufi, Mwatex na vinginevyo havikustahili kufa.

Makosa ya kuzubaa na kuendelea kuvikamua na kutumia mapato ya viwanda hivi kwa kazi nyingine ambazo hazihusiani na shughuli za uzalishaji mali wa viwanda hivi kama kujijenga kisiasa na vyama vya siasa, ulisababisha kwa kiwango kikubwa kuanguka kwa viwanda vyetu. Makosa ya kubebesha Mashirika na Viwanda mzigo wa Public Welfare, haukuwa mzuri. Ni mfumo huo ambao ulisababisha mapato ya wafanyakazi kudumaa na hivyo kuchochea vitendo vichafu ambavyo viliua moyo wa uchapa kazi, uwajibikaji na uadilifu.

Mpango wa Mchungaji ni kurejesha viwanda vya kusindika mazao ya chakula na biashara, viwanda vya mchecheto (processing) mazao kama katani, pamba, viwanda vya bidhaa za matumizi ya nyumbani na viwanda na yote haya ni katika jitihada za kupunguza uagizaji wa bidhaa za matumizi kutoka nje. Motisha utatolewa kwa viwanda vya zana za kilimo na ujenzi.

Msukumo wa kujijenga kiviwanda utalenga kujenga na kuimarisha viwanda kutokana na rasilimali tulizonazo zikiwa ni pamoja na kilimo na chakula, mifugo, uvuvi, misitu, madini, ngozi, nguo, madawa, mbolea, na kama tutakuwa na uwezo, viwanda vya teknolojia kama vifaa vya umeme.

Kwa kuwa tutakuwa tumeweka nguvu katika nishati, kuwepo kwa umeme wa kutosha kutakuwa ni motisha kukaribisha viwanda vya wawekezaji wa kimataifa ambao hukimbia nchi zao kutokana na gharama kubwa za uzalishaji na kutafuta gharama rahisi za kuzalisha mali. Kukaribisha wawekezaji hawa, hakuna maana kuwa Tanzania itakubali wafanyakazi wake wanyonywe au kudhalilishwa kwa kuwa ni cheap labor. Serikali itahakikisha kuwa sheria za kazi za nchi na kimataifa zinafuatwa ikiwa ni pamoja na kanuni za usalama viwandani.

Mashirika kama SIDO na NDC, yatapewa msukumo wa kuchocha ukuaji wa viwanda na taaluma za ndani. Wahitimu kutoka vyuo vya VETA , watapewa miongozo na usimamizi na kusaidiwa shughuli zao kupitia SIDO. NDC itarudishwa kuwa nguvu iliyoleta maendeleo ya viwanda kabla ya zoezi ka kuuza mashirika.

Kama Taifa, tumejijenga kwa kuwa na biashara ndogo ndogo na si biashara kubwa. Tumejenga utamaduni wa kukimbila biashara za bidhaa dhaifu na zisizo na ubora na kutokana na mtazamo duni, tunashindwa kukabili ushindani wa kibiashara kutoka kwa wageni.

Elimu ya biashara, utunzaji mahesabu, bajeti, masoko na matangazo ya biashara, yatasaidia sana kuhakisha sekta hii ya biashara na viwanda inakuwa kwa ushindani na umahiri. Tukiangalia wenzetu Wakenyana hata Rwanda, mipango yao ya maendeleo ni shirikishi katika kuelimisha wafanyabiashara wao mbinu bora za kufanya biashara.

Bodi kama BET na BIT zinabidi ziungane na TCCIA kuwa na mikakati bora ya kuimarisha viwanda na biashara.

Pendekezo moja ambalo litasaidia jamii na wafanyakazi katika nyanja hii na hasa katika Viwanda na Mashirika ya Biashara na Huduma ya umma ni kuanza kuwashirikisha wafanyakazi katika umiliki wa vyombo hivi kwa kutoa hisa za mashirika haya kwa wafanyakazi wake, ili nao wanufaike na mgawanyo wa riba za mapato. Hii itakuwa ni motisha na kichocheo kikubwa cha kujenga Uwajibikaji, Uaminifu, Tija na Utii (loyalty).

Katika kila nyanja ya uzalishaji mali, huduma na kuwa na malengo bora ni kiini cha mafanikio. Waliosema kuwa mteja ni mfalme hawakukosea. Viwanda, Mashirika na Wafanyabiashara wetu wanabidi kujizatiti na kukabili ushindani kwa kuwa na huduma na bidhaa bora, kuwa watangazaji wa bidhaa za ndani ili kuongeza mapato ya ndani

itaendelea...
 
