Maridhiano ya Wazanzibari: Ufafanuzi wa taarifa za magazeti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maridhiano ya Wazanzibari: Ufafanuzi wa taarifa za magazeti

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MrFroasty, Jan 24, 2010.

 1. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  MARIDHIANO YA WAZANZIBARI: UFAFANUZI 24 Januari 2010

  Kutokana na kuwepo kwa wimbi la upotoshaji wa habari zinazohusu Maridhiano ya Wazanzibari katika vyombo mbali mbali vya habari, Kurugenzi ya Uenezi na Mahusiano na Umma ya Chama cha Wananchi (CUF) imeamua kutoa ufafanuzi ufuatao kwa makusudi ya kuweka rekodi sawa:

  1. Suala la Maridhiano haya ni la Wazanzibari wote kwa ujumla wao. Lolote zuri linalohusiana nayo ni kwa maslahi ya Wazanzibari wote; na sio kwa CUF tu au CCM tu. Vile vile kama litafeli au kufelishwa kwa makusudi, basi hasara yake itakuwa ni kwa Wazanzibari wote; na sio kwa CUF tu au CCM tu. Kwa sababu hiyo, ndiyo maana CUF kama Chama, haina lolote la kusherehekea au kulilia peke yake; kwani furaha au kilio cha Maridhiano haya ni kwa Wazanzibari na Watanzania wote kwa pamoja. CUF haijapanga sherehe wala kujiundia Baraza la Mawaziri; kwani hivyo ni vitu vidogo mbele ya maslahi ya nchi, ambayo CUF inasimamia

  2. Aina ya uandishi inayoshuhudiwa sasa katika vyombo vyetu vya habari inaashiria kwamba, aidha vyombo hivi havijaelewa malengo halisi ya Wazanzibari na au vinafanya kusudi kuzidhoofisha juhudi za Wazanzibari kujiandikia historia mpya. Huko ni kupotoka na ni kupotosha maadili ya uandishi wa habari, ambao unatakiwa sana kuzingatia maslahi ya umma. Maslahi ya Zanzibar ni makubwa na ya muda mrefu kuliko chochote na hilo ni vyema likafahamika hivyo

  3. CUF inaendelea kusimamia kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Jakaya Kikwete, juu ya Maridhiano hayo, ambayo ilitamka kwamba ni wajibu wa kila mmoja kuyaunga mkono na kumdharau yule anayeyabeza.

  Pamoja na salamu za Chama.

  Imetolewa na:
  Salim Bimani
  Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma, CUF
  Simu: +255 777 414 112
  Zanzibar
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Haya sasa...Wazanzibari ...wazanzibari.....Wazanzibari...!

  Tumewaelewa jamani na Zanzibari yenu, na harakati zenu za kuandika historia mpya za Zanzibar!

  Mi nawashangaa watu wanaokulazimisheni muitwe Tanzania-Bara, wakati at-least kwa sasa mna kila kitu chenu...Bendera, Wimbo wa Taifa etc, bado sarafu tu!!

  Bara nini bana!

  By ze way, all the best!
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Jan 24, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Naona bado hujaelewa taarifa ya CUF! Furaha au kilio ni kwa Wazanzibari na Watanzania WOTE! Sasa mbona unaleta ubaguzi wa makusudi na kuchochea chuki ndugu?
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Umesoma auunajifurahisaha?

  Ngoja nikupestie kichwa cha thread tena: Re: Maridhiano ya Wazanzibari:

  Nimekusaidia kuquote ili uone vizuri kilichowekwa originally na mleta thread, then ulinganishe na ulichotunga weye mkuu!
   
Loading...