'Marshall Plan' - Restoration and Recovery Plan for Tanzania

DAR si LAMU

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
2,933
1,500
..rev,

..mpangilio mzuri kabisa wa maoni.

..sasa,ili iwe marshall plan inahitaji projections za mapato na matumizi. pia inahitaji time frame ya utekelezaji na kubainisha wasimamizi,watendaji,wadau,n.k wakuu.

..nadhani wapo wataalamu au na wasomi wa kutosha humu watakao iboresha kadri itakavyowezekana, bit by bit mpaka iive!

nb:tanzania ina viongozi wachache sana, wengi ni wahuni,wezi,wababaishaji na wabinafsi.

..invisible,

..nadhani inawezekana kutengeneza namna ya ku-edit hii "marshall plan". ila kabla haijafanyiwa masahihisho kamili lazima ipitiwe na jopo na kukubalika. halafu,tunaendelea na kazi......

..nitatoa maoni zaidi baada ya kupata muono wako kwenye hili.

..rev,

..kwa ruhusa yako, nawasilisha mawazo yangu.
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,528
2,000
Samahani waungwana, maboksi yalinizidi sikupata nafasi kumalizia vizuri. Itakuwa tayari Jumapili jioni!
 

Ogah

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
6,235
2,000
Dahh Mkuu Rev Kishoka....hii sikuiona hii..........hapa kuna mambo/elimu mazuri sana ya kuweka into practice.......ukishamaliza kazi yako hiyo........wazee waipitie na baada ya kuwa refined...........itabidi kupanga strategies za kui-action hiyo recovery plan......

.....Kudos to you Rev
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,528
2,000
..invisible,

..nadhani inawezekana kutengeneza namna ya ku-edit hii "marshall plan". ila kabla haijafanyiwa masahihisho kamili lazima ipitiwe na jopo na kukubalika. halafu,tunaendelea na kazi......

..nitatoa maoni zaidi baada ya kupata muono wako kwenye hili.

..rev,

..kwa ruhusa yako, nawasilisha mawazo yangu.


Dar si Lamu na wana Jamii kwa ujumla,

Naomba muwe na subira kwanza. Nikisha maliza draft yangu ya awali na kuwasilishwa, ndipo wakati wa mpito na kujadiliana uanze na kisha kama ni refinement ifanyike na mwisho ndipo tamko kuu litoke.

Nimeongelea takriban 50% ya kile nilichopanga kuandika. Sehemu kubwa iliyobakia ni kumalizia mambo ya uchumi na kisha kuongelea masuala ya uongozi. na haitakuwa haki kwangu na wengine na sahihi ikiwa sijamaliza kazi niachie wengine wajaze mapengo kwa kudhani lengo limekamilika.

Huko kutakuwa ni kufeli kama CCM na Serikali ya Tanzania!
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,528
2,000
Sijafanya uungwana kwa kushindwa kuwashukuru kwa msukumo mnaonipa na kubaini kuwa hili linawezekana na mnasubiri kwa hamu kubwa.

Nawashukuruni nyote kwa mawazo, maoni na hata maswali magumu.

Niliamua kuanza kuwamegea kidogo kidogo ili niweze kupata wakati kuyarudia niliyoyaandika kwa kusoma maoni na reaction zenu.

Jambo hili si dogo na rahisi, ni gumu na lahitaji muda kufikiri, kuhusisha kila mtu na zaidi ni kulifanya liwe jepesi na rahisi kueleweka na kuweza kumuhamasisha Mtanzania na kumshawishi asikate tamaa, ila atumie busara na ukunjufu katika maamuzi ya Maendeleo yake na vizazi vyake.

narudia tena kuwaomba radhi wote kwa kushindwa kuimaliza kazi hii katika muda niliotarajia kumaliza na zaidi kushindwa kuwashukuru kwa dhati kwa uchangiaji wenu.

Tunataka kulijenga upya Taifa letu, matokeo ya kazi yetu inawezekana tusiyaone ila watoto, wajukuu na vijukuu ndio watakaoneemeka, kufarijika na kunufaika.

Si kwamba Baba na Babu zetu walishindwa kazi, bali wao walikuwa ni wageni mno katika mambo mengi ya ulimwengu wa sasa ambao si wa kijima tena. Zaidi ni ile tabia mbaya iliyojengeka mara baada ya kupata Uhuru ya kutegeana ni nani afanye kazi au afikirie. Waliungana kwa nguvu, mali na maarifa kumngoa mkoloni. wakajisahau na kufikiri kazi imekwisha baada ya Taifa kuwa huru.

