Mario Magonga : Rubani wa naibu rais William Ruto afariki baada ya helikopta kuanguka Kenya

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,525

Mario Magonga : Rubani wa naibu rais William Ruto afariki baada ya helikopta kuanguka Kenya


_105878607_gettyimages-1093182772.jpg
Haki miliki ya pichaSOUTH CHINA MORNING POST
Rubani wa naibu rais William Ruto amefariki katika jali ya ndege baada ya helikopta aliyokuwemo kuanguka nchini Kenya.
Taarifa katika vyombo vya habari nchini zinaeleza kwamba ndege hiyo ilianguka Jumapili mwendo wa saa mbili usiku katika eneo la Turkana.
Inaarifiwa kwamba Kapteni Mario Magonga amefariki pamoja na abiria wengine wanne.

Polisi inasema helikopta hiyo imeanguka katika eneo la Labolo, kisiwa chenye milima ya volcano katikakati ya ziwa Turkana - Central Island National Park kaskazini magharibi mwa Kenya.
Ruka ujumbe wa Twitter wa @DennisOkari
#UPDATE: Police say Captain Mario Magonga died with four Americans after their helicopter came down at Labolo in Central Island National Park in Lake Turkana at 8pm. pic.twitter.com/Cs5fsuGtkv
— Dennis Okari (@DennisOkari) 4 Machi 2019
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @DennisOkari
"Taarifa zilizopo zinaashiria kwamba ndege mbili zilitua mapema katika kambi ya Lobolo katika kisiwa hicho kilichopo kwenye mbuga ya kitaifa, hatahivyo moja ndio iliyofanikiwa kutua salama katika eneo hilo," idara ya polisi imesema katika taarifa yake rasmi.
Ruka ujumbe wa Twitter wa @NPSOfficial_KE
Last evening at about 8pm, a helicopter crashed at Central Island National Park in Lake Turkana, killing all its five occupants on board.

Security personnel dispatched to the scene confirmed that among the five were four Americans and the Kenyan Pilot. 1/3
— National Police Service-Kenya (@NPSOfficial_KE) 4 Machi 2019
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @NPSOfficial_KE
Inaarifiwa kwamba vikosi vya usalama vimetumwa katika eneo hilo katika kusaidia kwenye jitihada za kuondosha miili na masalio ya ndege hiyo.
Kufikia sasa, chanzo cha ajali bado hakijajulikana.
Ruka ujumbe wa Twitter wa @Hon_Kiptoo
DP Ruto's pilot Captain Mario Magonga dies in a helicopter crash in Turkana. Magonga was a highly skilled, experienced and respected pilot. Cause of crash unknown. RIP. pic.twitter.com/SpmXtHcgux
— Eng. Peter Kiptoo (@Hon_Kiptoo) 4 Machi 2019
 
Back
Top Bottom