Inaendelea...

Serikali pia inabidi kuachana biashara ya kuwa “wenye nyumba” au Teksi.

Itaendelea....

Bravo Rev,Bravo Rev!!!!!
kuna nguvu za ziada zinahitajika sana,sio tu katika mfumo wa utawala bali watawala wenyewe na warithi wake(au wao jirithisha),inanishangangaza kusema umeme wa jua gharama wakati tuna vijisenti vyakulipa kina richmunduli & CO kwa siku Majisenti ya kufuru kwa dharura ya miaka miwili hivi,halafu isitoshe kila kukicha umeme wakubeep,nyakati wajameni ,nyakati wajameni
 
Hizi ndizo bongo tunazohitaji pale Dodoma na kule Magogoni. Kwa bahati mbaya Dodoma na Magogoni ni kama choo cha kwenye Park, kila mtu anaweza kuingia
 
Safi sana mkuu!

Ila hiyo ya elimu ni kama ya CCM, labda mtatofautiana utekelezaji!!

Inaruhusiwa kuiba hii na kuipeleka sehemu?
 
Waungwana,

Mkiangalia kwa makini, suluhisho la matatizo yetu ni jepesi sana. Kinachokosekana si uwezo kwa kusuluhisha na kuonda umasikini na utawala mbovu, bali ni kukosekana kwa utashi kutoka kwa waliopewa dhamana.

Tanzania ina uwezo mkubwa sana kujitegemea. Hayo niliyosema ya kuwepo kwa Shule, vyuo, hospitali na zahanati yanawezekana kabisa pamoja na ujenzi wa mfumo bora wa Barabara na nishati.

Tatizo tumelea visingizio kuwa hatuna pesa. Kama hatuna pesa, imekuwaje tumeibiwa pesa nyingi hivyo BOT na tunawaambia wafadhili wasihofu kwa kuwa hiyo pesa ilikuwa haina matumizi?

Inakuwaje tunakuwa na matumizi ya Shilingi Trilioni 3 ambayo hayadhibitiwi na hayana nyaraka kuthibitisha matumizi?

Serikali ikijifunga mkanda na kuwa waungwana kuwaomba Wananchi wajifunge mkanda, kubana matumizi, kila kona ya nchi itakuwa na Umeme, Maji, Shule, Hospitali na Usafiri wa kuaminika. Zaidi kupanuka na kuongezeka wa huduma hizi kutachochea kuongezeka kwa ajira na kupunguza watu kukimbilia miji mikubwa.

Lakini sidhani kama CCM watakuwa na nia ya kweli kuhakikisha hili linafanikiwa. Kwa kupitia Unyonge na Umasikini wa Mtanzania, CCM imeendelea kutawala nchi.

Angalia ni jinsi gani Umasikini unavyouza utu. Chama cha Viziwi Tanzania wametoa tamko kushutumu hatua ya KKKT kukataa mambo aliyoyafanya Rostam na wanadai kuwa wao CHAVITA wanashida hivyo watapokea msaada wowote kutoka kwa Rostam. Sasa pesa hizo ni tamu ingawa ni haramu?

Ni lini Mtanzania atajifunza kuachana na ulimbukeni wa kukubali kunyanyaswa? kwa nini Mtanzania asianze kuwaMaskini Jeuri kwa CCM?

Kitila ombi lako nimelisikia, nikimaliza kuandika plan nzima, nitakutumia katika word format, isambazeni kwa kila mwenye masikio na macho asome achambue na atumie plan hii kujiendeleza na kudai kwa nguvu maendeleo katika maeneo yao.

Nakaribisha constructive criticism, pindi nitakapo maliza kuwasilisha plan. Main objective ni kuanzisha msukumo chanya wa kuanza kufundisha Watanzania na kuwaonyesha yanayowezekana. tumeshalalamika sana na kukosoa sana, lakini hatujachukua fursa kuonyesa yanayowezekana na yanapuuzwa na Serikali kwa kuwa wanadhani hatuna uwezo kujua yanawezekana!

Mwambieni Allien aka GT aka Dr. Who kuwa nimeitika wito wake!
 
Waraka wa Mchungaji kwa Watanzania

Ndugu Mtanzania,

Naomba kuwasilisha kwako waraka huu ukiwa ni mwamsho na na hamasa kwetu kama Wananchi na Taifa ili kulikwamua taifa letu kutoka katika hali mbaya ya kiuchumi tuliyonayo inayoenda sambamba na kuzorota kwa Uongozi na Utawala bora.