Hilo ndilo kosa liliotoa mwanya kwa wachache kujifanyia mambo wanavyotaka na kuishia kuharibu dira ya maendeleo yetu.

Nafasi ni yetu, kulijenga upya Taifa letu tukitumia nguzo kuu ya Umoja, Amani na Mshikamano kulifikisha gurudumu la maendeleo kwenye tambarare.
 

MiratKad

JF-Expert Member
May 2, 2008
294
170
Rev. Kishoka, mawazo mazuri, kazi nzuri, Asante sana! Tunasubiri ukamilishe huo mtazamo...
 

MiratKad

JF-Expert Member
May 2, 2008
294
170
Mkuu Rev. Kishoka,
Maisha ya Mdanganyika hayatazami mbali zaidi ya riziki ya tumbo yaani SHIBE.. mtu mwenye njaa ama kiu cha maji mshikaji fikra zake kwanza ni kuondoa adha hiyo....
Hapa JF ni kundi ambalo tumebanwa haja kubwa na ndogo kwa mpigo..Tunahitaji kushusha mzigo huu kwanza kabla hatujafikiria vizuri mlo unaofuata, lakini sii wachovu wa mbinu za kutafuta kula!
Sasa unapokutana na makundi kama haya yaani wenye njaa kali na sisi ambao tunataka kushusha mzigo, vipaumbele vinagongana...Huu ni upande wa wananchi...safari ni ndefu mkuu kuwaweka watu hawa kitako wakapata kukuelewa... ndio maana unaona Bungeni wawakilishi wetu (walioshiba) huuchapa usingizi tu.. wafanyeje!..

Ndio inabidi watanzania waelimishwe na mambo yaendeshwe sambamba. Kutatua tatizo la shibe na hilo la ujinga.

Manake ukishikilia kuwa kuna vipaumbele vinagongana tuuu, watachelewa na wataendelea kuumia kwa muda mrefu zaidi. Kuna wengine hata huwa wanasema Afrika haihitaji teknolojia wanahitaji chakula!!? Angalia sasa mafanikio ya Simu na Intaneti....
 

MiratKad

JF-Expert Member
May 2, 2008
294
170
..rev,

..mpangilio mzuri kabisa wa maoni.

..sasa,ili iwe marshall plan inahitaji projections za mapato na matumizi. pia inahitaji time frame ya utekelezaji na kubainisha wasimamizi,watendaji,wadau,n.k wakuu.

..nadhani wapo wataalamu au na wasomi wa kutosha humu watakao iboresha kadri itakavyowezekana, bit by bit mpaka iive!

nb:tanzania ina viongozi wachache sana, wengi ni wahuni,wezi,wababaishaji na wabinafsi.

Hapa ndio mzizi wa matatizo mengi ya Afrika kwa ujumla na hususani Tanzania. Lazima vita kali ya ubadilishwaji wa katiba itangazwe. Infact, hata pendekezo la serikali ya mseto kuundwa bila kujali nani kashinda.
 

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,535
2,000
Miratkad,
Kazi ya kuwaelelimisha Wadanganyika nadhani imefikia mahala tusimame na kuanza kujipanga upya namna ya kuwaelimisha hawa watu kwa vitendo yaani kama ni darasa wakati wa theory umepita sasa ni Practical.. na ndivyo Rev Kishoka anachojaribu kuweka mikakati hapa sii somo tena na darasani ila tunaingia hatua nyingine..
Sasa basi ktk hatua hiyo ni muhimu sana tufahamu mazingira tuliyokuwa nayo -ARDHI na Watu wake..
Marshall Plan inayotayarishwa hapa imetazama sana upande wa ARDHI, SIASA na UONGOZI BORA, hivyo nimeongeza kipengele kidogo kinachotupa mwamko zaidi kuelewa hii Marshall Plan imekusudiwa WATU gani na wapo ktk hali gani..Trust me usipowaangalia WATU hata siku moja huwezi kukamilisha kitu..Hata benki wanapomsaidia mtu huangalia credit ya huyo mtu, yaani anatazamwa mtu sio biashara anayotaka kuingia ama mfumo wa biashara nchini. Kumbuka tu linalowezekana kwa babu Juma haina maana hata Achuman itawezekana....
Mkuu ogopa sana maskini kwanza haaminiki inapofikia swala la tumbo, tumeona hao walimu wakikopa fedha toka kwa mama Mkapa ktk masharti magumu sana.. swala ambalo haliingi akilini kabisa, sasa ni vigumu sana kuwaambia watu kama hawa ahead of time kuwa mikopo kama hiyo haifai, watakuona mchawi tu hadi wao wenyewe waingie wajaribu kisha wanaposikia maumivu ndio huanza kulialia na kutafuta mchawi..Hata siku moja kosa haliwezi kuwa lao ndio jeuri ya maskini.
Nimeyaona hapa JF kwa sana hasa baadhi ya watu wanaovamia kijiwe hiki.. Hutetea jambo wasilolifahamu hadi mishipa kuwavimba lakini siku kinapowawasha wao hushindwa hata kuomba samahani kwa makosa yao bali hutazama nje kumtafuta mchawi..
Chaguzi ziliopita ni mfano mzuri sana toka Mkapa hadi Kikwete ni hadithi ambayo huwezi kumwambia Mdanganyika kabla hajaumia.. wasingekuelewa kabisa ukisema Mkapa hafai au Kikwete wakati wanasikia harufu ya Pilau..lakini leo hii baada ya kuumia ndio kwanza unasikia vilio kila kona..
Kwa hiyo mkuu tujiandae na kila masahihisho mtakayo yafanya..Mikakati yote ni lazima itazame wananchi walengwa na jinsi ya kuwalinda ama kuwa push wafanye yale wao wanaona hayawezekani..
Ni Udikteta kusema kwamba wakati umefika kwa sisi wananchi wenye kuona mbali kuchukua hatua ambazo hazina Ushabiki wala dhana isipokuwa kile kinachoweza kujenga nchi yetu..
Kwa maana hiyo nasema hivi ni wakati wa wananchi kutupa yale magongo ya kutembelea..marshall Plan iwe ni taratibu za kumwezesha Mdanganyika kuamini kwamba hahitaji magongo na msukumo wetu ni lazima tufahamu kwamba huyu Mdanganyika hana imani kama anaweza kutembea bila magongo.. Utaratibu wa Mama cheza ni lazima ufanyike hata kama kuna maumivu makali.. ponya ni lazima pamoja na kwamba vipaumbele vinatofautiana...
Malengo yetu ama tunachotafuta sisi wote ni kuhakikisha Uzima wa mgonjwa huyu -MDANGANYIKA..
 

MiratKad

JF-Expert Member
May 2, 2008
294
170
Miratkad,
Kazi ya kuwaelelimisha Wadanganyika nadhani imefikia mahala tusimame na kuanza kujipanga upya namna ya kuwaelimisha hawa watu kwa vitendo yaani kama ni darasa wakati wa theory umepita sasa ni Practical.. na ndivyo Rev Kishoka anachojaribu kuweka mikakati hapa sii somo tena na darasani ila tunaingia hatua nyingine..
Sasa basi ktk hatua hiyo ni muhimu sana tufahamu mazingira tuliyokuwa nayo -ARDHI na Watu wake..
Marshall Plan inayotayarishwa hapa imetazama sana upande wa ARDHI, SIASA na UONGOZI BORA, hivyo nimeongeza kipengele kidogo kinachotupa mwamko zaidi kuelewa hii Marshall Plan imekusudiwa WATU gani na wapo ktk hali gani..Trust me usipowaangalia WATU hata siku moja huwezi kukamilisha kitu..Hata benki wanapomsaidia mtu huangalia credit ya huyo mtu, yaani anatazamwa mtu sio biashara anayotaka kuingia ama mfumo wa biashara nchini. Kumbuka tu linalowezekana kwa babu Juma haina maana hata Achuman itawezekana....
Mkuu ogopa sana maskini kwanza haaminiki inapofikia swala la tumbo, tumeona hao walimu wakikopa fedha toka kwa mama Mkapa ktk masharti magumu sana.. swala ambalo haliingi akilini kabisa, sasa ni vigumu sana kuwaambia watu kama hawa ahead of time kuwa mikopo kama hiyo haifai, watakuona mchawi tu hadi wao wenyewe waingie wajaribu kisha wanaposikia maumivu ndio huanza kulialia na kutafuta mchawi..Hata siku moja kosa haliwezi kuwa lao ndio jeuri ya maskini.
Nimeyaona hapa JF kwa sana hasa baadhi ya watu wanaovamia kijiwe hiki.. Hutetea jambo wasilolifahamu hadi mishipa kuwavimba lakini siku kinapowawasha wao hushindwa hata kuomba samahani kwa makosa yao bali hutazama nje kumtafuta mchawi..
Chaguzi ziliopita ni mfano mzuri sana toka Mkapa hadi Kikwete ni hadithi ambayo huwezi kumwambia Mdanganyika kabla hajaumia.. wasingekuelewa kabisa ukisema Mkapa hafai au Kikwete wakati wanasikia harufu ya Pilau..lakini leo hii baada ya kuumia ndio kwanza unasikia vilio kila kona..
Kwa hiyo mkuu tujiandae na kila masahihisho mtakayo yafanya..Mikakati yote ni lazima itazame wananchi walengwa na jinsi ya kuwalinda ama kuwa push wafanye yale wao wanaona hayawezekani..
Ni Udikteta kusema kwamba wakati umefika kwa sisi wananchi wenye kuona mbali kuchukua hatua ambazo hazina Ushabiki wala dhana isipokuwa kile kinachoweza kujenga nchi yetu..
Kwa maana hiyo nasema hivi ni wakati wa wananchi kutupa yale magongo ya kutembelea..marshall Plan iwe ni taratibu za kumwezesha Mdanganyika kuamini kwamba hahitaji magongo na msukumo wetu ni lazima tufahamu kwamba huyu Mdanganyika hana imani kama anaweza kutembea bila magongo.. Utaratibu wa Mama cheza ni lazima ufanyike hata kama kuna maumivu makali.. ponya ni lazima pamoja na kwamba vipaumbele vinatofautiana...
Malengo yetu ama tunachotafuta sisi wote ni kuhakikisha Uzima wa mgonjwa huyu -MDANGANYIKA..

