Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,528
Waraka wa Mchungaji kwa Watanzania
Ndugu Mtanzania,
Naomba kuwasilisha kwako waraka huu ukiwa ni mwamsho na na hamasa kwetu kama Wananchi na Taifa ili kulikwamua taifa letu kutoka katika hali mbaya ya kiuchumi tuliyonayo inayoenda sambamba na kuzorota kwa Uongozi na Utawala bora.
Matatizo ya Tanzania yamegawanyika katika makundi makubwa mawili ambayo ukiangalia kwa kina, yanaoana na kila moja kinategemea mwenziwe. Matatizo haya ni Uchumi (Umasikini, Ujinga na Maradhi) na Uongozi (Utawala holela, Uzembe, Rushwa, Uvivu, uwajibikaji).
Naomba upokee waraka huu kupima nafsi yako na wale watakao kuja kwako kuomba kura yako wakati wa uchaguzi, uwe ni wa Serikali ya Mitaa, Wabunge au Urais. Nakusihi utumie mwamko na hamasisho hili kujihoji nafsi kuwa wewe binafsi una nafasi gani na nguvu zako zina nafasi gani ili kuleta msukumo utakaoleta maendeleo ya kweli na kulikwamua Taifa kutoka kwenye shida zinazotuzingira na kutudumaza. Kutumia waraka huu, jiulize kwa makini ni nini maana ya Maendeleo na ni maendeleo ya namna gani Watanzania wanayataka na yatawasaidia vipi wao na vitukuu vyao.
Miaka 9 iliyopita niliandika haya yafuatayo hapa chini kama ningekuwa mgombea Uchagusi Mkuu 2000. Nayarudia tena kwa kuwa ni katika haya kumi (10) ndivyo Mipango ya Maendeleo kwa mujibu wa mawazo na maoni ya Mchungaji (pamoja na kuwa si mtaaluma katika Uchumi na Uongozi )yanaweza kutumika kama nyenzo na dira kutukwamua kama Wananchi binafsi, jamii na hata Taifa.
Uchumi wa Tanzania utakuwa pale ambapo Mtanzania ataacha kutafuta makombo ili aweze kumaliza siku moja anayoamka akiwa hajui kesho ikoje.
Kutokana na udhoofu wa Uchumi na kuzorota kwa Uongozi, hadhi yetu na kujivunia kwetu kuwa Watanzania kama tulivyozoea kujivuna na kuimba "Tazama ramani utaona nchi nzuri... Nasema kwa kinywa na kufikiri nchi hiyo nzuri ni Tanzania" imeshuka na hatujiamini tena. tumekuwa wanyonge na kukubali kuburuzwa na viongozi wetu na hata wafadhili.
Tunahitaji kujirudishia Uzalendo na hadhi yetu kama Taifa. Tukubali makosa tuliyofanya kwa kukusudia au bila kudhamiria. Hiyo itakuwa hatua ya kwanza ya kutafuta suluhisho la matatizo yetu na kujirudishia hadhi yetu na ya Taifa letu.
Msahafu na maandiko yanasema, "asiyefanya kazi na asile". Watanzania tumesahau nidhamu na wajibu wa kufanya kazi. Tumeendekeza malalamiko na manung'uniko, huku tukipunguza tija na juhudi kulilia motisha. Kama tutageuza nguvu zetu hasi kuhusu uchapaji kazi na kuzifanya chanya kuongeza uzalishaji mali na kuachana na kutegemea misaada, basi nafasi yetu ya kuwa na maendeleo ya kudumu yanayoendelea yatakuwa makubwa na hata viongozi wetu ambao wamekosa dira na mwamko wa kutuongoza wataona aibu tutakapoamka kudai haki zetu kutokana na jasho letu.
Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuangalia Kazi kwa mtazamo wa kimaendeleo na chanya. Bila kufanya kazi, kwa ufanisi, juhudi na uhodari, hatutaweza achana na umasikini na unyonge. Iwe ni mijini kwenye maofisi, biashara, viwandani, mashambani au migodini. iwe kazi za kuajiriwa au kujiajiri, ni lazima tuheshimu kazi na kazi ziwe ni zile halali za kutupa mapato.
