Mark Glenn: Huenda Israel itafanya njama za kuuaa Trump

raynew

Member
Jan 17, 2017
9
14
Mark Glenn, mchambuzi mashuhuri wa kisiasa nchini Marekani amesema yumkini serikali ya Washington ikapanga njama za kuuawa Rais mpya wa Marekani Donald Trump, iwapo hatasimamia maslahi ya Wazayuni.

Mark Glenn ambaye pia ni mwandishi wa vitabu ameiambia kanali ya televisheni ya Press TV kuwa, utawala khabithi wa Israel huenda ukapanga kuuawa Trump, namna ulivyochochea mauaji dhidi ya rais wa zamani wa Marekani John F. Kennedy, ambaye daima alipinga mradi wa silaha za nyuklia za utawala huo bandia.

Mchanganuzi huyo wa masuala ya siasa wa Marekani amefafanua kuwa, hatua ya vyombo vikubwa vya habari vinavyofadhiliwa na Wazyuni kumponda Trump katika siku hizi zake za kwanza ofisini, ni kutaka kumshinikiza afuate sera za utawala haramu wa Israel katika eneo la Mashariki ya Kati.

Mwandishi huyo wa vitabu wa Marekani ameongeza kuwa: "Sio Russia iliyofanya Trump achaguliwe kuwa rais, ni Wazayuni walioendesha kampeni za kutaka Hillary Clinton achaguliwe, na kwa sasa wamekanganyikiwa kwa kuwa hawawezi kumdhibiti rais huyo mpya."

Aghalabu ya mashirika makuu ya habari ya Marekani siku ya Ijumaa baada ya kuapishwa Trump, yaliakisia pakubwa maandamano ya Wamarekani wanaompinga rais huyo mpya, baadhi yazo yakiripoti kuwa, idadi ya walioandamana ilishinda idadi ya waliohudhuria sherehe za kula kiapo Trump.
 
source au umeamuwa kujifraisha mwenyewe? wewe unawezaje kuita taifa la watu kaifa la haramu????....thread yako umeijenga kwa chuki.....
 
Mimi pia sijui kwa nini naliona hili........

Huyu tu mkurugenzi Wa CIA aliyeapishwa Jana kamwambia hatharani aachane na Russia......

Wakati jamaa anataka mausiano na Russia yaanze upya.......

Wakati huo huo akijua kabisa Russia uwa inaweka kura ya hapana kwa kwa kila Sera ya Israel anayopeleka kwenye baraza la usalama la umoja Wa mataifa.................

Trump kama Sera zake ndio hizi za kujitoa kwenye TPP wakati Sera hizi zikitegemewa kupunguza mzunguko Wa biashara ndani ya marekani........

Nimemsikia pia akiongeza kodi kwa wafanyabishara Wa marekani wanaozalisha bidhaa nje ya nchi na kuzileta marekani anasahau kuwa ilo pia litasababisha wafanyabishara kuamisha biashara zao na kuelekeza nchi zenye kodi nafuu...........

Wakati huo huo jamaa anapambana na media wakati akijua kupambana na media kwa katiba ya marekani ni ngumu...........

Basi tutegemee surprise kutoka kwenye vyombo vya usalama vya marekani........

Au Impeachment kutoka kwa Wa marekani wenyewe ...........
 
bila shaka vyanzo vyako vya habari ni CNN a.k.a CLINTON NEWS NETWORK ama ABC news au sio mwalimu nyerere mzee wa ujamaa.
 
Back
Top Bottom