Mkuu Mkandara,

Nimekupata barabara. Kuna jamaa yangu mwingine tulijaribu kuzungumzia suala hili la wadanganyika kuwa wadanganyika kirahisi kiasi hiki na alitoa sababu zinazolingana sana na zako. Sasa kwa kiasi kibubwa nimewaelewa wakuu.

Ninaisubiri kwa hamu hii Marshal Plan. Tutaweza kuigawanya katika mafungu madogo madogo ambayo yatatekelezeka tu. Impossible is nothing.
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,989
2,000
Hawa ndio hatuwataki! angalia matumbo yao, hivi kweli wanatokea vijiji gani? Huko wilayani mwao Utapiamlo na Kwashiakor ni kiasi gani? maana kama Mbunge amenona kiasi hiki, basi hata Wananchi wa jimbo lake wana NEEMA!

attachment.php

Duh!! ebana hii kali....hivi ni kina nani hawa? Nahisi kama ni wabunge flani hivi lakini ningependa kujua majina yao....manake wamevimba si kidogo
 

DAR si LAMU

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
2,933
1,500
Dar si Lamu na wana Jamii kwa ujumla,

Naomba muwe na subira kwanza. Nikisha maliza draft yangu ya awali na kuwasilishwa, ndipo wakati wa mpito na kujadiliana uanze na kisha kama ni refinement ifanyike na mwisho ndipo tamko kuu litoke.

Nimeongelea takriban 50% ya kile nilichopanga kuandika. Sehemu kubwa iliyobakia ni kumalizia mambo ya uchumi na kisha kuongelea masuala ya uongozi. na haitakuwa haki kwangu na wengine na sahihi ikiwa sijamaliza kazi niachie wengine wajaze mapengo kwa kudhani lengo limekamilika.

Huko kutakuwa ni kufeli kama CCM na Serikali ya Tanzania!


..bila shaka, maalim!
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,528
2,000
Waungwana,

Naombeni cofta ya vidole kama ipo! Nimemaliza kazi na kwa kweli ilikuwa ni kazi ngumu.

Waraka ni mrefu kurasa 26!

Nimepata shida ku-attach waraka mzima, hivyo nitautuma kwa wenye utaaalamu ili uweze kuwekwa hapa ukumbini. Ikiwa unahitaji nakala origino, nitumie email yako kupitia PM, nami nitakupelekea nakala.

Mtiririko umebadilika kidogo na jinsi nilivyouleta hapa. Namalizia kuandika hapa kwenye thread kwa kubandika maoni yangu kuhusu uongozi.
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,528
2,000
inaendelea....