Hadhi na utu wa Uzalendo na Utaifa na Taifa letu, vitakuwa havina maana kama Mtanzania hatajua wajibu na haki zake Kikatiba, hatajua na kutumia Sheria na kanuni za nchi kujilinda na kujiongoza. Viapo vyetu vya utii visiishie kuwa ni viapo hewa kwa ajili ya kuapa. Tunapoapa kulitumikia Taifa na kuimba wimbo wetu wa Taifa "Mungu Ibariki.." ni lazima tuwe wakweli na wenye Uzalendo wa kweli ndani ya moyo. Kuelewa haki yetu Kikatiba kutaongeza ufanisi wetu na hasa wajibu wetu kama Raia katika kuweka Sheria za kuilinda nchi yetu na kuwa makini kuchagua viongozi wa kutuongoza kama Taifa.
Wajibu wetu mwingine ni kuhakikisha kuwa kazi yetu haishii katika kulinda katiba na kujua haki zetu kama Watanzania, bali ni kufuata sheria hizo na kuzithamini. Tuwe mstari wa mbele kufuata sheria na kanuni tulizonazo na tuwakosoe na kuwafikisha kwenye sheria wale wote ambao kwa makusudi au bila kukusudia wamekiuka sheria au kanuni. Tusiwaonee haya wale wanaopindisha sheria au kuvunja sheria biola kujali sehemu yao katika jamii. Kama Waziri anapinda Sheria ni wajibu wetu kama jamii kumwajibisha. Kama mbunge anavunja Sheria, ni wajibu kumfikisha mbele ya vyombo vya dola ili haki na hukumu kwa kuvunja Sheria ifanyike.
Sheria na kanuni hazikuwekwa zifuatwe na wananchi pekee. Watawala na Viongozi hawana kinga ya aina yeyote ya kuwaepusha kufuata kanuni,sheria au katiba. Sheria na katiba ziliundwa ili zifuatwe na kila raia na mkazi wa Tanzania.
Wakati wa Azimio la Arusha tulitamka kuwa ili tuendelee tunahitaji Watu, Ardhi, Siasa safi na Uongozi Bora. Tukatamka kuwa tunataka kujenga Taifa huru la Kijamaa na lenye Kujitegemea. Tukasisitiza kuwa vita dhidi ya Ujinga, Umasikini, Njaa na Maradhi vitashinda kama tutatumia Juhudi na Maarifa katika kazi zetu na maisha yetu.
Kazi tuliyonayo sasa si tofauti na ile ya mwaka 1967, ni ile ile na sana sana ni kulenga Nyenzo kuu za maendeleo yetu kama Taifa na kibinafsi kwa kupitia milango miwili. Ili tujikwamue kutoka hali hii mbaya tuliyonayo kama Taifa, ni wajibu wa kila mmoja wetu kuwajibika na kuwa na nia ya kweli kuyafanya yafuatayo;
Uchumi utakaoleta matunda ya kweli na ya maana ni uchumi utakaotokana na juhudi za wananchi katika shughuli zote za uzalishaji mali. Tunahitaji tuwe na mipango inayoeleweka na rahisi kufanikisha safari hii ya kujenga uchumi kwa kutumia mazingira yetu, rasilimali zetu na kwa faida yetu.
Moja ya njia zitakazotumika kuimarisha uchumi ni kubadilisha mfumo wa mapato ya Serikali na kudhibiti matumizi.
Kwa kuanzia, Serikali itabidi kupitia mikataba yote na kuongeza viwango vya kodi na ushuru (taxes, duty and royalties) zinazopatikana kutokana na wazalishaji mali wawekezaji. Kiwango cha asilimia 3% tunachotoza kwa shughuli za uchimbaji madini, gesi, makaa na hata huko mbeleni madini ni kidogo sana. Serikali ifuatilie kwa makini mapato halisi ya makampuni yote yanayojishughulisha na shughuli za uzalishaji mali na kuhakikisha kuwa Serikali inapata malipo ya kweli na yanayowiana na uzalishaji na mapato ya makampuni haya.
Serikali ipitie majedwali na ripoti za mapato ya kifedha (financial statements and bapance sheets) ya makampuni haya katika nchi zilikoandikishwa. Mfano pamoja na kuwa kampuni ya Barrick inatozwa asilimia 3% kama kodi kwa Serikali ya Tanzania, ni ukweli usiofichika kuwa Serikali na taifa la Tanzania linapunjwa. Mpango wangu utahamasisha kuchangua vitabu vya kampuni hii katika soko la mtaji la kimataifa kama NYSE, na kuangalia ni mapato kiasi gani ambayo wameyaorodhesha.
Mapendekezo ya kubadilisha viwango hivi vya mapato ya Serikali yanayotokana na uzalishaji mali wa makampuni mageni na hata enyeji, utahakikisha kuwa misamaha yote ya kodi na ushuru ambayo imetumika kama chambo cha kuvutia uwekezaji na kufanya biashara inafutwa au itapewa kipindi kifupi mno ili kupunguza hujuma na dhuluma. Mapendekezo ya kuongeza mapato yatakuwa ni kuongeza viwango vya kodi za mapato kwa makampuni haya kutoka 3% hadi kufikia 20% katika kipindi cha miaka mitano tangu sheria ianze kutumika.
Umiliki wa sekta za madini, uvuvi, utalii uhakikishe kuwa Watanzania kwa kupitia mashirika ya ndani yanakuwa naUshirika yanakuwa na 40% ya umiliki ili kuhakikisha kuwa Taifa haliendelei kunyonywa. Matarajio ya mpango huu ni kuwa Wawekezaji wenye utu watakubaliana na kufanya kazi na Serikali na Taifa kwa manufaa ya pande zote mbili.
Mapato haya ya kutokana na ongezeko la kodi, ushuru na umiliki yataliongezea Taifa pesa za kuweza kuondokana na misaada na mikopo ambayo imetulemaza na kutufanya kuwa tegemezi na masikini. Kuongezeka kwa mapato kutokana na kodi na ushuru kutapunguza ule mzigo wa Serikali kutegemea mazao ya chakula na biashara katika kupata fedha za uendeshaji. Mapato haya yatakuwa moja ya nyenzo kuu za kujenga uchumi kwa kutumika katika kuboresha sekta za Elimu, Afya, Miundombinu na Nishati.
Itaendelea...

- Kurudisha na kuimarisha Heshima, Utu na Uadhi ya Mwananchi na Taifa la Tanzania
- Kurudisha na kuimarisha Heshima, Wajibu na Hadhi ya kazi na kufanya kazi kwa Watanzania wote, vijijini na mijini
- Kuelimisha Wananchi haki zao kama raia, wajibu wao na sehemu yao katika Taifa na Serikali yao kupitia Katiba, Serikali Kuu, Bunge na Mahakama
- Kuimarisha Ufanisi na Ustawi wa Jamii katika kupiga vita Ujinga, Umasikini, Njaa na Maradhi
- Kuhakikisha kuwa Katiba, Sheria na Kanuni zilizowekwa zinatekelezeka kutokana na nyakati zilizopo, zinafuatwa ipaswavyo na vyombo vyote husika; Serikali, Bunge, Mahakama na Wananchi wenyewe. Aidha kuweka maamuzi na mipango ya Serikali wazi kwa wananchi wote ili kuhakikisha uadilifu na uwajibikaji wa Serikali haufanyiki kwa siri na na kuwapa wananchi wote haki kwa kuwa wao ndio waliotoa dhamana ya kuwepo kwa Serikali na kuruhusu Uongozi uliopo uongoze nchi
- Kubuni mbinu za kiuchumi ili kumpunguzia mzigo mwananchi wa kawaida hasa wale wa kipato cha chini na wakulima ili kujenga nguvu kubwa ya taifa kuwa katika Tabaka la kati (middle class)
- Kuhakikisha kuwa njia kuu za Uchumi na uzalishaji mali zinaboreshwa na kutumika kwa manufaa ya kila Mtanzania na taifa la Tanzania linanufaika kwanza
- Kuhamasisha na kuhakakisha kuwa Uzalishaji mali (kilimo, viwanda, uvuvi, ufugaji, biashara, madini , utalii, biashara, sanaa, michezo, huduma na maofisini) unafanyika kwa dhatgi, kisayansi, kiushindani, kiuwajibikaji, kiufanisi na kwa ubora wa hali ya juu kwa kutumia tija, kuongezeka kwa juhudi na maarifa ya uzalishaji mali huu
- Kuhakikisha kuwa huduma za msingi zinaboreshwa na kupewa kipaumbele na kufikishwa kwa wananchi ili kujenga maendeleo ya kweli kwa jamii na Taifa;- Afya, Elimu, Maji safi, Chakula, Uchukuzi na Nishati
- Kuhakikisha kuwa vita dhidi ya Rushwa, Ubadhirifu, Udini, Ukabila, Uzembe, Ufisadi, Uhujumu, Uvivu, Uzururaji na Kutowajibika au kutokujituma kwa watendaji wa Serikali na taasisi zake (wakuteuliwa au kuchaguliwa), waajiriwa , wafanyakazi na wakulima ni vita vya Taifa zima na linahitaji ushiriki na kushirikisha Wananchi wote. Wananchi wote bila kujali kabila, rangi, jinsia, umri, elimu au mwelekeo wa kisiasa ni wajibu wao kushiriki katika vita hii
Uchumi wa Tanzania utakuwa pale ambapo Mtanzania ataacha kutafuta makombo ili aweze kumaliza siku moja anayoamka akiwa hajui kesho ikoje.