Matatizo ya Tanzania yamegawanyika katika makundi makubwa mawili ambayo ukiangalia kwa kina, yanaoana na kila moja kinategemea mwenziwe. Matatizo haya ni Uchumi (Umasikini, Ujinga na Maradhi) na Uongozi (Utawala holela, Uzembe, Rushwa, Uvivu, uwajibikaji).

Naomba upokee waraka huu kupima nafsi yako na wale watakao kuja kwako kuomba kura yako wakati wa uchaguzi, uwe ni wa Serikali ya Mitaa, Wabunge au Urais. Nakusihi utumie mwamko na hamasisho hili kujihoji nafsi kuwa wewe binafsi una nafasi gani na nguvu zako zina nafasi gani ili kuleta msukumo utakaoleta maendeleo ya kweli na kulikwamua Taifa kutoka kwenye shida zinazotuzingira na kutudumaza. Kutumia waraka huu, jiulize kwa makini ni nini maana ya Maendeleo na ni maendeleo ya namna gani Watanzania wanayataka na yatawasaidia vipi wao na vitukuu vyao.

Miaka 9 iliyopita niliandika haya yafuatayo hapa chini kama ningekuwa mgombea Uchagusi Mkuu 2000. Nayarudia tena kwa kuwa ni katika haya kumi (10) ndivyo Mipango ya Maendeleo kwa mujibu wa mawazo na maoni ya Mchungaji (pamoja na kuwa si mtaaluma katika Uchumi na Uongozi )yanaweza kutumika kama nyenzo na dira kutukwamua kama Wananchi binafsi, jamii na hata Taifa.
  • Kurudisha na kuimarisha Heshima, Utu na Uadhi ya Mwananchi na Taifa la Tanzania
  • Kurudisha na kuimarisha Heshima, Wajibu na Hadhi ya kazi na kufanya kazi kwa Watanzania wote, vijijini na mijini
  • Kuelimisha Wananchi haki zao kama raia, wajibu wao na sehemu yao katika Taifa na Serikali yao kupitia Katiba, Serikali Kuu, Bunge na Mahakama
  • Kuimarisha Ufanisi na Ustawi wa Jamii katika kupiga vita Ujinga, Umasikini, Njaa na Maradhi
  • Kuhakikisha kuwa Katiba, Sheria na Kanuni zilizowekwa zinatekelezeka kutokana na nyakati zilizopo, zinafuatwa ipaswavyo na vyombo vyote husika; Serikali, Bunge, Mahakama na Wananchi wenyewe. Aidha kuweka maamuzi na mipango ya Serikali wazi kwa wananchi wote ili kuhakikisha uadilifu na uwajibikaji wa Serikali haufanyiki kwa siri na na kuwapa wananchi wote haki kwa kuwa wao ndio waliotoa dhamana ya kuwepo kwa Serikali na kuruhusu Uongozi uliopo uongoze nchi
  • Kubuni mbinu za kiuchumi ili kumpunguzia mzigo mwananchi wa kawaida hasa wale wa kipato cha chini na wakulima ili kujenga nguvu kubwa ya taifa kuwa katika Tabaka la kati (middle class)
  • Kuhakikisha kuwa njia kuu za Uchumi na uzalishaji mali zinaboreshwa na kutumika kwa manufaa ya kila Mtanzania na taifa la Tanzania linanufaika kwanza
  • Kuhamasisha na kuhakakisha kuwa Uzalishaji mali (kilimo, viwanda, uvuvi, ufugaji, biashara, madini , utalii, biashara, sanaa, michezo, huduma na maofisini) unafanyika kwa dhatgi, kisayansi, kiushindani, kiuwajibikaji, kiufanisi na kwa ubora wa hali ya juu kwa kutumia tija, kuongezeka kwa juhudi na maarifa ya uzalishaji mali huu
  • Kuhakikisha kuwa huduma za msingi zinaboreshwa na kupewa kipaumbele na kufikishwa kwa wananchi ili kujenga maendeleo ya kweli kwa jamii na Taifa;- Afya, Elimu, Maji safi, Chakula, Uchukuzi na Nishati
  • Kuhakikisha kuwa vita dhidi ya Rushwa, Ubadhirifu, Udini, Ukabila, Uzembe, Ufisadi, Uhujumu, Uvivu, Uzururaji na Kutowajibika au kutokujituma kwa watendaji wa Serikali na taasisi zake (wakuteuliwa au kuchaguliwa), waajiriwa , wafanyakazi na wakulima ni vita vya Taifa zima na linahitaji ushiriki na kushirikisha Wananchi wote. Wananchi wote bila kujali kabila, rangi, jinsia, umri, elimu au mwelekeo wa kisiasa ni wajibu wao kushiriki katika vita hii
Vipengele hivi kumi (10) si vigumu sana kutuumiza kichwa. Ni mambo ya kawaida ambayo tumekuwa nayo lakini kwa miaka karibu 20, tumeondokana nayo na kuishia kuzunguka kama punguani. Tumeshindwa kuwa makini katika Uongozi kitu ambacho kimezalisha uzorotaji na kudumaa kwa uchumi pamoja na takwimu zote zinazosema kuwa uchumi wetu unakua.
Uchumi wa Tanzania utakuwa pale ambapo Mtanzania ataacha kutafuta makombo ili aweze kumaliza siku moja anayoamka akiwa hajui kesho ikoje.