Uongozi; Serikali, Utawala, Dola
Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) zimebahatika kuwa na awamu si chini ya nne za uongozi wa Serikali kuu, ingawa kwenye Bunge na Mahakama, watumishi wake wameendela kuwa ni wale wale kwa muda mrefu.

Tatizo kubwa tulilonalo kama Taifa ni ufinyu wa viongozi bora na utashi binafsi wa wachache walio katika nyanja za uongozi kwa kukosa sifa muhimu kwa viongozi. Mzee Mwinyi amesema majuzi kuwa Tanzania ina viongozi wasomi wasioelimika. Kauli hii ni ya kweli na ni ya msingi kutambua kuwa uongozi si lelemama, ni kipaji na ni kazi ngumu.

Uongozi ni kujitolea na kuweka matwakwa na maslahi ya wengine kuwa mstari wa mbele na si matakwa binafsi na kujinufaisha. Marehemu John Kennedy rais wa Marekani alitoa kauli moja maarufu iliyosema kuwa "kiongozi ajiulize ni vipi atalitumikia Taifa na si Taifa kumtumikia yeye Kiongozi" Umashuhuri na uzuri wa Kiongozi unatokana na hekima, busara, uchapakazi, ufanisi, ufuatiliaji, uimara, uungwana, uwajibikaji na unyenyekevu wake. Ama fikra endelevu na upeo wa kuongoza ni muhimu na si kauli tamu au uzuri wa sura.

Uwezo wa Tanzania kuwa na maendeleo ya kweli utaanza na Uongozi bora.

Uongozi bora ni ule;
· wenye mapenzi ya kweli na dhati na kujivunia Utaifa wake
· wenye kujali na kulinda maslahi ya Taifa lake na watu wake
· wenye uwezo wa kupanda mbegu imara ya Uzalendo kwa kila mwananchi bila kujali itikadi, rangi, kabila, dini, elimu, umri au jinsia
· wenye uwezo wa kuhamasisha na kuchochea juhudi za maendeleo ya jamii, umma na Taifa
· wenye nidhamu, watiifu, kuwajibika, tija, ufanisi, kujituma na ufuatiliaji wa hali ya juu
· wenye usikivu, uungwana na unyenyekevu kukiri makosa, kukubali kukosolewa na kupokea na kufanyia kazi maoni ya wengine
· wenye uwezo wa kufanya kazi, kufikiri, kuwa na upeo na wepesi wa kukabili na kufanya maamuzi magumu
· usiolea uzembe, ubaguzi, unyanyasaji, uhujumu, ubadhirifu, rushwa, kudharau, kudhalilisha, kujuana au kulinda maslahi ya wachache au kikundi Fulani

Wajibu wetu kama Taifa na haki yetu kama wapiga kura kuchagua viongozi kutuongoza unabidi uachane na mfumo duni tulioujenga wa kuangalia sura na chama na tuangalie wagombea wetu wa uongozi kwa vigezo hivyohapo juu ili kuunda tabaka jipya la viongozi ambao ni wachapakazi na watakuwa manahodha wazuri kutuongoza katika safari yetu ya kulijenga Taifa.

Tukilegalega katika hili na kupuuzia wajibu juu mkubwa na kuendelea kuchagua viongozi na wawakilishi wabovu, tutakuwa hatuna sababu yeyote kulia na kulalamika kuwa tu masikini au wanyonge kwa kuwa ni Ujinga na Upumbavu wetu kutumia akili na busara zetu tulizopewa Mungu tumekimbilia kurudia makosa ya kuwapa dhamana ya uongozi watu ambao hawafai kutuongoza.

Tuchague viongozi si kwa kuangalia vyama au sura, bali tuangalie uwezo wao wa kuongoza, kuhamasisha na kufanya kazi. Tupime kauli zao na matokeo ya kazi zao kama wanavyojinadi.
Serikali ni watu, inaundwa na watu tuliowachagua na tunawapa watu hawa na Serikali mamlaka makubwa ya kutuongoza, kupanga na kulinda Taifa na Katiba yetu. Dhamana hii imefanywa kwa kuaminiana kuwa Serikali itafanya kazi kwa manufaa ya Wananchi wake na kwa matakwa na utashi wa Wananchi wake.

