Marioo, Mfalme wa Amapiano Bongo, Ndiye Msanii Bora kwa Sasa, Hajawahi Kutoa Wimbo Mbaya

Jerlamarel

JF-Expert Member
Sep 14, 2021
843
2,517
Ni wakati huyu kijana akapewa heshima ya pekee kunako industry ya muziki. Tangu atoe ngoma yake ya kwanza "Dar Kugumu" mwaka 2018, ameendelea kutoa hits after hits, ngoma zote ni moto wa kuotea mbali.

Hebu angalia hii list ya nyimbo zake ndio utanielewa:

1. Dar Kugumu
2. Yale
3. Manyaku
4. Ifunanya
5. Wauwe
6. Inatosha
7. Raha
8. Weka
9. Aya
10. Unanionea
11. Tikisa
12. Mamam Amina
13. For You
14. Wow
15. Bia Tamu

Historia Fupi Ya Marioo

Marioo alizaliwa Kibiti, Pwani ni mwimbaji wa Bongo Flava, pia mtunzi na mtayarishaji wa nyimbo. Marioo ameshawahi kutunga nyimbo na kuuza, mfano wimbo alioimba mwanamuziki Nandy 'The African Princess' uitwao 'Wasikudanganye'. Pia ndiye mwandishi wa wimbo wa msanii Jux uitwao 'Unaniweza'.

Wimbo wake wa kwanza ni [>]Dar Kugumu[/i], uliorekodiwa mnamo 2017, ulihit sana na kuwa wimbo nambari moja katika karibu vituo vyote vya redio na televisheni nchini. Kabila la Marioo ni Mndengereko. Pia amefanikiwa kufanya kolabo na wasanii wa nchi mbalimbali akiwemo Show Majozi wa Afrika kusini.


Marioo.jpeg
 
Jamaa anajua sana, bia tamu weee asikuambie MTU moja ya nyimbo zake niliyotokea kuipenda sana hasa ninapokuwa kwenye kiti kirefu.
 
Nafikiri huyu anaweza akawa anamkaribia Simba PlatNumz...

Atoke nje sasa.
 
Back
Top Bottom