Marmo: Katiba inakwamisha kupambana na ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marmo: Katiba inakwamisha kupambana na ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 2, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,680
  Likes Received: 82,533
  Trophy Points: 280
  Salim Said
  Mwananchi
  October 2, 2009


  Mkuu anayeshughulikia Sera na Bunge Philip Marmo, amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano inakwamisha utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati teule ya Bunge kuhusu uchunguzi wa mkataba tata katika kampuni ya Richmond.

  Kamati teule ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela Dk Harrison Mwakyembe ilifanya uchunguzi kuhusu zabuni ya kufua umeme wa dharura na kugundua kuwepo kwa ukiukwaji wa sheria na taratibu za manunuzi.

  Baada ya kamati hiyo, kubaini kuwepo kwa kasoro hizo, mawaziri watatu wa serikali, akiwemo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, walijiuzulu.

  Kamati hiyo, ilipendekeza mambo mbalimbali ya msingi yatekelezwe ili kukomesha ukiukwaji wa manunuzi.

  Moja ya mambo yaliopendekezwa ni kuwaajibisha baadhi ya watendaji wakuu wa taasisi za Serikali.

  Akizungumza katika mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji (TBC1) Mjini Arusha jana Marmo aliweka hadharani kwamba katiba inakwamisha utekelezaji wa mapendekezo ya kamati ya Dk Mwakyembe.

  "Kama serikali tunaona tuna mapungufu katika katiba, ndio maana hata utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati teule ya bunge kuhusu uchunguzi wa Richmond yanachelewa.

  "Hii ni kwa sababu mapendekezo yale ni nguvu kutoka bungeni na yameletwa serikalini, ambayo nayo ina taratibu na sheria zake na watendaji wa umma nao wana taratibu zao za kushughulikiwa, tofauti na bunge ambavyo imetaka iwe,"alisema Waziri Marmo.

  Marmo alisema kwamba matatizo hayo, mwanzo wake ni katiba ya mwaka 1961 ambayo alidai ni katiba chotara, iliyokopa sehemu kubwa kutoka Marekani, Ufaransa na Uingereza.

  "Kwa upande wa utendaji wa vyombo vya serikali tumekopa kutoka Uingereza, katika utendaji wa bunge, tumekopa kutoka Ufaransa na Uingereza kidogo, kwa hiyo haya yote yanafanya utendaji wa kila siku wa serikali yetu kuwa mgumu, moja wapo ni hili la utekelezaji wa mapendekezo ya kamati teule ya Bunge kuhusu Richmond," alisema Marmo.

  Alisema, kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri, hata kama bunge litapendekeza jambo, lakini mapendekezo hayo, lazima yatekelezwe na serikali, jambo ambalo ni gumu wakati mwingine.

  "Katiba hii imegawa madaraka katika misingi ambayo inakuwa ni vigumu kwa serikali kutekeleza kwa haraka mapendekezo ya bunge hata kama yanahusu mambo mazito ya nchi.

  "Hivyo basi unaweza kusema kwamba nguvu na uwezo mkubwa wa bunge uanakumbana na vikwazo, vizingiti na masharti magumu kutoka serikalini," alisema Marmo.

  Alifafanua kwamba, mgongano wa kimaamuzi kati ya serikali na bunge ni ya kwaida na mara nyingi huwa yanajenga na kutoa changamoto kwa pande zote mbili za serikali na bunge. "Hii ndiyo maana vyombo hivi vimepewa majukumu tofauti, lakini kwa upande wa serikali yetu haya ni mambo mazuri, yanayojenga na kuleta afya ya serikali katika nchi, ili serikali isionekane kwamba muda wote imelala,"alisema.
   
 2. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Marmo ni sell out!Mnakumba wale wabunge walitaka serikali 3,Tanganyika ,Zanzibar na Muungano!Tangu wakati huo CCM wamuweka chini,sio mtu wa msimamo tena
   
 3. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Marmo muongo, katiba hairuhusu watu kufanya ufisadi, kikwazo kipo wapi !!
  Anavyoongea ni kana kwamba katiba imesema "nendeni mkafanye ufisadi."
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mwaka huu lazima tupate wendawazimu kwa kauli hizi za hao mawaziri wa JK
   
 5. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Ukweli kuwa katiba yetu inahitaji mabadiliko makubwa kulingana na mahitaji ya sasa hauwezi kupingwa, lakini inawezekana tunayotaka yabadilike kwenye katiba siyo anawayowaza Marmo na jokers wenzake. Wakati wananchi tunapodai katiba mpya, inayoweka tume huru ya uchaguzi, kupunguza madaraka ya viongozi kama raisi na mengineyo, wako busy kusuppress, kwa kuwa wamebanwa kutekeleza maamuzi wanadai katiba ni kikwazo, toka lini waligundua lini? For some reasons, this guy must be insane and sick upstairs.
   
 6. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180

  Umenena 100%...Na ukiona hivyo basi soon ataleta mswaada unaotaka marekebisho /kiraka kingine kinachoendana na ufisadi ndani ya katiba iliyochoka, kwanini asiseme wazi kuwa katiba yetu kwa ujumla irekebishwe? watu tunataka katiba itakayodumu, itakayoongoza bila kujali chama gani nani, kabila gani, dini gani iko madarakani, katiba itakayotatua mgogoro wa Pemba na CCM, katiba itakayotatua mgogoro wa muungano, katiba itakayo tatua kinibu cha mafuta ya Zanzibar etc...
   
 7. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wakitaka hoja za mgombea binafsi wazizue wanabadilisha katiba haraka in one night.Wakitaka kujitengenezea mazingira mazuri ya kushinda kwa wizi wanabadilisha katiba over night.
  kupingana na ufisadi wameshindwa nini kubadilisha hiyo katiba overnight kama ilivyojaa viraka hivi sasa???
  Marmo aache upuuzi tena mara moja.Tumechoka ujinga.
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Mchnga wa macho ndugu yangu huo....wajanja wengi wanaona kurudi 2010 ni kuwafwataa wakina mwakyembe baada ya kuona makamba nae kawageuka hao waache wapige porojo zao lakini ni walewale hao
   
 9. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2009
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  nasikia kichefuchefu...........
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Atuambie ni ibara gani ya katiba ina matatizo na kwa jinsi gani labda great thinkers can assist him in solving that small problem. Awe particular on that mambo ya kuongea kwa ujumla jumla tu hawasaiidia kwenda kwenye mzizi wa matatizo
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,680
  Likes Received: 82,533
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kevo, ndiyo mafisadi walivyo siku zote huweka mbele maslahi yao badala ya yale ya Watanzania wote.
   
 12. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kama unavyosema Katiba yetu ni katiba ambayo haiangalii maslahi ya wananchi hata kidigo, toka kutungwa 1977 mpaka leo kuna mabadiliko zaidi ya mara 14, mara zote hizo ni kuangalia maslahi yao tu na si ya wananchi. Wanasahau kabisa kuwa hii ni Katiba ya wananchi na sio ya viongozi.Zaidi ya hivyo kuna sheria nyingi tu ambazo zimetungwa ambazo zinajaribu kukwepa katiba ambayo waliitunga wenyewe. Mfano wa karibu ni wanaweka bill of rights katika katiba na kuzifanya justiciable wakazidiwa na wakatunga sheria ya Basic Rights and Duties Enforcement Act ambayo inapingana na concept yote ya kuwa na bills of rights ambazo inalindwa na mahakama.
   
 13. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #13
  Oct 3, 2009
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Katika katiba yoote hiyo haina sehemu inayosema kuwa rushwa na uhujumu uchumi ni adui wa haki??? Kipengele hicho pekee kinatosha bila ya longa longa nyingine....
   
 14. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kama nimemuelewa waziri ni kuwa serikali inshindwa kuyafanyia kazi maoni ya Tume ya Richmond kutokana na katiba, Muda waliopewa umefika sasa wanatafuta scapegoats walahi mbona vichekesho.Wabunge waikomalie serikali kwa kudharau bunge kama hawatatekeleza, kusiwe na visingizio.
   
Loading...