Inapotokea kuwa Serikali inafanya kazi tofauti na dhamana iliyopewa, ni wajibu na haki ya kila Mwananchi kudai na kuhoji mapungufu yanayoonekana au kuzungumzwa. Ni wajibu wa Serikali na Uongozi kujibu na kuwajibika kwa Wananchi waliowapa dhamana ya kuongoza Taifa.
Ikiwa Serikali na watendaji wake na Viongozi wanashindwa kufanya kazi zao kama wanavyotegemewa kuzifanya na kushindwa kutimiza matarajio ya Wananchi na Taifa, ni wazi kuna umuhimu wa kupima uwezo wa viongozi na kuhoji Uzalendo wao na kama bado wanastahili kulitumikia Taifa.

Kuanzia Rais, Mawaziri, Majaji, Mahakimu, Wabunge, Wakuu wa Taasisi na Mashirika, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Polisi, Magereza,Jeshi na watendaji wengine wa Serikali, tumaini la Watanzania na Taifa ni kuwa watu hawa wamepewa nafasi hizo kwa kuwa wanauwezo wa kitaaluma na kiutendaji kuwa viongozi na walinzi wa nguzo za Taifa letu kupitia Katiba na Sheria zake.
Hivyo basi pamoja na kuwa ni jukumu la sisi kama Raia na Taifa kudai uwajibikaji, lakini uzito wa kuhakikisha ufanisi wa Uongozi na uwajibikaji wake utaanzia na Mkuu wa Nchi ambaye ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu.

Wasifu wa Uongozi bora nilioutaja hapo juu, si wa Rais pekee, ni wa kila mtu aliye kiongozi na ni shurti kila Mtanzania aishi kwa kuviangalia na kuvitumikia vipengele hivyo bila kujali yeye ni Kiongozi au la.

Serikali yetu ni kubwa sana na ina watendaji wengi ambao sitaficha kusema kuwa asilimia 55% hawastahili kuwa viongozi kutokana na kushindwa kuwa na sifa nilizozitaja hapo juu.

Hii ni hatari sana kwa Maendeleo na Usalama wa Taifa letu. Hatuwezi kuendelea kujiongoza kiholela huku zaidi ya nusu ya viongozi wetu hawana Uzalendo au uchungu na nchi yao. Swali kwako Mtanzania ni kwa nini basi ukubali kuendelea kujichagulia viongozi wabovu wasiofaa na kuwapa dhamana kubwa sawa na kumpa Simba jukumu la kulinda Mbuzi wako?

Kinachokosekana kutoka Uongozi Mkuu hasa Urais na hata Mawaziri ni uwezo wa kudai kwa nguvu uwajibikaji na uadilifu. Hadithi na tuhuma za ufisadi zilizotawala Taifa letu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 ni kutokana na kuwa na Uongozi dhaifu, usiojali maslahi ya Taifa, uongozi uliojaa woga na kulindana na kushindwa kusimama kidete kulinda rasilimali za Taifa letu.

Viongozi wakuu wa jamii kuanzia wakuu wa vijiji, kata, tarafa, wilaya, mikoa hata Taifa, wameendelea kufanya kazi bila kupimwa na waajiri wao wawe Wananchi au Serikali kuu kuhusiana na ufanisi na uwezo wao katika safari ya kulijenga Taifa na kuleta maendeleo.

Mapendekezo yangu ambayo yataanzia na wewe Mtanzania ni kuwapima viongozi wako kwa kutumia vipimo vyepesi sana. Vipimo hivi ni kama ifuatavyo;
· kupitia ripoti za kila mwezi, robo, nusu na mwaka mzima za maendeleo na kupima mafanikio na matatizo ya shughuli za maendeleo
· kuhoji na kuhakiki viwango vya kuongezeka vita dhidi ya ujinga katika wilaya au mikoa kupitia shule za msingi, sekondari, vyuo na elimu ya watu wazima
· kuhoji maendeleo ya afya kupiga vita maradhi, kuangalia takwimu za kupungua vifo vya Uzazi, vifo vya watoto, kupungua kwa uadimu wa lishe na magunjwa kama Kwashiakor, Utapiamlo, kupungua kwa magonjwa na vifo vya Malaria na Ukimwi
· ongezeko la nyumba bora, maji safi, barabara nzuri, shule, hospitali na zahanati, vyanzo vya ajira, viwanda na shughuli za kilimo
· hifadhi za chakula kukabiliana na njaa, mauzo ya mazao ya biashara na chakula
· matumizi bora ya fedha za bajeti ikiwa pamoja na kubana matumizi yasiyo ya muhimu, kudhibiti matumizi na mahesabu ya fedha za bajeti za matumizi na maendeleo
· kukagua na kuhakiki shughuli za maendeleo kuwa ni endelevu na kuhakikisha hazizoroti

Kwa kifupi ni kuhoji na kutathmini, ni shule ngapi tulizonazo, ni ngapi zimeongezeka, ni wanafunzi wangapi wamehitimu shule, ni hospitali ngapi tulizonazo zina uwezo gani, msisitizo wa kinga ni mkubwa kiasi gani kulingana na tiba, kuongezeka kwa shughuli za uzalishaji mali na hifadhi za mazao, kubana matumizi na matumizi mazuri ya fedha.