Kutokana na udhoofu wa Uchumi na kuzorota kwa Uongozi, hadhi yetu na kujivunia kwetu kuwa Watanzania kama tulivyozoea kujivuna na kuimba "Tazama ramani utaona nchi nzuri... Nasema kwa kinywa na kufikiri nchi hiyo nzuri ni Tanzania" imeshuka na hatujiamini tena. tumekuwa wanyonge na kukubali kuburuzwa na viongozi wetu na hata wafadhili.
Tunahitaji kujirudishia Uzalendo na hadhi yetu kama Taifa. Tukubali makosa tuliyofanya kwa kukusudia au bila kudhamiria. Hiyo itakuwa hatua ya kwanza ya kutafuta suluhisho la matatizo yetu na kujirudishia hadhi yetu na ya Taifa letu.
Msahafu na maandiko yanasema, "asiyefanya kazi na asile". Watanzania tumesahau nidhamu na wajibu wa kufanya kazi. Tumeendekeza malalamiko na manung'uniko, huku tukipunguza tija na juhudi kulilia motisha. Kama tutageuza nguvu zetu hasi kuhusu uchapaji kazi na kuzifanya chanya kuongeza uzalishaji mali na kuachana na kutegemea misaada, basi nafasi yetu ya kuwa na maendeleo ya kudumu yanayoendelea yatakuwa makubwa na hata viongozi wetu ambao wamekosa dira na mwamko wa kutuongoza wataona aibu tutakapoamka kudai haki zetu kutokana na jasho letu.
Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuangalia Kazi kwa mtazamo wa kimaendeleo na chanya. Bila kufanya kazi, kwa ufanisi, juhudi na uhodari, hatutaweza achana na umasikini na unyonge. Iwe ni mijini kwenye maofisi, biashara, viwandani, mashambani au migodini. iwe kazi za kuajiriwa au kujiajiri, ni lazima tuheshimu kazi na kazi ziwe ni zile halali za kutupa mapato.
Hadhi na utu wa Uzalendo na Utaifa na Taifa letu, vitakuwa havina maana kama Mtanzania hatajua wajibu na haki zake Kikatiba, hatajua na kutumia Sheria na kanuni za nchi kujilinda na kujiongoza. Viapo vyetu vya utii visiishie kuwa ni viapo hewa kwa ajili ya kuapa. Tunapoapa kulitumikia Taifa na kuimba wimbo wetu wa Taifa "Mungu Ibariki.." ni lazima tuwe wakweli na wenye Uzalendo wa kweli ndani ya moyo. Kuelewa haki yetu Kikatiba kutaongeza ufanisi wetu na hasa wajibu wetu kama Raia katika kuweka Sheria za kuilinda nchi yetu na kuwa makini kuchagua viongozi wa kutuongoza kama Taifa.
Wajibu wetu mwingine ni kuhakikisha kuwa kazi yetu haishii katika kulinda katiba na kujua haki zetu kama Watanzania, bali ni kufuata sheria hizo na kuzithamini. Tuwe mstari wa mbele kufuata sheria na kanuni tulizonazo na tuwakosoe na kuwafikisha kwenye sheria wale wote ambao kwa makusudi au bila kukusudia wamekiuka sheria au kanuni. Tusiwaonee haya wale wanaopindisha sheria au kuvunja sheria biola kujali sehemu yao katika jamii. Kama Waziri anapinda Sheria ni wajibu wetu kama jamii kumwajibisha. Kama mbunge anavunja Sheria, ni wajibu kumfikisha mbele ya vyombo vya dola ili haki na hukumu kwa kuvunja Sheria ifanyike.
Sheria na kanuni hazikuwekwa zifuatwe na wananchi pekee. Watawala na Viongozi hawana kinga ya aina yeyote ya kuwaepusha kufuata kanuni,sheria au katiba. Sheria na katiba ziliundwa ili zifuatwe na kila raia na mkazi wa Tanzania.
Wakati wa Azimio la Arusha tulitamka kuwa ili tuendelee tunahitaji Watu, Ardhi, Siasa safi na Uongozi Bora. Tukatamka kuwa tunataka kujenga Taifa huru la Kijamaa na lenye Kujitegemea. Tukasisitiza kuwa vita dhidi ya Ujinga, Umasikini, Njaa na Maradhi vitashinda kama tutatumia Juhudi na Maarifa katika kazi zetu na maisha yetu.
