Elections 2010 Marmo:jukumu la kuwarudisha wanavyuo kwenye vituo vyao vya kupigia kura ni la nec..!

urasa

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
434
2
tukisema watawala wetu ni vichwa maji wanasema tunawatukana na kuhatarisha amani ya nchi,hivi hili tamko la waziri marmo lina mwelekeo upi haswa?anasema nec ni taasisi huru na hawezi kusemea juu ya wanavyuo ambao hawataweza kupiga kura tokana na vyuo kufungwa,kwanza anasema:
  • serikali haijamzuia mwanachuo kwenda kupiga kura kwenye kituo alichojiandikisha,akisahau hao wanavyuo wanaishi kwa boom toka serikalini na si waajiriwa
  • nec ndio yenye jukumu la kuwarudisha hao wanafunzi,hivi kuna uhusiano gani wa nec na wanavyuo?kwanini serikali inakimbia kivuli chake?hao wanafunzi wanawekewa pesa za kujikimu na nec?
sasa huyu ni waziri anatoa majibu kama hayo,anataka tumwelewe vp?
 
Kama wanavyuo wenyewe wamekubali kutokupiga kura na wanakaa nyumbani wakiombea serikali "iwape" haki yao well.. hawana mtu mwingine wa kumlaumu.
 
Natamani kweli kupiga kura kwa mara ya kwanza na ya mabadiliko Tanzania, lakini nitafika vipi dar es salaam toka Tarime maana kukaa huko si mchezo razima uwe na kiasi cha kutosha!familia ina watoto kibao ukisha pata mkopo ndio umepunguza mzigo kwa mzazi tuna pata wapi hela kama bodi ya mkopo haitoi hela twende????

Maana chuo kimesema accomodation wanatoa kwanzia sasa, ina kua vipi bodi isitoe hela twende chuo kupiga kura?
 
  • nec ndio yenye jukumu la kuwarudisha hao wanafunzi,hivi kuna uhusiano gani wa nec na wanavyuo?kwanini serikali inakimbia kivuli chake?hao wanafunzi wanawekewa pesa za kujikimu na nec?
sasa huyu ni waziri anatoa majibu kama hayo,anataka tumwelewe vp?

Hapo umeongea ndugu yangu lakini jibu ni kuchagua Dr. Slaa na Chadema waje kuisafisha nchi hii kiupya kabisa
 
Natamani kweli kupiga kura kwa mara ya kwanza na ya mabadiliko Tanzania, lakini nitafika vipi dar es salaam toka Tarime maana kukaa huko si mchezo razima uwe na kiasi cha kutosha!familia ina watoto kibao ukisha pata mkopo ndio umepunguza mzigo kwa mzazi tuna pata wapi hela kama bodi ya mkopo haitoi hela twende????

Maana chuo kimesema accomodation wanatoa kwanzia sasa, ina kua vipi bodi isitoe hela twende chuo kupiga kura?

Mwanakijiji kasema hapo juu kwamba.... ni jukumu lenu wanavyuo ku ipressurise serikali(ccm) iwape haki yenu ya kupiga kura.
Mkinyamaza hakuna wa kuwasemea.! Naungana nae kabisa kwamba wanavyuo popote walipo wanatakiwa waseme na waonekane kusema kwamba wanataka haki yao ya kupiga kura ... wasitegemee serikali(ccm) itawapa hiyo haki bila kuidai
 
hata huko ni mbali sana, cha kujiuliza kwanza ni kwanini vyuo vibadilishiwe ratiba kipindi hiki cha uchaguzi?. Wanatengeneza tatizo halafu wanajifanya ni gumu kutatua. Ni unafiki wa ccm pamoja na nec yake.
 
tukisema watawala wetu ni vichwa maji wanasema tunawatukana na kuhatarisha amani ya nchi,hivi hili tamko la waziri marmo lina mwelekeo upi haswa?anasema nec ni taasisi huru na hawezi kusemea juu ya wanavyuo ambao hawataweza kupiga kura tokana na vyuo kufungwa,kwanza anasema:

  • serikali haijamzuia mwanachuo kwenda kupiga kura kwenye kituo alichojiandikisha,akisahau hao wanavyuo wanaishi kwa boom toka serikalini na si waajiriwa
  • nec ndio yenye jukumu la kuwarudisha hao wanafunzi,hivi kuna uhusiano gani wa nec na wanavyuo?kwanini serikali inakimbia kivuli chake?hao wanafunzi wanawekewa pesa za kujikimu na nec?
sasa huyu ni waziri anatoa majibu kama hayo,anataka tumwelewe vp?

Wengi tumejikita kufungua vyuo kama njia mbadala ya wanafunzi kupiga kura vyuoni lakini tunasahau kwamba vyuo vikifunguliwa wanafunzi wanaonza mwaka wa kwanza hawataweza kupiga kura vyuoni kwa kuwa walijiandikisha majumbani mwao kabla ya kupata nafasi ya masomo lakini pia kuna wanafunzi wa mwaka wa mwisho waliomaliza masomo yao walijiandikisha chuoni na sasa wako majumbani mwao. Kwa vyovyote vile, wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa mwisho waliomaliza masomo hawatapiga kura hata kama vyuo hivyo vitafunguliwa. Suala hili si la kukurupuka bali kutafuta jibu la kudumu.
 
Mwanakijiji kasema hapo juu kwamba.... ni jukumu lenu wanavyuo ku ipressurise serikali(ccm) iwape haki yenu ya kupiga kura.
Mkinyamaza hakuna wa kuwasemea.! Naungana nae kabisa kwamba wanavyuo popote walipo wanatakiwa waseme na waonekane kusema kwamba wanataka haki yao ya kupiga kura ... wasitegemee serikali(ccm) itawapa hiyo haki bila kuidai
Kwa maoni yangu bado hawajachelewa.Wanaweza kufungua kesi mahakamani kudai haki yao na kuitisha maandamano ya kudai haki yao ndani ya siku hizi chache zilizobaki.
Uongozi wa Chuo pamoja na NEC walikuwa wanajua kuwa wanachuo wote wamejiandikisha kupiga kura hapo chuoni na kwa kusogeza mbele tarehe ya kufungua chuo ni kunyume na matakwa ya haki ya kupiga kura mahali ulipojiandikisha.
Hapa ni mahala pake kwa wale wanaochukua Sheria vyuoni kuonyesha hawapo vyuoni kuonyesha Sura bali kujuzwa na kwamba kwa kiasi fulani wamejuzika na kwamba wanaweza kutetea haki yao.
 
Kupiga kura wanavyuo sio ishu, ishu ni kuwa je serikali ina hela za kuendesha nchi? Hela zote wamezipeleka CCM kufanyia kampeni, na hata hivyo vyuo vikifunguliwa leo hawana hela za kuwapa kukidhi mahitaji yao na ndio maana wakawapa likizo ndefu ili ccm itumie hela kwenye kampeni.Mi nashauri tume ya uchaguzi iwaruhusu kuchagua hata rais tu huko waliko wala sio madiwani na wabunge.Shime wanavyuo msirudi nyuma kwa hili, kura zenu ni muhimu sana kwetu, chagueni CHADEMA ili tulete madabiliko ya kweli.
 
Si shangai sana kauli ya Marmo. Ndivyo walivyo vciongozi wengi wa CCM. Waziri wa Elimu ya juu aliwahi kusema kuwa wanachuo wanapaswa kuzingatia elimu na waachane na siasa. Hii yote ni kwa sababu tu ya hofu waliyonayo wana CCM kwa kuwa wanajua wazi sehemu kubwa ya wanavyuo wengi CCM si chaguo lao. CCM ina tawi lake Mzumbe japo liko nje ya Chuo UDOM nako, je wanavyuo wakiwa CCM ni sawa lakini wakiwa wa vyama vingine ni jinai? siku zote mfa maji haachi kuhangaika. Bunge liliopita CCM lilikuwa na Viongozi wa madhehebu ya dini kama wabunge lkn Karatu kumsimamisha mgombea toka ktk dhehebu la dini imekuwa ishu kuwa viongozi wa dini wabaki kuwalea waumini wao na wasiwe wanasiasa. Je hiki chama kina dira kweli? Siwaelewi
 
Back
Top Bottom