Nimeweka wajibu huu kwako wewe mwananchi kwanza na si ile kasumba ya kusubiri Kiongozi Mkuu-Rais au Waziri Mkuu ndio wawe wenye jukumu na uhalali wa kuhoji haya.
Vipimo hivi haviishii kwa Mbunge, Mkuu wa Wilaya au Mkoa ni mpaka kwenye Serikali kuu na hata vigezo hivi vinaweza tumika katika mashirika na taasisi za umma na zile binafsi.

Kama vigezo hivi vya uongozi bora na kupima uwajibikaji vingekuwa vikifuatwa kwa makini, tungeweza kuona uwiano wa maendeleo wa Taifa letu. Lakini ni mpaka pale tutakaboshinikiza na kudai kwa nguvu Utawala na uongozi bora, ndipo tutakapoona mafanikio na hivyo kuanza kupata tumaini la maendeleo ya Taifa zima.

Uongozi na Utawala bora huendana sambamba na dola. Katika Utawala bora, Serikali na Viongozi ni wabunifu wa mipango mizuri ya maendeleo, ni wapimaji wa kasi ya maendeleo na hufuata kanuni na sheria katika kufanya kazi zao.

Panapokuwa na Uongozi na Utawala mzuri, kero za wananchi hupungua na hata matumizi ya dola na vyombo vyake huheshimika na huwa ni kwa ajili ya manufaa ya Taifa.
Hali halisi ya Tanzania imejenga mfumo wa utawala unaolinda utashi na maslahi ya chama tawala au kikundi chenye nguvu za madaraka nja mali. Hali hii imefikia hatua ya kikundi hiki cha watawala kutumia nguvu za dola kutawala kwa mabavu, kukiuka sheria na kanuni alimradi wanatumia kinga ya uongozi.

Utawala wa namna hii si mzuri na hauna manufaa hata kidogo kwa nchi yetu au Taifa lolote. Tunapaswa kukemea na kuondokana na mfumo huu mbovu wa Utawala ambao unatumia dola na kuweka wajibu wa kwanza wa Uongozi ni kulinda matakwa ya Chama au kikundi maalum.
Aidha matumizi mabovu ya dola na vyombo vyake, Bunge, Mahakama, Polisi, Jeshi na Usalama wa Taifa yamesababisha kwa kiwango kikubwa kuzorota kwa Uongozi, kuweko kwa utawala mbovu ambao umeishia kuangamiza uchumi na juhudi za maendeleo ya Taifa.

Wajibu wa vyombo kama Bunge na Mahakama ni kuwa mihimili mingine ya Serikali. Bunge likitunga Sheria, Mahakama ikitoa tafsiri za sheria na Serikali kuu kufanyia kazi sheria. Badala ya vyombo hivi kuwa huru na hata kuhakiksha vyombo visaidizi kama Polisi, Jeshi, Mahakama, Magereza, Usalama wa Taifa na ofisi ya Mwanasheria Mkuu vinabakia kuwa vyombu huru ndani ya mfumo wa kisiasa, vyombo hivi vimegeuzwa na kutumika kama silaha ya kulinda chama kinachotawala kwa kutoa vitisho kwa wananchi na vyama visivyo na madaraka.