Kutokana na udhoofu wa Uchumi na kuzorota kwa Uongozi, hadhi yetu na kujivunia kwetu kuwa Watanzania kama tulivyozoea kujivuna na kuimba "Tazama ramani utaona nchi nzuri... Nasema kwa kinywa na kufikiri nchi hiyo nzuri ni Tanzania" imeshuka na hatujiamini tena. tumekuwa wanyonge na kukubali kuburuzwa na viongozi wetu na hata wafadhili.

Tunahitaji kujirudishia Uzalendo na hadhi yetu kama Taifa. Tukubali makosa tuliyofanya kwa kukusudia au bila kudhamiria. Hiyo itakuwa hatua ya kwanza ya kutafuta suluhisho la matatizo yetu na kujirudishia hadhi yetu na ya Taifa letu.

Msahafu na maandiko yanasema, "asiyefanya kazi na asile". Watanzania tumesahau nidhamu na wajibu wa kufanya kazi. Tumeendekeza malalamiko na manung'uniko, huku tukipunguza tija na juhudi kulilia motisha. Kama tutageuza nguvu zetu hasi kuhusu uchapaji kazi na kuzifanya chanya kuongeza uzalishaji mali na kuachana na kutegemea misaada, basi nafasi yetu ya kuwa na maendeleo ya kudumu yanayoendelea yatakuwa makubwa na hata viongozi wetu ambao wamekosa dira na mwamko wa kutuongoza wataona aibu tutakapoamka kudai haki zetu kutokana na jasho letu.

Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuangalia Kazi kwa mtazamo wa kimaendeleo na chanya. Bila kufanya kazi, kwa ufanisi, juhudi na uhodari, hatutaweza achana na umasikini na unyonge. Iwe ni mijini kwenye maofisi, biashara, viwandani, mashambani au migodini. iwe kazi za kuajiriwa au kujiajiri, ni lazima tuheshimu kazi na kazi ziwe ni zile halali za kutupa mapato.

Hadhi na utu wa Uzalendo na Utaifa na Taifa letu, vitakuwa havina maana kama Mtanzania hatajua wajibu na haki zake Kikatiba, hatajua na kutumia Sheria na kanuni za nchi kujilinda na kujiongoza. Viapo vyetu vya utii visiishie kuwa ni viapo hewa kwa ajili ya kuapa. Tunapoapa kulitumikia Taifa na kuimba wimbo wetu wa Taifa "Mungu Ibariki.." ni lazima tuwe wakweli na wenye Uzalendo wa kweli ndani ya moyo. Kuelewa haki yetu Kikatiba kutaongeza ufanisi wetu na hasa wajibu wetu kama Raia katika kuweka Sheria za kuilinda nchi yetu na kuwa makini kuchagua viongozi wa kutuongoza kama Taifa.

Wajibu wetu mwingine ni kuhakikisha kuwa kazi yetu haishii katika kulinda katiba na kujua haki zetu kama Watanzania, bali ni kufuata sheria hizo na kuzithamini. Tuwe mstari wa mbele kufuata sheria na kanuni tulizonazo na tuwakosoe na kuwafikisha kwenye sheria wale wote ambao kwa makusudi au bila kukusudia wamekiuka sheria au kanuni. Tusiwaonee haya wale wanaopindisha sheria au kuvunja sheria biola kujali sehemu yao katika jamii. Kama Waziri anapinda Sheria ni wajibu wetu kama jamii kumwajibisha. Kama mbunge anavunja Sheria, ni wajibu kumfikisha mbele ya vyombo vya dola ili haki na hukumu kwa kuvunja Sheria ifanyike.

