Marine Salvage- (Uokoaji wa meli na mizigo)

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,946
12,513
Marine Salvage ni kitendo cha uokoaji meli na mizigo endapo meli inataka kuzama, imepata hitilafu kwenye hali mbaya ya hewa baharini, meli imekwama au kupatwa na janga lolote.

Kwanini inafanyika Marine Salvage
1.
Kuokoa mizigo na vitu vya thamani katika meli
2. Kuzuia uchafuzi wa bahari endapo meli itamwaga mafuta
3. Kutosababisha kikwazo sehemu za kupita meli nyingine endapo meli iliyozana itaachwa hapohapo.

Marine Salvage kwa meli yenye tatizo hufanywa kwa kuivuta kwa kutumia tug ship, kuokoa mizigo na vifaa kwa kutumia crane za meli au kama imezama upande itafanywa ielee kwa kutumia maboya.

Kwa sasa kuna makampuni ambayo kazi yao ni kufanya uokozi tu, tofauti na zamani ambapo meli iliyokatika msukosuko ilitegemea kupata msaada baada ya kutoa ishara ya hatari(Distress Call/ Signal) kwa vyombo vilivyo karibu na ndege zitakazo pita eneo la karibu.

Namna ambavyo Marine Salvage Company hulipwa.
Meli itakayofanya marine salvage hutakiwa kulipwa asilimia kadhaa kulingana na thamani ya meli na mzigo uliopo.Kampuni itakayofanya Marine Salvage hulipwa kati ya Asilimia 5-25. Wengi hufanya kazi kwa malipo ya 25%.

Miaka ya nyuma kulikuwa na sheria inayosema uwezi kulipwa pesa ya kuokoa kama ukufanikiwa kuokoa kwa ukamilifu "No Cure, No Pay". Hii ilipelekea meli za mafuta zenye muundo wa ngozi moja(Single hulled Plate/Skin) kuogopwa kuokolewa hivyo sheria ikafanyiwa mabadiliko ili kusijetokea uchafuzi wa bahari na kuwa yeyote aliyeshiriki katika uokoaji atajaza fomu ya malalamiko na atalipwa fidia yake.

Aina za Marine Salvage
1. Contract Marine Salvage

Hii inafanyika baada ya kuandikishana mikataba baina ya meli iliyokatika dhoruba na waokoaji.

2. Pure Salvage
Hii hufanyika bila makubaliano baada ya uokoaji ndipo watu hukaa na kufanya malipo.

3. Naval Salvage
Hii hufanyika kwa vyombo na meli za jeshi la wanamaji baada ya kuwa katika dhoruba au baada ya kukamilika oparesheni.

4. Intelligent Salvage
Hii hufanya na taasisi za kijasusi kuchunguza kuhusu meli za jeshi za wanamaji wa nchi nyingine au manowari zilizozama ili kujua teknolojia au silaha vita.

Maeneo ambayo Marine Salvage huweza kufanyika ni eneo la bandari,eneo la bahari kuu,kutoa mabaki ya meli iliyozama,kutoa mizigo na vifaa na kusaidia meli kuelea.

images (2).jpeg
 
Daah Changamoto ni hao waokoaji had wafike itakua ni muda gan si itakua imezama yote, na vp kuhusu usalama wa wafanyakazi wa meli maana hizo boya na life jackets mi naona hazipo salama sana aseee.

Japo mimi siyo mtaalam wa bahari ila Kuna movie moja nlichek Kuna baadhi ya maeneo bahar usiku huwa inaganda barafu kabisa.
 
Daah Changamoto ni hao waokoaji had wafike itakua ni muda gan si itakua imezama yote, na vp kuhusu usalama wa wafanyakazi wa meli maana hizo boya na life jackets mi naona hazipo salama sana aseee.

Japo mimi siyo mtaalam wa bahari ila Kuna movie moja nlichek Kuna baadhi ya maeneo bahar usiku huwa inaganda barafu kabisa.
Mkuu hayo makampuni ya Marine Salvage huwa wanatumia meli zenye nguvu,kasi na vifaa vya kunyanyua vitu vizito(crane). Na hizi huwa zinakaa maeneo ya bahari na si bandarini huwa zinajitosheleza mahitaji yote au kuletewa na boti ndogo.

Meli ikiwa inazama wafanyakazi hubonyeza au kutoa taarifa ya hatari kwa kutumia VHF Radio,Mfumo wa Satellite (Inmarsat) kwa kutuma email ya hali ya hatari. Pia meli INA kifaa kinachoitwa Emergency Position Indicating Radio Beacon (EPIRB) hiki meli ikizama na kuingia kwenye maji kitajilipua na kutoa taarifa kwa meli na ndege zote zilizo jirani pia kwenye minara ya kuongozea meli.Search and Rescue Transponder (SART) nayo ipo katika meli huwa inajilipua kuonyesha wapi meli imezama au baharia anaweza akaivuta ikaji activate na kutoa taarifa.

Life jacket zipo salama toa hofu, maana zipo kulingana na idadi ya watu waliopo melini pia zimetengenezwa za watoto na wakubwa. Kazi kubwa ya Life Jacket ni kukufanya uelee kwenye maji kisha usubiri boti ya uokoaji.Hizo boya Nazo hutumika kusaidia uelee katika maji kwa kushikilia pembeni.

Kesi ya bahari kuwa na barafu hii unaweza kukutana nayo maeneo ya vizio vya dunia upande wa kaskazini na kusini. Huko ajali ikitokea au barafu ikizidi na meli kama haziwezi kupita huwa kuna meli maalumu za kuvunja mabarafu (Ice Breaker Ship) hupita kwanza kuvunja na meli za kawaida hufata nyuma kama msafara (convoy) katika uelekeo huo huo aliopita wa kwanza.
 
Back
Top Bottom