Suluhisho la haya yote ni kuundwa kwa Katiba mpya na Sheria mpya ambazo zitalenga;
· kutoa haki sawa kwa kila mwananchi bila upendeleo
· kutofungamana na chama au kikundi cha siasa au watawala,
· kuwajibisha Watanzania wote bila kujali nafasi zao katika jamii na Taifa,
· kulinda maslahi, haki , uhuru na mali za Watanzania wote bila kujali itikadi, dini, elimu, jinsia, umri au kabila
· kutoa tafsiri na maelezo ya kisheria na kanuni ambayo hayana utata au kukosa nguvu kufanyiwa kazi na kufuatiliwa
· kumpa kila Mtanzania fursa na haki sawa katika kuchangia kwake ujenzi wa Taifa na hata kuongoza bila kuwa na vipingamizi vya kibaguzi ambavyo vimewekwa maksudi katika katiba ya sasa na Sheria kuzuia ushindani au kuwepo kwa uhuru kamili wa kujieleza na kufanya mambo ya siasa na uongozi
· kujenga miiko mikali na maadili kwa viongozi, utawala na wanachi kwa ujumla
· kuweka mfumo bora wa uteuzi au uchaguzi wa viongozi na wawakilishi

Penye nia pana njia, kama wote tutakaa mstari mmoja na kukubaliana kwa pamoja kuwa haya ndiyo tunayoyataka kutoka kwa viongozi wetu, mfumo wetu wa utawala na dola, nafasi ya kupata viongozi wazuri, kuwa na mipango mizuri itafanikiwa na hivyo kuruhusu wananchi na viongozi kuwajibika kwa dhati na kujituma ili kuhakikisha kuwa shughuli za Ujenzi wa Taifa kiuchumi unafanikiwa kukiwa na Amani, Mshikamano, Sheria na Uongozi Bora.

mwisho....
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,528
2,000
Nimeweza kubadilisha faili, pokeeni waraka wa mchungaji. Tatizo lilikuwa natumia Office 2007 na JF haikubali format ya word 2007. Ikabidi nibadilishe kuwa word 97-03!
 

Attachments

  • File size
    127.5 KB
    Views
    58

Mtuwamungu

Senior Member
Jun 21, 2007
110
195
AMEN!

Mchungaji,

Pongezi kwa kazi nzuri na makini. Umeonyesha njia. Mwenyezi Mungu akinipa nguvu, afya njema, uwezo, na nafasi nitajaribu kuchangia mawili matatu katika hoja hii muhimu. Ngoja nitafakari kwanza.

Ubarikiwe!
 

Bibi Ntilie

JF-Expert Member
May 30, 2008
245
0
Mchungaji,
Uzee umenizidi, leo ndio nimeiona hii thread! Kwa kweli nimefurahi mno kuona kwamba umeweza kuketi chini na kututengenezea kitu kizuri kama hiki!

Sasa nasema hivi, lini utarudi nyumbani na kugombea uongozi ili tukuunge mkono kabla bwana God hajatuita?

Aidha, natoa changamoto kwa nyie vijana na wazee wenye kuunga mkono mawazo mazuri kama haya, na wale wote ambao mmekuwa mkitoa michango ya 'kimapinduzi' yenye dhamira ya kuliokoa taifa letu linaloelekea kusikoeleweka. Jana wakati namsikiliza Kubenea na leo niliposoma hii thread nikajua nchini tunao vijana wanaoweza kuliokoa Taifa letu endapo utakuwepo mshikamano wa dhati.

Tatizo lenu humu ndani kila mtu ana chama chake anachoshabikia! Mie ningeshauri muachane na vyama vilivyopo, unganeni kwa mawazo mazuri na dhamira ya kutaka kulikomboa Taifa letu. Wekeni mikakati na ikibidi anzisheni chama kipya kabisa chenye lengo la kuinusuru nchi. Mtaungwa mkono na wengi.
 

Kuhani

JF-Expert Member
Apr 2, 2008
2,944
1,195
Serikali pia inabidi kuachana biashara ya kuwa “wenye nyumba” au Teksi.

Ukiondoa Raisi, Makamu wa Raisi, Waziri Mkuu, Spika, Jaji Mkuu, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Wakuu wa majeshi ya Ulinzi na Polisi, viongozi wengine wote wa Serikali, majaji, mahakimu, makatibu wakuu, wakurugenzi, wakuu wa wilaya , wabunge na wengineo wote, watabidi waingie gharama kutokana na mishahara yao kulipia gharama za nyumba na usafiri wao kwenda na kutoka kazini. Serikali inaingia gharama kubwa kutunza nyumba hizi na magari ambazo si za muhimu. Dhana ya kuufuma na kupata kila kitu kwa bure inabidi iishe. Serikali ipunguze madaraja ya Watendaji wake ambao wanastahili kupewa na kuishi katika nyumba za serikali na kutumia magari ya Serikali.

Ndio maana Mkapa aliamua kuuza nyumba za Serikali.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom