Marioo The Kid You Know Album Review: The Mix Of Bongofleva, Afrobeat And Amapiano Collaborations Of Wakali Wa Africa

Brother Wako

Member
Mar 18, 2017
21
19
Marioo The Kid You Know Album Review: Mchanganyiko Wa Kolabo Za Bongofleva, Afrobeat Na Amapiano Za Wakali Wa Africa

Siku kumi na moja baada ya kuitambulisha artwork yake sambamba na tracklist, hatimaye #TheKidYouKnowAlbum ya Marioo imefikishwa rasmi kwa wasikilizaji wake usiku wa kuamkia Disemba 9, 2022. Katika kusherehekea sikukuu ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania), huenda mwanamuziki huyu na CEO wa Bad Nation ameamua kuwapa mashabiki wake zawadi ya kufungia mwaka.

TKYN%20COVER.jpg


Ukisikiliza The Kid You Know, unaziisikia Bongofleva, afrobeat na amapiano, kitu ambacho kinaweza kufanya usiiache kuisikiliza albamu hii kila wimbo mmoja unapoisha na unapobadilika.

Unaweza kufikiria ni kama playlist iliyopangiliwa na muzki Kutokea Tanzania, South Africa, Kongo mpaka Senegal. Halafu Nigeria, ambapo Marioo amemvuta mkali LADIPOE na Dunnie ( huyu tutamzungumzia baadae).

Kwenye track namba kumi na saba, Gaz Mawete wa Kongo na Jeeba wa Senegal, hawa wamempa Marioo ushirikiano wa kutosha kuifanya reggatone version ya Mi' amor Remix ikamilike.

Huenda ngoma hiyo ikawatambulisha washikaji kwa mashabiki wa Bongo fleva wanaofuatilia muziki wa Marioo, Mi amor orijino version na Jovialy wa Kenya ipo kama wimbo namba tisa, kutokea Uganda utamsikia Fac Fameica kwenye Djudju.

Mpaka kufikia mchana wa sikukuu ya Uhuru wa Tanzania, The Kid You Know imeingiza nyimbo 13 mpya kwenye chati ya #itunes kwenye nyimbo 100 zinazosikilizwa Tanzania. Kati ya hizo, nyimbo nne zipo Top 10.

Kwa mujibu wa chati hiyo, Lonely waliyoshirikishwa Abbah pamoja na Loui, ndio wimbo unaoshika nafasi ya kwanza kwenye chati hiyo. Kwa maana hiyo, Lonely ndio wimbo wa Marioo unaosikilizwa zaidi leo.

Kama chati hii itazidi kuzipandisha nyimbo za Marioo zaidi ya leo, Marioo atakuwa miongoni mwa wanamuziki wanosikilizwa mara nyingi wikiendi hii na kipindi chote cha mapumziko ya sikukuu ya krismasi na mwaka mpya kwani, production ya album hii imekusanya ladha za wanamuziki wote wanaofanya vizuri Afrika.

Kuna wanamuziki hawajashirikishwa kwenye albamu hii kwa sababu Marioo amepita na fleva ya muzki wao wote

Album hii ya kwanza ya Marioo itakufanya ujisikie kupendwa hata utamani kuingia kwenye mapenzi tena, utakuwa mpweke, Utakumbuka zamani, utafurahishwa, utasikitishwa, utajifariji uwe na wasiwasi halafu ule bata na maisha yaendelee.

Anisamehe na Chui Rayvanny inaenda kuwa ngoma itakayofanyiwa tiktok challenge na warembo wengi waliokosea kwenye mahusiano yao. Mchuano wa Marioo na Rayvanny ni mkali hapa ndani, lakini kitu kizuri ni kwamba wameshirikiana vizuri sana kuikamilisha hii track namba kumi na tatu.

Mwagia Ndani, humu Marioo ameshirikiana na Robot Boii wa Afrika Kusini, Native Deep na mtanzania Tin Starkid, hii ni ngoma ambayo inaenda kuwa favourite ya wavimbaji. Kuna mahali Marioo anasikika akisema "Tunamuogopa Mungu Pekee", sio wewe, sio yule, sio kifo, sio majukumu.

Unaweza kuimagine vile hii ngoma itapita na vibe ya washikaji zetu ambao hawajali wala kuogopa kuhusu mtu yeyote, bali wanaamini katika mawazo yao wenyewe.

Wapendao wamepewa nafasi ya ku'vibe na siwezi ambayo Marioo anaitumia kumwambia mpenzi wake kuwa hawezi kuachana nae wala kumliza mpaka azikwe. Maudhui ya siwezi yanaipa ruhusa ya heshima kabisa ngoma hii kupigwa kwenye matukio ya sherehe za harusi.

Kwenye siwezi, Marioo ameongezea ladha ya Kiingereza kidgo kinachoeleweka, kitu ambacho kinaweza kushawishi wasiojua Kiswahili kuelewa kinachozungumziwa kwenye wimbo huo.

Ngoma nyingine maalum kwa wapendao ni Only You, production ya Abbah iliyowakutanisha Marioo na Jux, Marioo na Jux wanasema vitu vyote vizuri kwenye dunia wapewe watu wangine lakini wao waachiwe my wao tu.

Hapana ikitumika kama dedication kutoka kwa mwamba anaeteswa na mapenzi kwenda kwa mapenzi wake ambaye anaamua kuondoka kwenye maisha yake, inaweza kufufua penzi linalokufa. Marioo anadai ahadi yake akimkumbusha mchumba jinsi ambavyo mwamba amezama kwenye mapenzi yake.

Kuna amapiano inaitwa Amawele, Marioo ameshirikiana na Tyla na Chi'cco. Amawele inamfanya Marioo abaki na taji lake la mfalme wa amapiano Bongoflevani akifuatiwa na Harmonize ambaye wameshirikiana kwenye track namba 12, Naogopa.

King Kiba ametoa shavu la nguvu kwenye track namba 10, I miss, ambayo ni production ya Abbah. Marioo na Alikiba watakufanya umkumbuke Ex wako, ndani ya wimbo huu kuna feelings za mshikaji anaye-experience breakup inayomfanya ayakumbuke mazuri yote ya ex wake.

Mapenzi kama mapenzi, Marioo ameitumia ngoma hii kuelezea jinsi anavyompenda baby wake, Marioo anatusimulia hadithi ya mpenzi mwenye wivu kiasi ambacho ukisumbuana na Baby wake atakutoa meno.
Mapenzi ni Production ya Blaq ambaye alifanya nae Raha mwaka 2019. Combination ya Blaq na Marioo inaonyesha kupendeza kwenye nyimbo za kupendwa.

Kuhusu uandishi, Tracklist haijatoa credit kwa waandishi waliohusika kukusanaya mistari ya The Kid You Know. Lakini kuna uwezekano mkubwa Marioo alishirikiana na wataalam wengine kulikamilisha hilo.

Marioo sio msanii wa kawaida, yupo kwenye Top 10 ya wanamuziki wanosikilizwa kila siku BoomPlay, Report ya Spotify Wrapped Imemuweka kwenye top 5 ya wanamuziki wanaosikilizwa Tanzania akiwa na zaidi ya wasikilizaji laki nne kila mwezi kwa mwaka huu 2022.

Bila shaka, The Kid You Know itaboresha thamani yake kama mwanamuziki ambaye for the record, albamu yake ya kwanza ameirelease chini ya Label yake mwenyewe 'BAD NATION'.
 
Back
Top Bottom