Sheria na kanuni hazikuwekwa zifuatwe na wananchi pekee. Watawala na Viongozi hawana kinga ya aina yeyote ya kuwaepusha kufuata kanuni,sheria au katiba. Sheria na katiba ziliundwa ili zifuatwe na kila raia na mkazi wa Tanzania.

Wakati wa Azimio la Arusha tulitamka kuwa ili tuendelee tunahitaji Watu, Ardhi, Siasa safi na Uongozi Bora. Tukatamka kuwa tunataka kujenga Taifa huru la Kijamaa na lenye Kujitegemea. Tukasisitiza kuwa vita dhidi ya Ujinga, Umasikini, Njaa na Maradhi vitashinda kama tutatumia Juhudi na Maarifa katika kazi zetu na maisha yetu.

Kazi tuliyonayo sasa si tofauti na ile ya mwaka 1967, ni ile ile na sana sana ni kulenga Nyenzo kuu za maendeleo yetu kama Taifa na kibinafsi kwa kupitia milango miwili. Ili tujikwamue kutoka hali hii mbaya tuliyonayo kama Taifa, ni wajibu wa kila mmoja wetu kuwajibika na kuwa na nia ya kweli kuyafanya yafuatayo;
  1. Kujenga Uchumi imara na madhubuti. Hili litatusaidia katika vita dhidi ya Umasikini, Ujinga, Maradhi na Njaa
  2. Kuwa na Uongozi mahiri na fanisi. Utawala na uongozi wa nchi unahitaji na unategemea Uongozi mahiri kutekeleza sera na mipango, wenye ufanisi kuhamasisha uzalishaji mali na uwajibikaji na wenye kuwa wanyenyekevu na kuheshimu dhamana walizopewa
Uchumi wetu hauwezi kujengeka kwa kutegemea misaada au wawekezaji kutoka nje kuja na kusukuma gurudumu la uzalishaji mali ili kutuongezea kipato. Aidha uchumi wetu hautajengeka kuwa madhubuti kwa kuanzisha mipango mipya au kufanya makosa yaleyale ya kale yaliyofanyika wakati wa Azimio la Arusha, Mipango ya kufufua uchumi 1985-2000 au mipango ya kuchochea Uwekezaji na kuvutia wageni washike hatamu za Uchumi ya 1992-2010.

Uchumi utakaoleta matunda ya kweli na ya maana ni uchumi utakaotokana na juhudi za wananchi katika shughuli zote za uzalishaji mali. Tunahitaji tuwe na mipango inayoeleweka na rahisi kufanikisha safari hii ya kujenga uchumi kwa kutumia mazingira yetu, rasilimali zetu na kwa faida yetu.

Moja ya njia zitakazotumika kuimarisha uchumi ni kubadilisha mfumo wa mapato ya Serikali na kudhibiti matumizi.

Kwa kuanzia, Serikali itabidi kupitia mikataba yote na kuongeza viwango vya kodi na ushuru (taxes, duty and royalties) zinazopatikana kutokana na wazalishaji mali wawekezaji. Kiwango cha asilimia 3% tunachotoza kwa shughuli za uchimbaji madini, gesi, makaa na hata huko mbeleni madini ni kidogo sana. Serikali ifuatilie kwa makini mapato halisi ya makampuni yote yanayojishughulisha na shughuli za uzalishaji mali na kuhakikisha kuwa Serikali inapata malipo ya kweli na yanayowiana na uzalishaji na mapato ya makampuni haya.

Serikali ipitie majedwali na ripoti za mapato ya kifedha (financial statements and bapance sheets) ya makampuni haya katika nchi zilikoandikishwa. Mfano pamoja na kuwa kampuni ya Barrick inatozwa asilimia 3% kama kodi kwa Serikali ya Tanzania, ni ukweli usiofichika kuwa Serikali na taifa la Tanzania linapunjwa. Mpango wangu utahamasisha kuchangua vitabu vya kampuni hii katika soko la mtaji la kimataifa kama NYSE, na kuangalia ni mapato kiasi gani ambayo wameyaorodhesha.