Kazi tuliyonayo sasa si tofauti na ile ya mwaka 1967, ni ile ile na sana sana ni kulenga Nyenzo kuu za maendeleo yetu kama Taifa na kibinafsi kwa kupitia milango miwili. Ili tujikwamue kutoka hali hii mbaya tuliyonayo kama Taifa, ni wajibu wa kila mmoja wetu kuwajibika na kuwa na nia ya kweli kuyafanya yafuatayo;
- Kujenga Uchumi imara na madhubuti. Hili litatusaidia katika vita dhidi ya Umasikini, Ujinga, Maradhi na Njaa
- Kuwa na Uongozi mahiri na fanisi. Utawala na uongozi wa nchi unahitaji na unategemea Uongozi mahiri kutekeleza sera na mipango, wenye ufanisi kuhamasisha uzalishaji mali na uwajibikaji na wenye kuwa wanyenyekevu na kuheshimu dhamana walizopewa
Uchumi utakaoleta matunda ya kweli na ya maana ni uchumi utakaotokana na juhudi za wananchi katika shughuli zote za uzalishaji mali. Tunahitaji tuwe na mipango inayoeleweka na rahisi kufanikisha safari hii ya kujenga uchumi kwa kutumia mazingira yetu, rasilimali zetu na kwa faida yetu.
Moja ya njia zitakazotumika kuimarisha uchumi ni kubadilisha mfumo wa mapato ya Serikali na kudhibiti matumizi.
Kwa kuanzia, Serikali itabidi kupitia mikataba yote na kuongeza viwango vya kodi na ushuru (taxes, duty and royalties) zinazopatikana kutokana na wazalishaji mali wawekezaji. Kiwango cha asilimia 3% tunachotoza kwa shughuli za uchimbaji madini, gesi, makaa na hata huko mbeleni madini ni kidogo sana. Serikali ifuatilie kwa makini mapato halisi ya makampuni yote yanayojishughulisha na shughuli za uzalishaji mali na kuhakikisha kuwa Serikali inapata malipo ya kweli na yanayowiana na uzalishaji na mapato ya makampuni haya.
Serikali ipitie majedwali na ripoti za mapato ya kifedha (financial statements and bapance sheets) ya makampuni haya katika nchi zilikoandikishwa. Mfano pamoja na kuwa kampuni ya Barrick inatozwa asilimia 3% kama kodi kwa Serikali ya Tanzania, ni ukweli usiofichika kuwa Serikali na taifa la Tanzania linapunjwa. Mpango wangu utahamasisha kuchangua vitabu vya kampuni hii katika soko la mtaji la kimataifa kama NYSE, na kuangalia ni mapato kiasi gani ambayo wameyaorodhesha.
Mapendekezo ya kubadilisha viwango hivi vya mapato ya Serikali yanayotokana na uzalishaji mali wa makampuni mageni na hata enyeji, utahakikisha kuwa misamaha yote ya kodi na ushuru ambayo imetumika kama chambo cha kuvutia uwekezaji na kufanya biashara inafutwa au itapewa kipindi kifupi mno ili kupunguza hujuma na dhuluma. Mapendekezo ya kuongeza mapato yatakuwa ni kuongeza viwango vya kodi za mapato kwa makampuni haya kutoka 3% hadi kufikia 20% katika kipindi cha miaka mitano tangu sheria ianze kutumika.
Umiliki wa sekta za madini, uvuvi, utalii uhakikishe kuwa Watanzania kwa kupitia mashirika ya ndani yanakuwa naUshirika yanakuwa na 40% ya umiliki ili kuhakikisha kuwa Taifa haliendelei kunyonywa. Matarajio ya mpango huu ni kuwa Wawekezaji wenye utu watakubaliana na kufanya kazi na Serikali na Taifa kwa manufaa ya pande zote mbili.
Mapato haya ya kutokana na ongezeko la kodi, ushuru na umiliki yataliongezea Taifa pesa za kuweza kuondokana na misaada na mikopo ambayo imetulemaza na kutufanya kuwa tegemezi na masikini. Kuongezeka kwa mapato kutokana na kodi na ushuru kutapunguza ule mzigo wa Serikali kutegemea mazao ya chakula na biashara katika kupata fedha za uendeshaji. Mapato haya yatakuwa moja ya nyenzo kuu za kujenga uchumi kwa kutumika katika kuboresha sekta za Elimu, Afya, Miundombinu na Nishati.
Itaendelea...
Last edited by a moderator: