Mark Mwandosya: Wiki nzima tumekosa mvua lakini leo kwa ujio wako Rais Magufuli tumepata mvua ya ghafla na hii ni Baraka

Kichekesho Mwandosya anamwambia Magufuli kafika na baraka ya mvua, huku Magufuli alikuwa Dar muda wote hakuna mvua! Kwa sifa hiyo usishangae kesho akamtea kwa cheo chochote Mwandosya atakachotaka.
Dar mvua ya nini?

Rungwe wanahitaji mvua ndio maana imekuwa ni baraka, Dsm mvua unataka mafuriko mabondeni?!!!
 
Jina Makwale limenijia kichwani.

Kwa hizo ahadi za Magu kuahidi kila anayemsaifia, sipati picha akiwa na mwanamke mweupe anahonga kiasi gani. Huyo jamaa ni wale wakiingia bar wananunulia kila mtu bia ili kuonekana ana hela kisa wanamsifia.
 
Dar mvua ya nini?

Rungwe wanahitaji mvua ndio maana imekuwa ni baraka, Dsm mvua unataka mafuriko mabondeni?!!!

Hakuna mahali pasipohitaji mvua kwani ni balance of nature. Mafuriko mabondeni ni matokeo ya ujenzi usiofuata taratibu za ujenzi.
 
Rais Magufuli anaendelea na ziara yake wilayani Rungwe na sasa yuko Busokelo nyumbani kwao mzee Mwandosya.

Mzee Mwandosya ambaye ni mbunge mstaafu amemshukuru sana Rais Magufuli kwa ujio wake hapo Busekelo ambao umeambatana na mvua ya baraka..
Mzee Mwandosya amemwomba Rais Magufuli awasaidie fedha za ujenzi wa barabara ambapo kuna kama 20km hivi hazina lami na ana uhakika Rais atawakamilishia tena si km 20 bali na zaidi.

Source TBC

Maendeleo hayana vyama!

Up dates;
Rais Magufuli anasema bunge lilipanga kuanza na km 17 kwa mujibu wa bajeti lakini kutokana na ombi hilo maalumu ambalo mh Mwandosya amekuwa akimuomba tangu wakiwa mawaziri, hivyo serikali itajenga km zote 71 kwa kiwango cha lami.

CCM hoyeee.......... Mwandosya hoyeee!!
Hivi bunge huwa linakaa kichwan kwa mhe au mana kila kitu akiombwa utasikia bunge limekaa
 
Prof. Mwandosya akiwa kwenye keyboard anashambulia sana utawala wa jiwe. Akikutana nae anamsifia.

Unafiki huu japo wengine wataita busara.

Anakuwa kama CDM wakikutana na jiwe wanajichekesha!
Au ndo na yye kamdeshi kumuongezea km17 kuwa 71 akijua kabisa jamaa huwa ana mnanga
 
Hata CAG na kukomaa kwake kote alipoulizwa live na mkuu Kuna Fedha zimeibiwa akasema hakuna. Japo ripoti yake ilionyesha upotevu wa fedha kibao.
Mkuu akiwa katika enzi yake, anakuwa na utisho flani wote wenye mawazo mbadala wanasinyaa.
sishangai
Lile jibu la Prof.Assad lilikuwa sahihi kabisa mkuu, hakuna sehemu yeyote aliyosema fedha zimeibwa katika report yake. Katika ukaguzi wa taasisi za umma public finance act imezungumia kitu inaitwa nugatory expenditures kwa tafsiri yake (swahili), ni matumizi hewa. Hii ni professional mkuu, kuwa CAG it doesn't come easy anyway. Yaani mjumbe wa bodi inayokagua taasisi zote za umoja wa mataifa ashindwe kujibu swali dhaifu kama lile? Chekecha akili yako mkuu!
 
Hivi waafrika ujinga huu tutaacha lini?! Inasikitisha sana Professor mzima kuhusisha ujio wa rais na mvua.
It doesn’t make any sense. Huu upumbavu huwezi kuisikia katika nchi zilizoendelea
 
Chademaaaaa nini Shida haswa? Kwani Prof alishahama fisiemu? Mimi Ndivyo his bado Sana tu......
 
Baada ya kutishwa tu akatulia ni kauli ya kinafiki sana"

Mimi niko mbeya Pia kama week sasa ila mvua inanyesha kila baada ya siku moja au mbili ......

Toka tulipozindua Mwenge pale Songwe mvua nyanda za juu kusini mvua inanyesha kila siku au baada ya siku mbili leo unasema Rais kaleta mvua?....

Rais amekuwa Mungu au yeye ndiye aliyepanda miti na kuotesha milima iliyopo nyanda za juu kusini?

Siasa ni unafiki sana au anaishi ndani yeye alipotoka njee na alipoona kijiwingu ndio kaamua kujitoa ufahamu..

Shame....
pasuka
 
Prof Mwandosya kaamua kutumia akili na Busara zake

Kuna watu walidhan angeiga ya Yule Muhaya Balozi Hamis Kagasheki kupuuza ujio wa Rais Bukoba akabaki zake Dar ea salaam wakati angepaswa kwenda Bukoba kumpokea Mkuu wa Taifa

Busara chache za Mwandosya kujishusha kwa Boss imesababisha wajengewe kilometa 71 za lami badala ya 17
Namba zimegeuka 17 kuwa 71 chezea Magufuli wewe
 
Rais Magufuli anaendelea na ziara yake wilayani Rungwe na sasa yuko Busokelo nyumbani kwao mzee Mwandosya.

Mzee Mwandosya ambaye ni mbunge mstaafu amemshukuru sana Rais Magufuli kwa ujio wake hapo Busekelo ambao umeambatana na mvua ya baraka..
Mzee Mwandosya amemwomba Rais Magufuli awasaidie fedha za ujenzi wa barabara ambapo kuna kama 20km hivi hazina lami na ana uhakika Rais atawakamilishia tena si km 20 bali na zaidi.

Source TBC

Maendeleo hayana vyama!

Up dates;
Rais Magufuli anasema bunge lilipanga kuanza na km 17 kwa mujibu wa bajeti lakini kutokana na ombi hilo maalumu ambalo mh Mwandosya amekuwa akimuomba tangu wakiwa mawaziri, hivyo serikali itajenga km zote 71 kwa kiwango cha lami.

CCM hoyeee.......... Mwandosya hoyeee!!
yaani sisi maCCM tupo extremely trivial, agricultural and childish... kuanzia kule juu mpaka kwa sisi vidampa kina johnthebaptist !!
 
Nimeishi Wilaya ya Rungwe, Mwakaleli kwa miaka miwili.

Hapo mvua kunyesha ni kawaida.

Mwandosya kaamua tu kusema hivyo.

Mvua pale ni mwaka mzima.

So hakuna cha muujiza
Magufuli anatisha, hakuna cha mkapa,kikwete shein,karume wala nani! Mbele ya magufuli wanatetemeka tu huku jasho likiwatoka. Amaa! Kweli
 
Back
Top Bottom