Mapendekezo ya kubadilisha viwango hivi vya mapato ya Serikali yanayotokana na uzalishaji mali wa makampuni mageni na hata enyeji, utahakikisha kuwa misamaha yote ya kodi na ushuru ambayo imetumika kama chambo cha kuvutia uwekezaji na kufanya biashara inafutwa au itapewa kipindi kifupi mno ili kupunguza hujuma na dhuluma. Mapendekezo ya kuongeza mapato yatakuwa ni kuongeza viwango vya kodi za mapato kwa makampuni haya kutoka 3% hadi kufikia 20% katika kipindi cha miaka mitano tangu sheria ianze kutumika.

Umiliki wa sekta za madini, uvuvi, utalii uhakikishe kuwa Watanzania kwa kupitia mashirika ya ndani yanakuwa naUshirika yanakuwa na 40% ya umiliki ili kuhakikisha kuwa Taifa haliendelei kunyonywa. Matarajio ya mpango huu ni kuwa Wawekezaji wenye utu watakubaliana na kufanya kazi na Serikali na Taifa kwa manufaa ya pande zote mbili.

Mapato haya ya kutokana na ongezeko la kodi, ushuru na umiliki yataliongezea Taifa pesa za kuweza kuondokana na misaada na mikopo ambayo imetulemaza na kutufanya kuwa tegemezi na masikini. Kuongezeka kwa mapato kutokana na kodi na ushuru kutapunguza ule mzigo wa Serikali kutegemea mazao ya chakula na biashara katika kupata fedha za uendeshaji. Mapato haya yatakuwa moja ya nyenzo kuu za kujenga uchumi kwa kutumika katika kuboresha sekta za Elimu, Afya, Miundombinu na Nishati.

Itaendelea...

But you re forgetting one thing: the culture of the people. The way how we eat, we work and how we behave is an expression of our culture and this automatically influence our working system and our accountability. For instance; if only Kilimanjaro and Iringa could feed the whole Tanzania and export the surplus to other countries before 1967, and also if Shinyanga, Mwanza, and Tabora could feed the whole Tanzania with meat and export to other countries. Remember that during the colonial period there was a movement of hard workers from place to place. Hard workers moved from more hard work cultured Regions to those lazy regions. These in the modern times are called migrant workers. They moved from to Tanga and Morogoro for Sisal plantations, they moved even to tobbacco growing regions.

Pundits may argue that people from less developed regions moved to make money from the highly paid incomes especially in the coastal cities. But surely that was not the case. The cultures in Coastal areas like Tanga, Pwani (Dar), etc were in different culture; their cultures at that time didn't suit as hard workers.

Our Migrant workers were caught in this cultural shock; with the introduction of religions, and centralization, we found ourselves adapting the assimilation to new cultures. Our cultures in Tanzania are determined from our Dar Es Salaam culture which is dominant. The founder of the nation JKN united us on such a cuklture though he struggled to make it comfortable by all people. But still today we have the same culture that Dar Es Salaam is an index of our culture (Coastal Culture is our index).

JKN corrupted our minds by ideology which made all of us accept Ujamaa. Mali ya umma, etc etc. WE had free education, free medical care and what we paid back was by having more children who will rely from the government handouts. The culture was built on this.

Now what we need today is having another ideology telling people that, we must feed our children, educate them and build our own country; again is culture!

Is really a problem of our time!
 
IO.. umenifanya nikumbuke misemo fulani kama bado ina maana tena..

a...: Kazi ndiyo kipimo cha utu

b...: Kila mwenye uwezo wa kufanya kazi afanye kazi

c...: Kufanya kazi kwa juhudi na maarifa

d....: Nidhamu ya kazi ni msingi wa mafanikio kazini

e....: Migogoro na migongano makazini, ni ukosefu wa nidhamu

f.....: Kazi ndiyo msingi wa maendeleo
 
IO,

Masterplan ya Mchungaji haijaisha. bado tuko kwenye Uchumi, ngwe ya Utawala na Uongozi inakuja usitie shaka, shukrani kwa kuchambua!
 
IO,

Masterplan ya Mchungaji haijaisha. bado tuko kwenye Uchumi, ngwe ya Utawala na Uongozi inakuja usitie shaka, shukrani kwa kuchambua!
Mchungaji,

Je watakusikiliza,watakubeza tu,.Mie nina mpango wa kukata tamaa,wiki hana nilisikia wana mpango wa kujua humu JF ni nani ni nani na huyu ni nani na anafanya shghuli gani.Personal wameshaniumia E-mail..
 
Back
Top Bottom