Marijani Rajabu alikuwa Mwanamuziki kipenzi cha Baba wa Taifa

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,685
11,988
Jabali la muziki Afrika Marijani Rajabu alikuwa na kipaji hasa mpaka sasa hatujapata mwanamuziki bora Tanzania kama Marijani Rajabu.

Alikuwa na sauti ambayo unatamani usikilize kila neno analoimba,alikuwa mwanamuziki mwenye ushawishi mkubwa kuanzia haiba yake hadi kukubalika katika jamii. Alikuwa kipande cha mtu.

Pamoja na kuwa kipindi kile Watu walikuwa na ushabiki wa kuwa wafuasi wa bendi za muziki km DDC Mlimani Orchestra, Dar Maquiz, Dar international, Moro Jazz nk. Lakini kuna wasanii waliojijengea majina binafsi mojawao akiwa Marijani Rajabu, huyu mtu amekuwa kwenye ubora wake hadi umauti unamkuta.

Hawa wanamuziki walikuwa watanashati hasa wasafi wa mwili na akili anaingia jukwaani yupo very smart, afro imesimama nywele safi. Mwanamuziki anapiga gita huku anaimba Achana na vijana wa siku hizi wanaopanda jukwaani huku wakiwa wameshika tupu zao.

Toka kizazi cha kina Marijani rajabu kimotoweka hakika Tanzania haijawahi kupata kizazi cha dhahabu hicho walikuja kina banza stone,mwinjuma, lkn hakikufua dafu mpaka sasa tumebaki na wasanii wasio jua nini maana ya mwanamuziki

Katika siku ya leo ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa mwalimu Nyerere, nakumbuka pia Mwalim alivyokuwa mfuasi sugu wa Marijani rajabu katika mikutano ya chama na serkali alikuwa akialiakwa na bendi yake kutumbuiza,
Marijani rajabu ameimba nyimbo nyingi za ukombozi wa Tanzania na Africa pia

Hakika huchoki kumsikiliza nyimbo zake,kama vile usivyochoka kusikiliza hotuba za Nyerere

R.I.P Baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere
R.I.P Marijani rajabu, jabali la muziki Africa
 
Jabali la muziki Africa Marijani rajabu alikuwa na kipaji hasa mpaka sasa hatujapata mwanamuziki bora Tanzania kama Marijani Rajabu.

Kipindi hicho mtu ulikuwa unajua muziki wa kitanzania ukoje. Kwa Afrika Mashariki na ya kati, ukiondoa iliyokuwa Zaire, Tanzania ilikuwa inatisha katika muziki. Tuli export wanamuziki mpaka nchi kama Kenya na wakawika sana. (Simba wa Nyika na matawi yake). Siku hizi muziki umekuwa ni kiki, kutembea na ma bodygurds na kutembea na wanawake wengi. Ukiambiwa muziki wa kitanzania ukoje unakuwa huna jibu.
 
Siku hizi ni uchafu mtupu Mkuu, kwenye santuri yangu Siwezi kutunza hizi nyimbo za wasanii wa siku hizi

Kipindi kile muziki wa Tanzania ulitikisa Africa ulikuwa unachuana vikali na muziki wa Congo

Na hii lipelekea wanamuziki wengi wa kikongo kuhamia nchini Tanzania kufanya shughuli za muziki
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom